Katibu
Mkuu wa Chadema,Dk Willbroad Slaa amedai kuwa anachukia udhaifu wa
utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete,kama kiongozi mkuu wa nchi na
katu hamchuki kutokana na dini yake kama watu wengine wavyopotosha.
Dk
Slaa aliyasema hayo jana kwenye maeneo ya Riroda,
Galapo,Mwada,Magara,Magugu,Mutuka,Sendo na Mamire,wilayani
Babati,mkoani Manyara na kudai kuwa hatanyamaza kamwe kwa kuwa
wananchi hawatendewi haki na matumaini yao yanaminywa na watawala.
Alisema
hatamung’unya maneno wala kusita kuendelea kusema udhaifu wa Rais
Kikwete hasa katika kushindwa kuchukua au kufanya uamuzi sahihi na
kwa wakati sahihi kwa sababu matokeo yake yanaathiri Watanzania wote
ambao yeye pamoja na chama chake wamejitolea kuwa wasemaji wao.
“Nchi
hii inavunjwa,napambana na Kikwete kwa sababu ni dhaifu,” alisema
na kuongeza:
“Kuna
watu wanapotosha jambo hili,mimi sina chuki na Rais Kikwete kwa
sababu ya dini yake”. Alisema.
Source
Mwanachi.
0 comments:
Post a Comment