Nilizaliwa
mkoa wa Dodoma na nilishi vizuri tu tangu utotoni na hata
sikujihusisha na ngono hadi nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada ya
kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi kwa mama mdogo aliyeolewa hapa
Mwenge.
Nilipata
marafiki wengi tu na kuna kijana mmoja alinitongoza kwa muda mrefu
sana na siunajua vijana wengi hutumia muda mrefu kutongoza ili
msichana unadhani kwamba labda huyo anakupenda kumbe anataka tu ngono
na wadada wengi sana hudhani kufuatiliwa kwa muda mrefu na mvulana
basi huyo yuko serious kumbe hakuna lolote.
Nilimkubalia
tukawa wapenzi ila nilikataa kuhusu kufanya mapenzi maana
anayekupenda kiukweli sio uongo lazima asitake ngono kabla ya ndoa.
Kwa
miezi kama 5 hadi 6 aliniambia kuhusu kufanya mapenzi nilikataa
alitumia mbinu nyingi sana kwa kunibembeleza na hata kulia mbele
yangu ili tufanye tu mara moja ila nilikataa, alisema atavumilia hadi
siku ya ndoa yetu ambapo tulipanga kuoana mwaka sept 2009.
Siku
moja aliniambia twende kwenye kumbi za starehe na mimi kwa sababu ya
upagani na kumwamini pia kwa sababu nampenda nilikubali tulienda huko
na kulikua na bendi fulani maarufu ya mziki wa dansi ilikua
inatumbuiza.
Tulitafuta
sehemu na kukaa na mpenzi wangu akaagiza pombe alianza kunywa huku
akinionjesha, nilikataa kwa sababu nilikua sijawahi kunywa pombe
katika maisha yangu yote, hata sijui alinishawishi vipi nilijikuta
nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa tulikaa pale kwa muda zaidi ya
masaa 5 nadhani nikunywa kama bia 3 au 4 japokua nilikua nakunywa
kidogo kidogo tu tena kwa kunywesha na mpenzi wangu maana nikama
nikua nanyweshwa kila baada kama ya dakika 25 ndipo nakunywa mara
moja na sikujuia kama nakunywa pombe ila niliihisi tu naonja ili
kumlizisha mpenzi wangu.
Ilipofika
saa 10 alfajiri nilihisi usingizi na pia nilijiona wa tofauti najua
nililewa hata kama sikujua kama nimelewa maana nakumbuka tulitoka
pale huku amenishika mkono huyo mpenzi wangu. Tulikodo tax na
kuondoka na siku hiyo aliniambia twende kwake alikokua amepanga
chumba maana tulikua na usingizi sana nilikubali huku nikidhani
hatuwezi kufanya mapenzi.
Tulifika
salama na kuingia ndani ukweli pombe ni kichocheo cha ngono na
ningekua mimi ndio Raisi wa Tanzania ningefunga bar zote. Nilijikuta
natamani kufanya mapenzi na huyu mpenzi wangu hata alikua hana nia
maana alijua atanichukiza sana na uhusiano ungekufa siku hiyo lakini
kwa sababu ya pombe nilimwambia siku hiyo tufanye kidogo maana mwili
wangu unataka.
Ni
kweli siku hiyo kwa sababu ya pombe nilifanya mapenzi na huyo mpenzi
wangu na baadae akanipeleka nyumbani baada ya wiki mbili maana
tulikaa wiki mbili bila kuonana alikuja na kunieleza habari ambayo
sikuihitaji katika maisha yangu maana nilikua nasikia tu kwa watu
wengine lakini sio kwangu alisema ”JANE ISHI KWA MATUMAINI KUANZIA
SASA”
Nilidhani
utani lakini aliniambia kuwa yeye ana UKIMWI tangu miaka mitano
iliyopita na anapenda tu ngono maana hawezi kuacha.
Nililia
sana na baada ya wiki moja baadae nikaenda kupima na kukutwa nina
ugojwa ambao niliusikia tu kwa watu na chanzo cha yote ni pombe,
kupenda starehe,disko na upagani unaotusumbua wanadamu wengi.
Nilikua
na UKIMWI na kwa hasira maana mpenzi wangu alihamia Arusha huku
akisema neno moja la mwisho kwamba ”shetani amemtuma kuwaambukiza
wanadamu UKIMWI”
Sikujua,
sikujua, sikujua, sikujuaaaaaaaaa, basi tu ooh YESU nihurumie mimi
leo.
Nilibebeshwa
mzigo ambao haukunistahili mimi. Hata leo hua najiuliza kwamba
nilijitunza kwa miaka 23 yote lakini pombe na huyu wakala wa shetani
wamenifanyia hivi. Baada ya kujua nina UKIMWI na hali hiyo
nikaikubali na kulikua na kundi kubwa sana la wanaume ambao walikua
wamewahi kunitongoja na niliwakataa sana kwa sababu hii niliwakubali
ili nami nife na wengi.
Nilianza
kumkubali kila mmoja na kuna baba mmoja ambaye ana wake 3 niliwahi
kumtukana sana kipindi cha nyuma kila aliponitongoza lakini wakati
huu nilimkubali na hakuamini na tukafanya ngono tena bila kinga na
akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya kumkubali kumbe naye hakujua
kuwa namwambukiza na hata leo hua nawahurumia tu wale wake zake ambao
wana UKIMWI uliotoka kwangu.
Kiukweli
tangu may 2009 hadi 2012 nimeshatembea na wanaume zaidi 1500 maana
ilifika kipindi nala na wanaume 3 kwa siku na lengo langu niwakomeshe
kama mimi nilivyokomeshwa na nina uhakika kutokana na mimi
wameambukizwa UKIMWI wanadamu zaidi ya 10,000 na hili tangazo la
”TUKO WANGAPI” huwa linaniliza kila siku maana hata mimi najua
kabisa nilianzisha mtandao kama huo wa ngono kwa idadi kubwa sana ya
watu.
Nimeokoka
miezi 7 iliyopita na siku naombewa nilikutwa na mapepo mengi sana na
hata waombeaji wakashangaa. Ningejua ningeokoka tangu nikiwa na miaka
5 lakini ndio hivyo sina jinsi wala uwezo wa kubadirisha hali hiyo.
Na
naomba kila atakayesoma ujumbe huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni
dhambi pia kwenda disko ni dhambi,kuuza pombe ni dhambi na kila
kichochoe chochote cha dhambi ni dhambi. Hadi sasa mtu yeyote hawezi
kujua kama nina UKIMWI na sijui MUNGU ana mpango gani na mimi maana
kwake yote yanawezekana. Nauamini uponyaji wake na sijawahi kutumia
ARV hata siku moja na afya yangu iko sawa tu na huwezi hata wewe
kujua kama uovu huu nimefanya mimi.
Ndugu
zangu kama una UKIMWI nenda kanisani ukaombewe na kama una akili mpe
YESU maisha yako maana pia baada ya kifo ni hukumu. Yasalimishe
maisha yako kwa YESU na usiambukize wengine tena.
Mimi
tangu niokoke sijawahi kufanya mapenzi tena na sitafanya hivyo wala
sitaolewa na mtu yeyote maana yatosha kwa uovu niliofanya na hadi
sasa wapo ninaowajua zaidi ya 15 wameshafariki na nilihudhulia
misibani huku nikijua kabisa chanzo ni mimi.
Mwisho
nawashauli wababa kulidhika na wake zao na wamama pia lidhikeni na
waume zenu, vijana ambao hamjaoa wala kuolewa subiri hadi utakapooa
au kuolewa na kabla ya kuolewa au kuoa kapimeni kwanza kwani wenye
UKIMWI ni wengi kuliko unavyozani.
Fuata
unachofundishwa kanisani na pia soma BIBLIA na uwe mtakatifu.
MUNGU
akubariki
Ni
mimi Jane,
Mwenge, Dar es salaam
Tanzania
Mwenge, Dar es salaam
Tanzania
Chanzo:
Jukwa huru
0 comments:
Post a Comment