Sunday, April 21, 2013

JUSTIN BIEBER NA SELENA GOMEZ:WAKUTWA WAKI KISS KISS



Mpango mzima umeanzia kwenye Ndege wakiwa wanaelekea Norway wiki iliyopita walengwa wakiwa wanaelekea kwenye concert ndipo walipoanza kuoneshana malovee mpaka maraia tukazinyaka.

hivi karibuni Selena Gomez alikuwa nyuma ya Stage katika Concert aliyoifanya Justin Bieber huko Oslo wiki hiyo ya jana lakini hali hiyo inaonesha kuwa walengwa hao wawili kuwa wamerudiana baada ya kukutwa waki Kiss huko Norway walipokwenda katika show.

Walikuwa wakishikana mikono,wakikumbatiana na kukiss mara kwa mara katika Lips kiukweli wal;ikuwa wakionekana kuwa ni wapenzi kama hakuna ugomvi ambao umewahi tokea siku za nyuma kati ya wawili hao hii ni dalili kuwa wamerudiana tena na kuwa wapenzi kwa mara nyingine.

Justin and Selena walivunja uhusiano wao mnamo mwaka 2012,lakini kwa wale waliokuwa karibu nao walikuwa wakidai wawili hao walikuwa wakiendelea kuwasiliana kipindi ambacho walikuwa katika ugomvi wao.
Wengine walikuwa wakidai kuwa Gomez alikuwa akimpigia sana na kumsumbua Bieber kwa simu na meseji za simu ingawa Bieber hakuwa teyari kuwa nae tena .




0 comments:

Post a Comment