Sunday, April 21, 2013

WASANII WA BONGO FLEVA NI KAMA TOILET PAPER


Ndiooo wakunielewa atanielewa na asietaka kunielewa shauri yake pia
Muziki wa Bongo fleva ni muziki uliopata mafanikio makubwa sanaa hapa nchini Kuanzia kwenye muziki wenyewe,wasanii na hata vyombo vya muziki kiukweli umekuwa mno.

Kupitia muziki wa bongo fleva Wasanii wamejiajiri na kufanya kazi ya sanaa kama kazi nyingine na kuwapatia vipato vizuri tuu,imefika wakati vijana hao wameweza kutoa ajira kwa vijana wenzao na kuwalipa kutokana na kipato wakipatacho katika kazi ya sanaa waifanyayo.

Kutokana na kukubarika kwa muziki wa bongo fleva na wasanii wa nyumbani kuwa juu katika jamii wasanii hao wamekuwa wakitumika kuhamasisha,kutuburudisha na kuelimisha pia viulevile wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya vyama vya siasa na wanasiasa kuhamasisha wananchi waweze kufika katika vikao vyao vya siasa na mikutano mikubwa.

Sasa hapa tujiulize kwanini nimewafananisha wanamuziki wa Bongo Fleva sawa na Toilet paper naamini kila mtu anatambua matumizi ya Toilet paper na ikisha tumiwa huwa haina matumizi mengine zaidi ya kutupwa,lakini tukumbuke kuwa hiyo Toilet Paper imenunuliwa kwa pesa hivyo ni sawa na wasanii wetu kwani wanatumiwa na baadhi ya vyama vya siasa pamoja na wanasiasa na kulipwa pesa zao lakini baada ya hapo hawapewi tena thamani mpaka wakati watapokuwa na maitahi yao tena.

Miaka nenda ludi wasanii wamekuwa wakilalamika juu ya masirahi ya kazi yao na namna wanavyonyonywa na kundi fulani la watu hivyo wamekuwa wakiomba serikali kuweka nguvu yake japo kuweza kujitoa katika wimbi kubwa la umasikini na unyonywaji wanaokutana nao lakini serikali haijawa sikivu kwao wala kusikia kilio chao,lakini viongozi hao hao wanawasujudu na kuwapigia makofi pindi mfanyapo kazi zao za kuwaleta watu uwanjani ili baadae waweze kuwadanganya na kunadi sera zao baada ya hapo dhamani ya msanii haitakuwepo tena.



Wasanii mnatumika kama ngazi ya kuwaweka wanasisa juu na kuweza kuwafanikishia mambo yao lakini wao mbona si watetezi wenu?mnakuwa na furaha kupata hizo pesa mzipatazo kwa siku kadhaa?au na nyinyi ni wasahaulifu kama walivyo wanasiasa wa bongo? 
 
Juzi hapa Mh Zitto kabwe yeye kaonesha nia ya kutaka kuwasaidia maana anajua matatizo yanayowakumba kama wasanii lakini hoja ilipoingia serikalini ilipigwa danadana na kuwatetea wawekezaji.

Baada ya hapo wasaniii mlionesha kukelwa na hali hiyo kiasi kwamba baadhi yenu mlikumbuka kazi mnayoifanya katika kampeni zao na mikutano yao kama si makongamano mpaka nikahisi sasa inaweza kuwa basi mfano Diamond Platinum uliandika kuwa wanasiasa wanawapeni kipaumbele pindi wawapo na shida hivyo nilitegemea ungetia ngumu ilikuonesha msimamo wenu kama wasanii katika kupigania haki zenu lakini jana umeibuka tena morogoro na kuendelea kuwatengenezea maisha wanasiasa jamani njaaa mbaya kuweni na msimamo msipelekwe kama gari bovu.


0 comments:

Post a Comment