Tulianza kusikia wimbo wa JOTO HASIRA aliofanya Jaydee pamoja na Prof JEEZY ambao kwa namna moja wimbo ule umeeleza namna mtu atumiapo nafasi yake kuhakikisha mtu mwingine hanufaiki japo katika kutafuta walikuwa pamoja lakni baada ya wimbo huo kutoka nilitegemea kuusikia kwanza kupitia Redio ya Watu Clouds Fm kwani ndio Radio iliyokuwa ikitambulisha nyimbo za dada yetu kwa mara ya kwanza lakini haikuwa hivyo nilijiuliza kunaniiii?
Mpango nilianza kuulewa baada ya dada Yangu kuanza kutiririka na kuweka wazi yaliomkuta na baadhi ya viongozi wa Redio hiyo ikiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho cha Redio,Lakini mwanzo alitumia lugha ya mficho kusema yaliyopo moyoni mwake japo imefika wakati JOTO HASIRA IMEPANDA na kuamua kuweka wazi kila jambo.
“Wote mnafahamu msemo wa Mungu si Athumani, si ndio? Mie nina wangu mpya,Naamini kabisa kuwa Mungu sio Ruge wala Kusaga. Atanisimamia kwenye hili
maneno haya yananipa picha kuwa hata wafanye wawezavyo au watumie njia wawezazo lakini kila jambo linapangwa na mungu hapa nahisi ndicho alichomanisha mwanadada Jaydee.
Siku mbili tatu zilizopita Kaka yangu Saley Ally aliandika makala juu ya Lady Jaydee ilisomeka LadyJaydee MNAFIKI WA MIAKA 10,SHUJAA WA MWEZI MMOJA.
baada ya kuandika makala hiyo Lady Jaydee alifunguka juu ya Mwandishi wa Habari za michezo Tanzania na kumtuhumu kuwa ni mtu wa Ruge hivyo anatumiwa na Ruge katika kutaka kumsafisha na kumchafua LadyJaydee hivyo amesema
“Huyo Saleh pia si alimsema Shigongo mbona alirudi nyuma na kufanya kazi kwake? Nafahamu pia ni mtu wa Ruge hivyo hanisumbui,Hajui tulichokipitia na tulichovumila anadhani tulikuwa tunaogelea mfereji wa maziwa na asali, km ni kuzuri mbn watu tumetoka,Then anajiita mwandishi halafu anatoa habari ambazo hana uhakika nazo. Bullshit”
La msingi wakianza kukuchanganya we vuruga inakuwa uji, Mnachanganyikiwa wote then kila mtu anatafuta tiba ya ukichaa kivyake muda unapita
Naamini kabisa kuwa Mungu sio Ruge wala Kusaga. Atanisimamia kwenye hili
0 comments:
Post a Comment