NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Siku ya leo akikujia mtu kukuaga kwamba anahama au anakwenda safari ambayo itamchukua muda mrefu, hiyo ni dalili kwamba yule ambaye unamuhisi ni mbaya wako basi ni kweli. Tegemea kupata marafiki wengi wapya leo.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Siku hii ya leo Mwanamke akikutana na mtu analima, hiyo ni dalili ya kukutana na mtu anayefanya kazi ya ukarani ambaye atamtaka na atakuwa mpenzi au mume mzuri sana katika mapenzi au ndoa yao.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Siku hii ya leo uki pata salamu kutoka kwa Mzazi wako wa kiume au akija ghafla au ukikutana naye njiani, basi ujue hiyo ni dalili kwamba kuna habari nzuri za upendo utakazopata leo. Jaribu kufanya utafiti wa mambo yako kabla hujachukua hatua.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Siku hii ya leo ukikutana na Baba Mkwe wako, hiyo ni dalili mbaya kwako, leo utadanganywa, utatishwa au utapigwa bila sababu na mipango yako yote leo itakwama, kama una mgonjwa aliye hospitali atakufa.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Siku hii ya leo ukikutokea ukafanya kosa lolote ambalo ukalijutia, hiyo ni dalili kwamba utapendwa sana na wale unaowafahamu zaidi. Utapendwa kwa sababu ya busara zako hata wale wanaokuchukia watakukubali.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Siku hii ya leo ukikutana na mtu mwenye wasiwasi wa jambo lolote, hiyo ni dalili kwamba utapata habari nzuri kutoka kwa Wakili wako kwamba kuna ndugu yako amekuachia mali au fedha ili upewe uyamalize matatizo yako yanayokusumbua..
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Siku hii ya leo ukiuona Unyoya Unapeperuka angani, hiyo ni dalili ya kwamba utapata wasiwasi kuhusiana na mtu unayemuamini na ni dalili vile vile kwamba watu wanaokudai wameamua kukuisamehe deni lako..
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Siku ya leo katika shughuli zako ukimuona Mwanamke anamlisha mtoto, au mtu anamlisha mgonjwa, hiyo ni dalili kwamba leo mambo yako ya kikazi yatakuwa mazuri mipango yako ya fedha itatimia na watoto wako watapata mambo uliyotaka wapate.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Siku ya leo ukiwa katika mizunguko yako ukakuta sehemu kuna Sherehe, hiyo ni dalili kwamba mtoto wako ataugua na kuvuruga mipango yako na utavunjiwa heshima na rafiki yako ambaye hana heshima au wewe utapata maradhi ya kuumwa na kichwa.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Siku hii ya leo ukimwona mtu anawanywisha Wanyama maji, basi ujue hiyo ni dalili kwamba kuna habari za uongo utaambiwa na Mkeo au Mpenzi wako kuhusiana na biashara zako. Jaribu kufanya uchunguzi kabla hujachukua hatua.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku hii ya leo ukikutana na mtu anamwaga Majivu, hiyo ni dalili kwamba mgonjwa wako aliye hospitali atapona au utaletewa habari ya nzuri za kupona ugonjwa wa mzazi wako wa kiume
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Hii leo ukikutana na mtu na akakwambia habari ukahisi anakudanganya, hiyo ni dalili ya kupata habari nzuri zinazohusiana na mtu ambaye unampenda sana.ni siku nzuri ya kufanya biashara zako
0 comments:
Post a Comment