Watu wanao sadikiwa kuwa ni majambazi wameua na kupora fedha taslimu zaidi ya millioni kumi jijini dar es salaam.
Tukio
hilo limetokea mchana wa leo jijini dar es salaam baada ya wati hao
kumpiga risasi mwanamke mmoja ambae jina lake halijafahamika kwa
haraka na kusababisha kifo chake hapo hapo na kupora fedha zaidi ya
milioni kumi.
Kwa
mujibu wa chanzo kisicho rasmi kilisema kuwa mwanamke huyo alikuwa
ametoka katika Bank ya CRDB tawi la Uhuru na kuvamiwa na majambazi
hao waliokuwa wakitumia usafiri wa bodaboda baada ya kuligonga gari
alilokuwa akilitumia dada huyo,alipotoka nje ya gari ili kujionea
namna gari lake lilivyohalibika ndipo walipompiga risasi na kupora
pesa hizo na kutoweka kusiko julikana.
Mwanamke
huyo amepigwa risasi kifuani na kusababisha kifo chako hapo hapo.
0 comments:
Post a Comment