Mbunge
wa Jimbo la bumburi na Naibu Waziri wizara ya mawasiliano nchini Mh
Januari Makamba ametoa kauli yake dhidi ya vita ya kimuziki
iendeleayo kati ya Viongozi wa Clouds media na msanii wa muziki Lady
jaydee.
kauli
hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa Facebook leo baada ya kiongozi
mmoja muandamizi wa Radio hiyo kutumia muda mwingi kuzungumzia suala
la kupigwa kwa nyimbo au kutopigwa kwa nyimbo katika vituo vya Redio
mbalimbali,Mh Makamba alilifananisha suala hilo ni sawa na kukosa
uzalendo katika taifa kama tanzania linalo kabiliwa na matatizo mengi
ya msingi na yenye kuihitaji kutatuliwa na kutafutiwa ufumbuzi.
“Kama
Taifa tunayo matatizo makubwa zaidi ya kujadili na kutafuta ufumbuzi
zaidi ya kutumia muda mwingi kujadili ni nyimbo za nani zinapigwa
kwenye redio stesheni hii au ile na za nani hazipigwi”
MTIZAMO
WANGU KWA KAULI YA RUGE “MSIPIGE BONGO FLEVA”
katika
Mazungumzo aliyoyafanya Kiongozi wa Redio ya Clouds Fm Ruge Mutahaba
katika kipindi cha Power Breakfast alimaliza kwa kutoa amri kwa
wafanyakazi wa Redio hiyo kutocheza muziki wa bongo Fleva siku ya leo
na amefanya hivyo kuonesha nguvu yake kama Ruge kuwa anaweza kufanya
chochote na wakati wowote katika Redio hiyo hivyo kwangu mimi naona
kweli si mahitaji ya watu kusikiliza kile alichoamrisha boss huyo.
Nikuache
na swali kidogo KWA KAULI HIYO CLOUDS FM NI REDIO YA WATU?
NA
je kama wasanii wa bongo fleva nao wakiweka mgomo kwa nyimbo zao
kutochezwa katika kituo hicho nini kitatokea?
Muda
mwingine Busara ndiyo jibu kwa matatizo.
0 comments:
Post a Comment