Kiungo
mshambuliaji kutoka Timu ya Azam Fc alimaarufu kam Uhuru Seleman
Mwambongo baada ya kumaliza msimu wa Pili wa Ligi kuu bara akiwa na
Timu ya Azam Fc amewataka mashabiki wake wamchagulie timu ya kwenda
kucheza msimu ujao huku akiwa ametaja timu nne tu Simba Sc,Coastal
Union.Azam Fc na Tusker Fc.
“Leo ni Tarehe 24 May nisiku ambayo namaliza miezi sita ndan ya Azam ... Na nakupa nafasi wewe kama shabiki wangu kuchagua msimu ujao nicheze timu (gani) vigezo na hekima .... 1.Simba sc .2.Coastal 3.Azam fc 4.tusker fc”
Mbali
na kuwapa vigezo hivyo mashabiki wake lakini amewaomba kutumia hekima
katika kumshauri acheze timu ipi,nilipofanya utafiti wangu nikagundua
kuwa mashabiki wengi wa Simba Fc walimtaka Uhuru arejee nyumbani kwa
kujiunga na timu hiyo aliyokwisha ichezea kipindi cha nyuma kabla ya
kujiunga na Azam Fc,na yeye alikili hilo na kusema kuwa wengi wape.
Kwa
mtazamo huo inawezekana msimu ujao uhuru akalejea kuichezea timu ya
Simba Sc kwani ameonesha mapenzi hayo dhahiri kwanza kwa kuipa nafasi
ya kwanza katika list ya timu alizozitaja pili katika list hiyo
hajaitaja kabsa Yanga hivyo inawezekana hawajaonesha uitaji au laah
hajapenda kuungana na timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment