Katika
ule mpango wa kuhakikisha vijana wanashika Mic na kuchana mistari yao
na kuonesha vipaji vyao kupitia Marcho Chali Foundation unaokwenda
kwa jina Epic Open Mic wasanii kama Diamond Platinum,Madee,Ney wa
Mitego na Godzillah wataonesha uwezo wao bure katika viwanja vya
Mwembe Yanga pande za Temeke Jumapili hii.
Kwa
mujibu wa Marcho Chali amesema kuwa lengo la Epic Open Mic ni
kuwakuza wasanii wadogo ili kufikia malengo yao na kuwa wasanii
wakubwa na kupewa misingi mizuri ya kuwa wasani bora katika fani ya
kuimba kama walivyo wasanii wengine.
Aliongeza
kuwa kama kama wewe ni msanii na una ndoto ya kuja kuwa msanii
mkubwaaa bhasi hakuna sehemu nyingine inayoweza kukupa nafasi
kirahisi kama Epic Open Mic.
“kama
wewe ni msanii na una ndoto ya kuja kuwa msanii mkubwaaa … EPIC
OPEN MIC inakuhusuuu”.
Wakali
hao wa Bongo wanaotamba na ngoma zao kibao wataanza kukisanua mida ya
saa nane mchana mpaka time ile ya kumi na mbili za jioni huku wasanii
wadogo wenye lengo la kuwa kama wao wakishuhudia nini kaka zao
wakifanya na ikifika wakati wao nao watapewa nafasi ya kufanya yao
pia.
0 comments:
Post a Comment