Wanawake
wawili wakazi wa Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam waliofahamika
kwa majina ya Nasra Omari (36) na Mwanaisha Kapama (36) walikutwa na
maiti
iliyokuwa na dawa za kulevya aina ya heroin pipi 33 zenye
thamani ya mamilioni ya fedha.
Kamishna
Kova alisema alipata taarifa kuwa kuna mtu aliyefahamika kwa majina
ya Rajabu Kidunda na Mashaka Mabruki (43) ambaye ni
mfanyabiashara aliyefika Dar es Salaam kutoka mkoani Mtwara kwamba
alifariki dunia ghafla muda mfupi baada ya kutoka bafuni
kuoga.
Baada ya kufikishwa Hospitali walipoipasua maiti walikuta pipi hizo zenye urefu wa sentimita sita.
Baada ya kufikishwa Hospitali walipoipasua maiti walikuta pipi hizo zenye urefu wa sentimita sita.
uchunguzi unaonyesha kuwa marehemu alifika Dar es Salaam kutoka Mtwara Septemba 21 mwaka huu kwa maelezo kwamba alifika kwa ajili ya matibabu kwa kuwa alikuwa mgonjwa.
Hata hivyo, mtu huyo alifariki siku hiyo hiyo aliyowasili jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment