Wednesday, September 25, 2013

HAYA NDIO MAAMUZI YA YANGA KWA MRISHO NGASA.

Baada ya Ngasa Mwenyewe kushindwa kulipa deni la Millioni 45 Kwa Club yake ya Zamani ya Simba kama ambavyo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
Shirikisho la Soka nchini (TFF),ilivyomtaka Ngasa kuzilipa kama adhabu na kutocheza mechi sita msimu huu pamoja na baada ya usajili wake kuleta utata kutokana na kujisajili klabu mbili tofauti, Simba na Yanga.

Jana Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa, wapo tayari kumsaidia Ngasa kulipa deni hilo ila kwa masharti mawili.

"Kwanza akubali kukatwa kiasi hicho kidogo kidogo katika mshahara wake  hadi deni hilo litakapomalizika, au laah aridhie kuingia mkataba mwingine wa miaka mitatu," alinukuliwa Mwalusako.

Mmoja wa rafiki wa karibu wa Mchezaji huyo amesema kuwa Mpira ni Maisha ya Mrisho ngasa hivyo hawezi kupingana ma maamuzi ya Club yake ya Yanga.

"Soka ni maisha yake. Amesema hana ujanja wa kupindua uamuzi huo kwa kuwa kinyume na kufanya hivyo, itamlazimu kuendelea kukaa benchi hadi atakapolipa deni hilo la Simba kama alivyotakiwa kufanya na Kamati ya TFF," alisema rafiki huyo huku akiomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa yeye si msemaji wake.

0 comments:

Post a Comment