Friday, April 12, 2013

KUSHUKA KWA KIWANGO CHA ELIMU TANZANIA RIPOTI HII HAPA.



source Jamii Forums.com

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NA OFISI YA
WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA YA UTAFITI
KUHUSU KUSHUKA KWA KIWANGO CHA
UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO
CHA 4 MWAKA 2010
Dar Es Salaam
Juni, 2011
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
i
SHUKRANI
Utafiti huu umehusisha wataalamu mbalimbali katika hatua za kubuni, kutayarisha,
kukusanya, kuchambua takwimu na kuandika ripoti. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
kwa pamoja zinawashukuru wataalamu wote waliohusika kwa njia moja ama nyingine
katika hatua mbalimbali za utafiti huu. Pia tunawashukuru wadau wote wa elimu
waliohusika katika kutoa taarifa za utafiti. Aidha shukrani za pekee ziiendee Wizara ya
Fedha kwa kufanikisha mchakato mzima wa utafiti.
Shukrani pia zimwendee Bwana Jumanne Abdallah Sagini, Naibu Katibu Mkuu -
TAMISEMI kwa kuwa msimamizi mkuu wa kazi hii. Aidha, shukrani za dhati ziwaendee
wajumbe wa kikundi kazi kilichohusika katika utafiti huu kuanzia hatua za awali hadi
mwisho. Wajumbe hao ni:
JINA TAASISI WADHIFA
1. Francis M. Liboy OWM-TAMISEMI - Mwenyekiti
2. Lawrence John Sanga WEMU - Katibu
3. Fred Davidson Sichizya WEMU - Mjumbe
4. Abdallah Shaban Ngodu WEMU - Mjumbe
5. Hadija Mchatta Maggid WEMU - Mjumbe
6. Paulina Jackson Mkoma WEMU - Mjumbe
7. Elia Kalonzo Kibga WEMU - Mjumbe
8. Paulina Mbena Nkwama OWM-TAMISEMI - Mjumbe
9. Makoye J.N. Wangeleja TET - Mjumbe
10.Edward Simon Haule NECTA - Mjumbe
Aidha shukrani zimwendee Mkurugenzi Mkuu wa TET kwa kugharamia vikao vya kikundi
kazi kupitia huduma ya ukumbi na chakula wakati kikiwa Dar-es-salaam.
Prof. Hamisi O. Dihenga
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
ii
DIBAJI
Ripoti hii ya utafiti inahusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa Kidato
cha 4 mwaka 2010. Utafiti huu umefanywa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu-
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi (WEMU) ikihusisha Taasisi ya Elimu Tanzania na Baraza la Mitihani la
Tanzania.
Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa
Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri kwa
wadau wa elimu Serikali iliamua kufanya utafiti ili kuweza kubaini chanzo na ukubwa wa
tatizo. Utafiti huu unatoa mapendekezo kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu na ubora wa
elimu ya sekondari.
Ripoti hii inaonesha kwamba yapo masuala ya kimfumo, mfano mapungufu katika
usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini ambayo yanaweza kutatuliwa na serikali moja
kwa moja. Aidha, yapo masuala yanayohusu kujenga uwezo kwa wasimamizi na
watekelezaji wa mitaala, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa bora na vya kutosha vya
kufundishia na kujifunzia na uboreshaji wa majengo na miundombinu ambayo
yanahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wabia wake.
Matokeo ya utafiti huu ni muhimu kwa serikali, washirika wa maendeleo na wadau
mbalimbali wa elimu kwani inaonesha chanzo na ukubwa wa matatizo na changamoto
zinazojitokeza na inatoa mapendekezo ya namna ya kuyatatua na kukabiliana na
changamoto za kielimu. Hivyo sote kwa pamoja yatupasa tujipange na kuelekeza nguvu
zetu kupitia mipango yetu ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili tuweze
kuyamaliza matatizo haya na kuinua ubora wa elimu nchini.
Ninawaomba wadau wa elimu nchini kuyafanyia kazi matokeo ya utafiti huu ili kuweza
kupiga hatua katika utekelezaji wa utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi. Serikali inayo
nia ya dhati ya kutekeleza mapendekezo haya ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu
ya sekondari nchini.
Mh. Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (MB)
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
iii
YALIYOMO
SHUKRANI............................................................................................................................................ i
DIBAJI................................................................................................................................................... ii
VIFUPISHO........................................................................................................................................... v
MUHTASARI PEMBUZI..................................................................................................................... vi
SURA YA KWANZA: UTANGULIZI................................................................................................ 15
1.1. Usuli ...................................................................................................................................... 15
1.2. Hoja ya Kufanya Utafiti ....................................................................................................... 18
1.3. Malengo ya Utafiti................................................................................................................ 19
1.4. Maswali ya Utafiti................................................................................................................. 19
1.5. Muundo wa Ripoti................................................................................................................ 20
SURA YA PILI: MAPITIO YA MAANDIKO.................................................................................... 21
2.1 Sera na Mipango ya Elimu.................................................................................................. 21
2.2 Mipango na Mikakati ya Elimu ........................................................................................... 22
2.3 Uongozi katika Elimu ........................................................................................................... 23
2.4 Usimamizi na Uendeshaji.................................................................................................... 24
2.5 Ugharamiaji wa Elimu ......................................................................................................... 25
2.6 Ufuatiliaji na Tathimini ya Elimu........................................................................................ 27
SURA YA TATU: MWONGOZO WA UTAFITI............................................................................... 55
3.1. Utangulizi .............................................................................................................................. 55
3.2. Mbinu ya Utafiti .................................................................................................................... 55
3.3. Eneo la Utafiti ....................................................................................................................... 56
3.4. Uchaguzi wa Sampuli .......................................................................................................... 56
3.5. Zana za Utafiti ...................................................................................................................... 57
3.6. Utaratibu Uliotumika Kufanya Utafiti ................................................................................ 58
3.6.1. Kukusanya Taarifa Kutoka Ngazi ya Taifa ................................................................ 58
3.6.2. Kukusanya Taarifa Kutoka katika Kanda, Mkoa na Halmashauri .......................... 58
3.6.3. Kukusanya Taarifa Kutoka Shuleni na katika Jamii................................................. 59
3.7. Uchambuzi wa Data............................................................................................................. 59
3.8. Maadili ya Kufanya Utafiti................................................................................................... 59
SURA YA NNE: MATOKEO YA UTAFITI NA UCHAMBUZI WA DATA................................... 61
4.1. Utangulizi .............................................................................................................................. 61
4.2. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu .................................................................................. 63
4.2.1. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Ngazi Mbalimbali................................. 63
4.2.2. Mmomonyoko wa Maadili Katika Jamii...................................................................... 68
4.2.3. Mwamko Duni wa Jamii Katika Elimu........................................................................ 69
4.2.4. Siasa Kuingilia Masuala ya Kitaalam ya Kielimu....................................................... 69
4.2.5. Ufinyu wa Bajeti ya Elimu ........................................................................................... 70
4.2.6. Maoni Kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu ................................................. 71
4.2.7. Mapendekezo kwa Walioshindwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 Mwaka
2010 75
4.3. Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala ............................................................................. 76
4.3.1. Utayarishaji wa Mitaala................................................................................................ 76
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
iv
4.3.2. Uwepo wa Mihtasari Shuleni na Vyuoni.................................................................... 77
4.3.3. Utekelezaji wa Mtaala .................................................................................................. 78
4.3.4. Mafunzo Kabilishi kwa Ajili ya Mtaala Ulioboreshwa ............................................... 79
4.3.5. Maoni Kuhusu Utekelezaji wa Mtaala ........................................................................ 79
4.4. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa........................................................................... 80
4.4.1. Utungaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 ....................................................... 80
4.4.2. Usambazaji na Usimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4.......................... 82
4.4.3. Usahihishaji wa Mtihani ya Taifa wa Kidato cha 4 .................................................. 83
4.4.4. Mchango wa Alama za Mazoezi Endelezi (Continuous Assessment-CA)
Katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4................................................................................ 85
4.4.5. Upangaji wa Madaraja Unaofanywa na NECTA ....................................................... 86
4.4.6. Matumizi ya Miongozo na Nyaraka Mitihani ............................................................. 88
4.4.7. Athari za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2............................................................ 88
4.4.8. Maoni Kuhusu Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa ......................................... 90
4.5. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu ................................................... 93
4.6. Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu............................................................... 97
4.6.1. Mfumo wa Utayarishaji wa Walimu............................................................................... 97
4.6.2. Ajira na Upangaji wa Walimu ..................................................................................... 98
4.6.3. Uwepo wa Walimu katika Shule .................................................................................. 100
4.6.4. Maoni ya Kuimarisha Ubora na Uwepo wa Walimu .............................................. 106
4.7. Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia ........................................................ 108
SURA YA TANO: HITIMISHO NA MAPENDEKEZO.................................................................. 115
5.1. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu ................................................................................ 115
5.2. Utekelezaji wa mitaala ...................................................................................................... 118
5.3. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa......................................................................... 119
5.4. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu ................................................. 121
5.5. Mfumo wa utayarishaji wa walimu.................................................................................. 121
5.6. Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia.......................................................................... 124
REJEA ............................................................................................................................................... 126
VIAMBATISHO ............................................................................................................................... 130
Kiambatisho Na. 3.1: Maeneo Yaliyohusika katika Utafiti ...................................................... 130
Kiambatisho 3.5: Zana na Idadi ya Wajibuji Kitaifa na Kimkoa........................................... 132
Kiambatisho 4.1 – Takwimu za ukaguzi wa shule ( 2007–2010) katika Halmashauri
zilizofanyiwa utafiti....................................................................................................................... 133
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
v
VIFUPISHO
BEST Basic Education Statistics in Tanzania
CA Continuous Assessment (Mazoezi Endelezi)
CG Capitation Grant
CDTI Community Development Training Institute
CWT Chama cha Walimu Tanzania
EFA Education for All
EMAC Educational Materials Approval Committee
ETP Education and Training Policy
FDC Folk Development College
FTC Full Technician Certificate
GBS General Budget Support
GDP Gross Domestic Product
GER Gross Enrolment Rate
MKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania
MMES Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari
MEMK-WSM Mkakati wa Elimu ya Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Shule za
Msingi
MMEM Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi
MMEMWA Mkakati wa Menejimenti na Maendeleo ya Walimu
MoEVT Ministry of Education and Vocational Training
MWAKEM Mafunzo ya Walimu Kazini Elimu ya Msingi
MTEF Medium Term Expenditure Framework
MDGs Milemium Development Goals (Malengo ya Maendeleo ya Milenia)
MUCE Mkwawa University College of Education
NCDF National Curriculum Development Framework
NECTA National Examinations Council of Tanzania
OC Other Charges
OUT Open University of Tanzania
OWM-TAMISEMI Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
PETS Public Expenditure Tracking System
SEDP Secondary Education Development Programme
TAMONGSCO Tanzania Association of Managers of Non Government Schools and
Colleges
TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
TET Taasisi ya Elimu Tanzania
TEN/MET Tanzania Education Network/Mtandao wa Elimu Tanzania
TES Tanzania Elimu Supplies
TIE Tanzania Institute of Education
TSD Teachers Service Department (Idara ya Huduma kwa Walimu)
UKIMWI Ukosefu wa Kinga Mwilini
URT United Republic of Tanzania
TRC Teachers Resource Centre
UPE Universal Primary Education (Elimu ya Msingi kwa Wote)
WEMU Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
vi
MUHTASARI PEMBUZI
Utoaji wa elimu nchini Tanzania unaongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo (ETP) ya
mwaka 1995. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo unaenda sambamba na Dira ya
Taifa 2025, MKUKUTA, kutimiza malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo ya
Maendeleo ya Milenia (MDGs).
Katika kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu
ilianzishwa. Aidha, Programu za Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na
Sekondari (MMES) zilianzishwa kutekeleza program ya sekta. Mafanikio ya MMEM
yameongeza mahitaji ya upanuzi wa elimu ya sekondari, ambapo Mpango wa
Maendeleo ya Elimu ya Sekondari – MMES I (2004-2009) ulitekelezwa kwa lengo kuu la
kuongeza uandikishaji wa wanafunzi katika shule za sekondari na MMES II (2010-
2014) imeweka kipaumbele katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari.
Kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka kila
mwaka kwa mfululizo wa miaka minne 2007 (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na
2010 (50.4%). Kutokana na hali hiyo, Serikali iliamua kufanya utafiti ili kubaini sababu
za kushuka kwa kiwango cha ufaulu na kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na tatizo
hilo.
Utafiti huu ulifanyika katika mikoa 11, ikiwa ni mmoja kwa kila Kanda ya Elimu. Aidha,
jumla ya Halmashauri 22 zilihusishwa, mbili kutoka kila mkoa ikiwa moja iliyofanya
vizuri na nyingine iliyofanya vibaya katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Kwa kila
Halmashauri jumla ya shule sita zikiwemo nne za serikali na mbili zisizo za serikali
zilihusika katika utafiti huu. Jumla ya shule 132 ambapo 88 ni za Serikali na 44 ni
shule zisizo za Serikali zilihusishwa. Pia, ofisi za elimu na ukaguzi wa shule, Taasisi ya
Elimu Tanzania (TET), Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), pamoja na baadhi ya
asasi za serikali na zisizo za serikali zilihusishwa. Jumla ya wajibuji 3,894 walilengwa
katika utafiti ambapo washiriki 3,037 sawa na asilimia 80.0% walifikiwa.
Taarifa na takwimu za utafiti zilikusanywa kwa kutumia Madodoso, Majadiliano ya
Pamoja, Hojaji, maandiko na makala mbalimbali. Uchambuzi wa takwimu umefanyika
kwa kuwasilisha hoja za wajibuji katika namba (asilimia), majedwali na chati ili kuleta
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
vii
taarifa zenye mantiki kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti kuhusu
kushuka kwa kiwango cha ufaulu cha Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 2010
yamewasilishwa kama ifuatavyo:-
a) Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu
Utafiti umedhihirisha kuwa matatizo yanayohusu usimamizi na uendeshaji
yameathiri ufanisi katika utoaji wa elimu bora nchini. Baadhi ya viongozi wa
elimu huteuliwa bila kuzingatia utaalamu, taaluma, uwajibikaji, uwezo na
uadilifu. Aidha, maamuzi ya kitaalamu kuhusu uendeshaji wa elimu hufanyika
kisiasa bila kuzingatia utaalamu na tafiti. Vile vile ufinyu wa bajeti ya Wizara ya
Elimu na TAMISEMI (Elimu) unafanya usimamizi na uendeshaji wa elimu
kutokuwa fanisi.
Utekelezaji wa Sera ya matumizi ya vitabu vingi vya kiada na ziada umekuwa na
changamoto ambazo zimeathiri uchapishaji, usambazaji na upatikanaji wa vitabu
vyenye ithibati katika shule na vyuo. Aidha, kuna uelewa mdogo kwa wanafunzi
na walimu katika matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia na kujifunzia
katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu.
Utafiti umebaini kuwa, mmomonyoko wa maadili kama vile matumizi ya lugha
mbaya; matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),
kutozingatia mafundisho ya dini, matumizi ya dawa za kulevya na kujiingiza
katika masuala ya mapenzi ni masuala yaliyobainishwa kuchangia kumeathiri
maendeleo ya taaluma shuleni.
b) Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala
Utafiti umeonesha kuwepo kwa changamoto za utayarishaji na utekelezaji wa
mtaala kwa miaka mitano iliyopita. Mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2005
umetekelezwa bila kufanyiwa majaribio (piloting). Aidha, utafiti umebaini kuwa
kwa miaka mitatu iliyopita (2008 hadi 2010), jumla ya walimu 588 (1.5%)
walipata mafunzo kabilishi. Taarifa hii inaonesha kuwa walimu wengi hawana
maarifa na stadi za kufundisha mtaala wa sekondari uliboreshwa.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
viii
Ni muhimu watekelezaji mitaala kupatiwa mafunzo kabilishi ili kuimarisha
utendaji kazi wao na kuwawezesha kupata fursa ya mabadiliko ya mtaala, dhana
na nadharia za ufundishaji na ujifunzaji.
Pia, utafiti umebaini upungufu wa mihtasari ya mtaala ulioboreshwa katika shule
za sekondari. Katika shule zilizofanyiwa utafiti, takwimu zinaonesha kuwa kuna
upungufu wa mihtasari kwa wastani wa asilimia 45.4 ambapo masomo ya
Mathematics na Geography yameongoza kwa kuwa na upungufu wa zaidi ya
asilimia 50. Vilevile, kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa mihtasari kutoka
TET kwenda shuleni.
c) Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu
Utafiti huu ulilenga Kuchunguza ufanisi wa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya
utoaji wa elimu, utekelezaji wa mtaala na ukaguzi wa shule.
Utafiti ulibaini kuwa asilimia 49 ya wakuu wa shule hawafuatilii kikamilifu utoaji
wa taaluma shuleni, hali hii inapunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.
Hivyo inapaswa wakuu wa shule wasimamie kikamilifu majukumu yao kama
ilivyoainishwa katika Mwongozo wa Usimamizi wa Shule.
Aidha, ilibainika kuwa hakuna ufuatiliaji wala tathmini iliyofanyika tangu mtaala
wa elimu ya sekondari ulioboreshwa uanze kutumika mwaka 2005 na kwamba
mitaala hiyo haikufanyiwa majaribio kabla ya utekelezaji wake. Kutofanya
tathmini kwa wakati kuhusu utekelezaji wa mtaala hakutoi fursa kwa serikali na
wadau wa elimu kubaini matatizo na changamoto za utoaji elimu na kuyapatia
ufumbuzi kwa wakati na hivyo kupunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji
Pia utafiti umebaini kuwa, katika shule 132 zilizotembelewa, shule 18 (13.53%)
zilikaguliwa mara 3 hadi 4 kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010. Hali kadhalika
shule 6 (51.88%) zilikaguliwa mara moja au mbili, na shule 46 (34.59%)
hazikukaguliwa kabisa. Aidha, taarifa za ukaguzi wa shule hazifanyiwi kazi
ipasavyo. Kutokaguliwa kwa shule hizo za sekondari kumepunguza ufanisi wa
usimamizi na utoaji wa elimu bora.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
ix
d) Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu
Ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa huchangiwa na sababu mbalimbali.
Uwepo wa walimu wenye sifa stahiki shuleni ni moja ya sababu muhimu.
Utafiti umebaini kuwa, sifa za udahili kwa walimu tarajali wa stashahada ni za
ufaulu wa kiwango cha chini (1Principal na 1Subsdiary) katika masomo ya
kufundishia na baadhi yao hawana wito wa kazi ya ualimu. Aidha utafiti umebaini
kuwa kuna changamoto katika matayarisho ya walimu tarajali unaosababishwa
na upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Aidha, matokeo ya utafiti yameonesha kuna upungufu mkubwa wa walimu
kimasomo hususani katika masomo ya sayansi na Mathematics unaosababishwa
pia na upangaji usiozingatia mahitaji hususan katika sehemu zenye mazingira
magumu. Katika shule zilizofanyiwa utafiti imebainika kuwa somo la
Mathematics, lina mahitaji ya walimu 436 ambapo waliopo ni walimu 172 hivyo
kuna upungufu wa walimu 264 sawa na asilimia 60.6. Tatizo la upungufu wa
walimu ni changamoto katika utoaji wa elimu.
e) Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa
Matokeo mbalimbali yahusuyo mfumo wa mitihani yamebainishwa ikiwa ni
pamoja na muundo wa maswali yatolewayo shuleni kutokidhi viwango
vinavyotumika na NECTA.
Aidha, Miundo ya mitihani ya Taifa haiwafikii baadhi ya walimu na wanafunzi na
hivyo kutoielewa. Hii inaonesha jinsi ambavyo baadhi ya walimu na wanafunzi
hawapati fursa ya kuiona na kuitumia miundo ya mitihani na miongozo katika
shule za sekondari. Uwepo wa Nyaraka na miongozo mbalimbali ya mitihani
katika shule ni muhimu katika kumwandaa mtahiniwa hivyo, wadau wote
wanapaswa kupata na kutumia machapisho hayo.
Utafiti umebaini kuwa, uteuzi wa wasahihishaji katika ngazi ya shule haufanywi
kwa makini. Aidha, utaratibu wa kulipa wasahihishaji kwa idadi ya ‘scripts’
walizosahihisha badala ya posho ya kujikimu na muda mrefu wa usahihishaji
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
x
kwa siku ni baadhi ya masuala yanaweza kuchangia kupungua kwa umakini wa
usahihishaji.
Aidha utafiti umebaini kuwa, mwongozo kuhusu mchango wa CA wa 50% (45%
majaribio na mazoezi na 5% projekti) katika mtihani wa Taifa hautumiki au
mchakato wake katika matokeo ya mwisho haufahamiki kwa wadau wa elimu.
Hata hivyo NECTA wanatumia vigezo vingine vya ulinganifu sanifu ambavyo
mchakato wake wa kuvitumia haueleweki kwa wadau. Aidha utafiti umebaini
kuwa, gredi zinazotumika shuleni kwa uzoefu wa miaka mingi ni A (81-100), B
(61-80), C (41-60), D (21-40), F (0-20). Hata hivyo NECTA imethibitisha kuwa
alama za gredi zinazotumika kwa Mtihani wa Taifa wa K4 huamuliwa na Kamati
ya Kutunuku ambapo gredi D huwa si chini ya alama 30 na A si chini ya alama
70. Hali hii ya kutokuwepo kwa alama za gredi zenye ulinganifu baina ya shule
na NECTA kumeleta mkanganyiko wa matumizi ya alama za gredi. Vilevile, kuna
mapungufu ya kuadhibu watahiniwa kwa kuteremshwa daraja la I au la II kuwa
la III kutokana na kufeli baadhi ya masomo ya msingi na ya mchepuo.
f) Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
Utafiti umebaini kuwa katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti, kuna upungufu mkubwa
wa miundombinu, samani na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni ikijumuisha
maabara ya Chemistry (79.6%), Biology (66%) na Physics (65.2%) nyumba za
walimu (72%), na maktaba (80.6%). Aidha, baadhi ya shule zimepata usajili bila
kutimiza vigezo na nyingine kujengwa mbali na makazi ya jamii husika. Vilevile
utafiti umebaini upungufu wa vifaa vya kufundishia ikiwa ni pamoja na vitabu vya
kiada na ziada vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa kwa baadhi ya masomo
kwa wastani wa 75.5% katika shule zilizofanyiwa utafiti.
Matokeo ya utafiti pia yamebaini kutokuwepo kwa chakula cha mchana kwa
wanafunzi katika shule za kutwa, na hivyo kuathiri mahudhurio na umakini wa
wanafunzi katika ujifunzaji.
Hali hii ya upungufu wa miundombinu, upatikanaji wa vitabu vinavyoendana na
mihtasari iliyoboreshwa na kutokuwepo kwa chakula cha mchana ni changamoto
ambazo zinaathiri utekelezaji wa mitaala shuleni.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
xi
Mapendekezo
Kutokana na taarifa za utafiti kuna mapungufu na changamoto mbalimbali zilizoathiri
kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 mwaka 2010. Mapendekezo
muhimu yametolewa ambayo yanaweza kutekelezwa kwa muda mfupi, kati na mrefu.
1. Uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kielimu uzingatie uzoefu, utaalamu, uwezo,
uadilifu na uwajibikaji. Aidha, nafasi za uongozi zilizoachwa wazi zijazwe na
zisikaimishwe kwa muda mrefu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu;
2. Maamuzi yanayohusu masuala ya elimu yafanywe kwa kuzingatia utaalam,
tathmini na tafiti za kisayansi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya
utoaji wa elimu;
3. Bajeti ya elimu iongezwe na izingatie vipaumbele katika sekta ya elimu ili kutatua
changamoto zilizopo;
4. Chombo cha Kusimamia Taaluma ya Ualimu (Teachers Professional Board)
kianzishwe kwa lengo la kushughulikia viwango vya taaluma, maadili, utendaji
na haki za walimu ili kulinda hadhi ya kazi ya ualimu na kuhakikisha kuwa
inakidhi malengo yaliyokusudiwa; Utaratibu wa motisha kwa walimu
unaoendana na uzito wa kazi, wadhifa na ugumu wa mazingira anapofanyia kazi
uandaliwe na utekelezwe ipasavyo;
5. Wanafunzi wanaofeli katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 wahimizwe kufanya
mitihani ya marudio kama watahiniwa binafsi ili wapate sifa za kujiendeleza
kitaaluma na kitaalamu;
6. Vyuo vya ufundi stadi kama vile VETA vipanuliwe ili kuwawezesha wahitimu wa
kidato cha 4 wanaopenda kujiunga na vyuo hivyo kujiunga na kupata ujuzi na
stadi za kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri;
7. Walimu wenye sifa wasambazwe kwa usawa kwa kuzingatia mahitaji katika shule
zote. Pia, Programu za mafunzo zisizoathiri ikama ya walimu katika kila shule
ziandaliwe;
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
xii
8. Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji yaimarishwe.
9. Usajili wa vyuo na shule za Serikali na zisizo za Serikali uzingatie vigezo
vinavyotakiwa;
10.Walimu wawapime wanafunzi kwa kuwapa mazoezi endelezi (CA) yenye uhalisia
pia alama za CA zitumike katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kama
ilivyoelekezwa katika mwongozo wa mazoezi endelezi;
11.Utungaji na uhakiki wa mitihani ya taifa uboreshwe na uzingatie mitaala
inayotekelezwa
12.Adhabu katika upangaji wa madaraja inayomshusha mtahiniwa hadi daraja la III
baada ya kufeli mojawapo ya masomo ya msingi au mchepuo iondolewe ili kila
mtahiniwa apate daraja linalolingana na kiwango cha ufaulu wake;
13.Hadhi ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 irudishwe ili utumike kuchuja
wanafunzi. Aidha, wanafunzi wasiokuwa na uwezo wapatiwe masomo ya ziada
(Remedial)
14.Mfumo rasmi wa kupata gredi katika mitihani ya shule na Taifa unaofahamika
kwa wadau wote wa elimu utayarishwe na kutumika kikamilifu ili kuleta haki
kwa watahiniwa;
15.Wasahihishaji wa mitihani ya taifa walipwe posho ya kujikimu kwa sababu ni
haki ya mwajiriwa wa serikali;
16.Mafunzo kabilishi kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na
kutekelezwa kwa walimu na wakaguzi wote. Aidha Mafunzo maalumu kuhusu
dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na kutekelezwa kwa maafisa
mitaala na maafisa mitihani ili kuwajengea uwezo;
17.Mihtasari ya kutosha isambazwe shuleni na isiuzwe. Aidha nakala laini (soft
copy) ya mihtasari iwekwe kwenye mtandao (website) ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na TET ili wadau waweze kuipata kiurahisi;
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
xiii
18.Jukumu la kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mtaala litekeleze kikamilifu ili
kubaini dosari za kiutekelezaji na hivyo kufanya marekebisho stahiki;
19.Taratibu za utayarishaji wa mitaala zizingatiwe ikiwa ni pamoja na kufanya
utafiti, tathmini na kujaribisha mitaala kabla ya utekelezaji wake.
20.Fedha za kutosha kwa ajili ya kununua samani na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia shuleni zitengwe na kutumika ipasavyo. Vilevile, Hosteli/mabweni na
nyumba za walimu zijengwe kwenye shule za sekondari zilizo mbali na makazi
ya watu, na wanafunzi katika shule zote za kutwa wapatiwe chakula cha
mchana;
21.Sifa za udahili wa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada
zipandishwe kuwa Principal mbili za masomo atakayofundisha, ili kumwezesha
mwalimu kuwa mahiri kitaaluma;
22.Vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha vipatikane na upanuzi wa
miundombinu ufanyike katika vyuo vya ualimu na vyuo vikuu ili kuendana na
ongezo la udahili na kufikia viwango vilivyowekwa. Wakufunzi na wahadhiri
wapewe mafunzo kazini juu ya mtaala unaozingatia ujuzi (Competence Based
Curriculum);
23.Maabara ya lugha ya kiingereza (language laboratory) zianzishwe na
kuimarishwa katika Vyuo vya ualimu na Vyuo vikuu ambapo walimu tarajali
watatumia kujifunzia lugha ya kiingereza ili kuongeza stadi za kuongea na
kuandika. Pia Programu maalumu ya mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa
walimu wa masomo yote ianzishwe na itekelezwe katika shule zote za
sekondari;
24.Utaratibu maalumu uanzishwe kwa kuwapatia mafunzo ya Ualimu (Post
Graduate Diploma in Education) wahitimu wa shahada zisizo za ualimu ili
kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mfupi;
25.Ukaguzi wa shule, utafiti wa elimu, ufuatiliaji na tathmini uimarishwe kwa
kupatiwa nyenzo na wataalamu wa kutosha ili kutoa maamuzi yenye uhalisia;
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
xiv
26.Ufuatialiaji wa usambazaji, upatikaji na utumiaji wa vitabu vya kiada na ziada
pamoja na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia uimarishwe;
27.Sheria ya vitabu itungwe ili kudhibiti usambazaji na matumizi ya vitabu visivyo
na ithibati katika shule nchini.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
15
SURA YA KWANZA: UTANGULIZI
1.1. Usuli
Utoaji wa elimu nchini Tanzania unaongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka
1995. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo unaenda sambamba na Dira ya Taifa
2025, MKUKUTA, kutimiza malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo ya
Maendeleo ya Milenia (MDGs). Aidha, utekelezaji wa será hiyo unaenda sambamba na
utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama ya Mapinduzi ya mwaka 2010.
Katika kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya
Elimu ilianzishwa 1997 na kuhuhishwa 2001 na 2008. Aidha, Programu za Mipango ya
Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Sekondari (MMES) zilianzishwa kutekeleza
program ya sekta. Mafanikio ya MMEM (2002-2006) na MMEM II (2007-2011)
yameongeza mahitaji ya upanuzi wa Elimu ya Sekondari, ambapo Mpango wa
Maendeleo ya Elimu ya Sekondari – MMES I (2004-2009) ulitekelezwa kwa lengo kuu
la kuongeza uandikishaji wa wanafunzi katika shule za sekondari na MMES II (2010-
2014) imeweka kipaumbele katika kuinua ubora wa Elimu ya Sekondari. Mafanikio
hayo yalihitaji dhamira kubwa ya uwekezaji katika elimu ambapo Serikali imetoa
mgawo mkubwa wa fedha za umma. Aidha, wazazi, jamii, na wahisani wana mchango
mkubwa katika utoaji wa elimu nchini na kuifanya Tanzania iwe mbele ya muda wa
kuyatekeleza na kuyafikia malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yanayohusu
upatikanaji wa elimu kwa usawa wa kijinsia.
Mantiki ya elimu ni kumsaidia kila mtoto kukuza maarifa, stadi na mielekeo ili aweze
kuishi maisha yenye ustawi duniani kwa kumsaidia kuanza kujua kusoma na kufanya
hesabu na stadi ambazo zinaweka msingi wa uwezo wa kudadisi, kufikiri, kusikiliza,
kuuliza maswali, kuchambua, kupambanua na kuwasiliana kwa kujiamini (UWEZO,
2010). Stadi hizi na maendeleo ya mwanafunzi yanapimwa wakati wa mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji wa somo husika ambapo mazoezi na mitihani anuai hutolewa
na walimu. Wakati mwingine, upimaji hufanyika baada ya mchakato wa ufundishaji na
ujifunzaji nje ya darasa.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
16
Mitihani ni nyenzo mojawapo inayotumika katika upimaji ambayo hufanyika kwa
nyakati mbalimbali kama vile robo, nusu au mwisho wa muhula na wakati wa kuhitimu
ngazi ya elimu husika. Mitihani ya ndani katika ngazi ya Elimu ya Msingi, Sekondari na
Vyuo vya ualimu hutolewa na taasisi husika. Aidha ipo mitihani ya kitaifa ambayo ni
Mitihani ya Darasa la IV na VII (Msingi), Mitihani ya Kidato cha 2, 4 na 6 (Sekondari)
na Mitihani ya Cheti na Stashahada (Vyuo vya Ualimu). Mitihani ya Darasa la IV
huendeshwa na Idara ya Elimu ya Msingi ya WEMU na ya kidato cha 2 huendeshwa
na Idara ya Ukaguzi wa Shule. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) inahusika na
uendeshaji wa Mitihani ya Darasa la VII (Msingi), Kidato cha 4 na 6 (Sekondari) na
Mitihani ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada.
Mtihani wa Taifa wa Darasa la IV ni sehemu ya tathmini ya maendeleo ya mwanafunzi
katika kupima ufahamu na kumudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Mtihani huu hutumiwa kutathmini maendeleo ya mwanafunzi kwa kipindi cha miaka
minne ya kwanza ya Elimu ya Msingi. Aidha, Mtihani wa Darasa la VII hutumika
kuthibitisha kuhitimu kwa mwanafunzi katika ngazi ya Elimu ya Msingi na hutumiwa
kufanya maamuzi ya uchaguzi wa mwanafunzi kuendelea na Elimu ya Sekondari na
mafunzo ya fani mbalimbali.
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 ni sehemu ya tathmini ya maendeleo ya
mwanafunzi. Mtihani huu hutumiwa kutathimini maendeleo ya mwanafunzi kwa
kipindi cha miaka miwili ya mwanzo ya elimu ya sekondari. Aidha, mtihani huu ni
sehemu ya mazoezi endelezi (Continuous Assessment-CA), hivyo huchangia katika
matokeo ya mwanafunzi katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 (Waraka wa Elimu
Na. 5, 1999).
Mitihani ya Taifa ya Kidato cha 4 na 6 inathibitisha kuhitimu kwa mwanafunzi katika
ngazi za elimu ya sekondari ya kawaida (Ordinary Level) na juu (Advanced Level).
Matokeo ya mitihani hii hutumiwa kufanya maamuzi ya uchaguzi wa wanafunzi
kuendelea na mfumo rasmi wa elimu kwa ngazi inayofuata, mafunzo ya fani
mbalimbali na ajira. Mitihani hii inalenga katika kupima ubora wa elimu itolewayo na
matokeo yake ni kiashiria cha ubora huo.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
17
Mwaka 2005 na 2007 mtaala wa elimu ya sekondari uliboreshwa kutoka mtaala
unaozingatia maudhui (Content Based Curriculum) na kuwa mtaala unaozingatia ujuzi
(Competence Based Curriculum). Tofauti na mtaala unaozingatia maudhui, mtaala
unaozingatia ujuzi upimaji wake ni wenye kumjali mwanafunzi kwa kuzingatia usawia
katika maeneo makuu matatu ambayo ni maarifa (knowledge), mwelekeo (attitudes)
na stadi (skills). Aidha, upimaji huu pia huzingatia uelewa wa wanafunzi katika dhana
(nadharia), vitendo na mtazamo.
Zana zinazotumika wakati wa upimaji ni pamoja na mazoezi ya darasani, majaribio,
mitihani, vitendo (practicals) na projekti. Mwongozo wa NECTA wa Mazoezi Endelezi
(NECTA: 1990) unafafanua kuwa ufaulu wa mwanafunzi utapimwa kwa kutumia
alama za mazoezi endelezi na alama za Projekti ambazo zitajumuishwa kuchangia
asilimia 50 kwenye alama ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4.
Kiwango cha ufaulu kwa Mitihani ya Taifa ya Darasa la VII, Kidato cha 2 na 4
kinaonesha kuendelea kushuka katika ngazi za Elimu ya Msingi na Sekondari tangu
mwaka 2007 toka asilimia 70.48 mwaka 2006 hadi 53.55 mwaka 2010 kwa ngazi ya
elimu ya msingi, asilimia 91.9 mwaka 2007 hadi asilimia 61.8 mwaka 2010 kwa
Mtihani wa Kidato cha 2 na asilimia 90.3 mwaka 2007 hadi asilimia 50.4 mwaka 2010
Mtihani wa Kidato cha 4 kama inavyooneshwa katika Jedwali Na.1.1.
Jedwali Na. 1.1 Kiwango cha Ufaulu Mitihani wa Darasa la VII, Kidato cha 2
na Kidato cha 4 (%) Mwaka 2006 – 2010
Mtihani 2006 2007 2008 2009 2010
Darasa la VII 70.48 54.18 52.73 49.41 53.55
Kidato cha 2 76.2 91.9 73.5 65.3 61.8
Kidato cha 4 89.12 90.3 83.6 72.5 50.4
Chanzo: The National Examinations Council of Tanzania, Examinations Results
Statistics 2007-2010, WEMU, 2010.
Pamoja na kushuka kwa ufaulu wa jumla katika Mtihani wa Taifa ya Kidato cha 4, vile
vile ufaulu umeshuka katika baadhi ya masomo kama vile Mathematics na English
Language kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 1.2.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
18
Jedwali Na. 1.2: Kiwango cha Ufaulu (%) Kidato cha 4 kwa Masomo ya
Mathematics na English Language 2006 – 2010
Somo 2006 2007 2008 2009 2010
Mathematics 23.67 31.32 24.33 17.78 16.09
English 80.98 75.54 63.23 60.03 30.33
Chanzo: The National Examinations Council of Tanzania, Examinations Results
Statistics 2007-2010
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 yameonesha kuwa
kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa asilimia 39.9 toka mwaka 2007. Matokeo hayo
pia yanaonesha idadi ya watahiniwa ambao hawakufaulu ni asilimia 49.60.
1.2. Hoja ya Kufanya Utafiti
Kitaalamu, mitihani ni nyenzo itumikayo kupima kiwango cha ujuzi ambacho
mwanafunzi amekipata. Mtihani unalenga katika kupima uelewa wa wanafunzi kwa
elimu itolewayo na matokeo yake ni kiashiria cha ubora huo. Kiwango cha ufaulu wa
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka mfululizo kwa miaka minne
tangu 2007 (Jedwali Na.1.1). Hali hii imejitokeza pia kwa matokeo ya mitihani ya
Darasa la IV, Kumaliza Elimu ya Msingi (Darasa la VII) na ile ya Elimu ya Sekondari ya
Kidato cha 2. Athari ya matokeo mabaya katika mitihani ya kuhitimu ni kuwa na jamii
ambayo haina elimu ya kiwango kilichokusudiwa kitaifa.
Kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 kumekuwa
tofauti na matarajio ya Serikali na wadau wengine wa elimu na hivyo kuibua hoja
mbalimbali juu ya sababu zilizochangia hali hiyo. Jamii ya Watanzania kwa ujumla
ingependa kujua hali halisi kuhusu kushuka kwa ufaulu. Hivyo, Serikali kwa kupitia
WEMU na OWM-TAMISEMI ikaona ni muhimu kufanya utafiti wa kisayansi ili kubaini
kiini cha tatizo.
Utafiti huu umefanyika kwa matarajio ya kuibua mambo yaliyosababisha kushuka kwa
ufaulu ikiwa ni pamoja na kubaini uzito na upeo wa matatizo yaliyojitokeza. Matokeo
ya utafiti huu yatatumiwa na Serikali na wadau wa elimu katika kufanya maamuzi na
kuchukua hatua stahiki za kuinua kiwango cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
19
Kidato cha 4. Utafiti huu unatoa mwelekeo sahihi kwa Serikali ili kupata ufumbuzi wa
changamoto zinazoikabili Sekta ya Elimu.
1.3. Malengo ya Utafiti
1.3.1.Lengo Kuu
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu ili
kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na tatizo la kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa
Kidato cha 4 na hatimaye kuinua ubora wa Elimu ya Sekondari nchini.
1.3.2. Malengo Mahsusi
Malengo mahsusi ya utafiti huu yalikuwa:
(i). Kufanya uchambuzi wa kiwango cha ufaulu wa watahiniwa wa Mtihani wa Taifa
wa Kidato cha 4 mwaka 2010;
(ii). Kubaini utoshelevu wa walimu katika shule za sekondari;
(iii). Kuchunguza hali ya mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji;
(iv). Kukusanya maoni ya wadau wa elimu kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu wa
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4;
(v). Kuchunguza ufanisi wa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu;
(vi). Kuchambua mfumo wa uendeshaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4;
(vii). Kubaini michango ya wadau wa elimu katika usimamizi na uendeshaji wa Elimu
ya Sekondari; na
(viii). Kuchambua mfumo wa utayarishaji wa walimu wa sekondari.
1.4. Maswali ya Utafiti
a) Nini sababu za kushuka kwa ufaulu wa watahiniwa wa Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4 mwaka 2010?
b) Je shule zina walimu wenye sifa na wa kutosha katika kutekeleza mtaala?
c) Hali halisi ya mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ikoje?
d) Nini maoni ya wadau wa elimu kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu wa Mtihani
wa Taifa wa Kidato cha 4?
e) Nini kifanyike kwa wahitimu waliofeli Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka
2011?
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
20
f) Mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu ni wa namna gani?
g) Mfumo wa uendeshaji (utungaji, usambazaji, usimamizi, usahihishaji na
upangaji wa madaraja) Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 ukoje?
h) Alama za mazoezi endelezi (CA) zina mchango gani katika Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4?
i) Wadau wa elimu wana mchango gani katika usimamizi na uendeshaji wa Elimu
ya Sekondari?
j) Walimu katika Shule za Sekondari wanaandaliwaje?
1.5. Muundo wa Ripoti
Ripoti ya utafiti kuhusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4 mwaka 2010, ina sura tano ambazo zimepangiliwa katika mtiririko
unaoanza na tatizo la utafiti mpaka hitimisho. Kila sura imebeba dhima moja ili
kujenga mtiririko wenye mantiki katika kujibu hoja na maswali ya utafiti.
Sura ya kwanza ya ripoti, imebeba utangulizi wa tatizo la utafiti ambapo usuli wa
tatizo, hoja ya kufanya utafiti, malengo na maswali ya utafiti yameainishwa. Sura ya
pili imeeleza mapitio ya maandiko kuhusu Sera na Mipango ya Elimu, usimamizi na
uendeshaji, ufuatiliaji na tathmini ya elimu, mitaala na utekelezaji, mitihani,
upatikanaji na usambazaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, mazingira ya
kufundishia na kujifunzia na uandaaji na upatikanaji wa walimu.
Mwongozo wa utafiti (Methodolojia) umetolewa katika sura ya tatu na unajumuisha
eneo la utafiti, walengwa wa utafiti, uchaguzi wa sampuli, zana za utafiti, utaratibu wa
kufanya utafiti na uchambuzi wa takwimu. Matokeo ya utafiti na uchambuzi wa
takwimu kulingana na malengo na maswali ya utafiti yamejadiliwa katika sura ya nne.
Taarifa ya utafiti imehitimishwa katika sura ya tano ambapo hitimisho na
mapendekezo muhimu kutokana na matokeo ya utafiti yameainishwa.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
21
SURA YA PILI: MAPITIO YA MAANDIKO
2.1 Sera na Mipango ya Elimu
Kama ilivyo kwa mataifa yote, Tanzania ina mfumo wake wa elimu tangu ilipopata
uhuru mwaka 1961. Mfumo huo umepitia katika mabadiliko anuai ikiwa ni pamoja na
utoaji wa elimu, mitaala na tathmini na upimaji. Serikali ilifuta Sheria ya Elimu ya
mwaka 1927 na kupitisha Sheria ya Elimu ya mwaka 1962 ili kurekebisha utoaji wa
elimu kwa kuleta usawa na kutoa ubaguzi wa rangi na dini uliokuwepo wakati wa
ukoloni (Sera ya Elimu na Mafunzo, 1995).
Mwaka 1967, falsafa ya Elimu ya Kujitegemea (Education for Self Reliance) ilianzishwa
ambapo msisitizo mkubwa uliwekwa kwenye ujenzi wa maarifa, ujuzi na mwelekeo
unaotakiwa katika kujenga jamii inayojitegemea (Nyerere, 1967). Pamoja na mambo
mengine falsafa hiyo ilisisitiza utoaji wa elimu utakaowasaidia wahitimu kushiriki
ipasavyo katika kujenga na kuiletea maendeleo jamii ya Watanzania juu ya masuala
yahusuyo ujenzi wa ari, udadisi na kufanya uchunguzi wa kisayansi, ubunifu, uwezo
wa kutatua matatizo ya kijamii na uwezo wa kujiamini na ushirikiano. Mitaala ya
Tanzania huandaliwa kwa kuzingatia dhana ya falsafa ya elimu ya kujitegemea.
Kati ya mwaka 1967 na 1978, Serikali ilichukua hatua kadhaa na ilitunga sheria
mbalimbali ili kuhalalisha hatua zilizochukuliwa wakati wa azimio la Arusha na Elimu
ya Kujitegemea. Sheria na hatua hizi zilijumuishwa na sheria za elimu za 1969 na
1978; Mpango wa Madaraka Mikoani wa 1972; Sheria ya Baraza la Mitihani la Taifa
Na. 21 ya 1973; Elimu ya Msingi kwa Wote (UPE) na Azimio la Musoma la mwaka
1974; Sheria ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Na. 12 ya 1975 na Sheria ya Taasisi
ya Elimu Tanzania Na. 13 ya 1975.
Mwaka 1981, Tume ya Rais ya Elimu iliundwa ili kuchunguza mfumo wa elimu
uliokuwepo na kutoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya lazima yaliyohitajiwa
kufanyika nchini ifikapo mwaka 2000. Mapendekezo mengi yaliyowasilishwa na Tume
mwaka 1982 yalitekelezwa na Serikali ikiwemo upanuzi wa elimu ya sekondari.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
22
Mwaka 1990, Serikali iliunda Tume Maalumu ya Elimu kuangalia upya mfumo wa
elimu kwa ajili ya Karne ya 21. Mwaka 1992 Tume hii iliwasilisha taarifa serikalini
ambapo mapendekezo yake yalizingatiwa katika kuunda Sera ya Elimu na Mafunzo,
1995.
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ambayo ipo katika mchakato wa kuhuishwa
ndiyo inayotumika katika utoaji wa elimu nchini. Sera hiyo inatekelezwa na Wizara
zote lakini zilizo muhimu kwa elimu rasmi na elimu ya nje ya mfumo rasmi ni Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU), Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo pia unaenda sambamba na Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2025, MKUKUTA, Malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo
ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ambapo Serikali imeridhia Mikataba hiyo (SEDP II,
2010).
Elimu ya Sekondari ni kiungo muhimu kati ya Elimu ya Msingi na Elimu ya Juu. Moja
ya malengo ya elimu ya sekondari ni kumwandaa mwanafunzi kwa ajili ya elimu ya
kati, ya juu, ya ufundi na ufundi stadi na kujiunga na ulimwengu wa kazi (Sera ya
Elimu na Mafunzo, 1995).
2.2 Mipango na Mikakati ya Elimu
Serikali ilianzisha Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu mwaka 1997 na
kuifanyia marekebisho mwaka 2001 na 2008 ili kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo
nchini. Ili kufanikisha utekelezaji wa programu hiyo, ilianzishwa mipango na mikakati
mbalimbali kama vile Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM, 2002-2006)
na awamu ya pili ya MMEM (2007-2011). MMEM ilianzishwa ili kuboresha elimu ya
msingi na kutoa fursa sawa ya elimu kwa watoto wote.
Mafanikio ya MMEM yamesababisha upanuzi wa elimu ya sekondari, ambapo Mpango
wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari - MMES awamu ya kwanza, 2004-2009 na
awamu ya pili (2010-2014) unatekelezwa ili kuongeza uandikishaji wa wanafunzi
katika shule za sekondari kwa kuzingatia fursa na usawa. Aidha, MMES II imetoa
kipaumbele katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari, ambapo mpango huu
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
23
umeharakisha utekelezaji wa ibara ya 5.4.2 ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka
1995 inayosisitiza kujenga na angalau shule moja ya sekondari kwa kila Kata nchini.
Idadi ya shule za sekondari (za serikali na zisizo za serikali) imefikia 4,266 mwaka
2010 ukilinganisha na shule 1,745 zilizokuwepo mwaka 2005, ongezeko hili ni sawa
na asilimia 144.5. Mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi
(Kidato cha 1-4) walioandikishwa katika shule za sekondari za kawaida kutoka
wanafunzi 489,942 mwaka 2005 hadi kufikia 1,566,685 mwaka 2010. Vilevile,
kumeimarika kwa vigezo vya kupimia maendeleo ya Elimu kama Gross Enrolment
Ratio (GER) na Net Enrolment Ratio (NER) kutoka asilimia 15.9 na 10.3 mwaka 2005
kufikia asilimia 47.3 na 30.8 mwaka 2010. Mafanikio haya makubwa yamepatikana
kutokana na ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, Serikali, Wafadhili pamoja na
wadau wengine mbalimbali wa elimu.
Katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari, MMES awamu ya kwanza ilikuwa na lengo
la kuboresha mtaala ili uendane na mahitaji ya soko la ajira. Maboresho ya mtaala
yalifanyika katika ngazi ya Elimu ya Msingi, sekondari na mafunzo ya ualimu mwaka
2005 na 2007. MMES pia ilikuwa na lengo la kuongeza ubora wa elimu ya sekondari
kwa kutatua tatizo la upungufu wa walimu na kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya
ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia (Updated SEDP, 2007 ).
2.3 Uongozi katika Elimu
Mfumo wowote wa elimu unategemea uongozi na utawala bora ili kufikia malengo
yaliyowekwa. Mbinu nzuri za uongozi ni muhimu kwa ufanisi wa mfumo wa elimu na
mafunzo na asasi zake. Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inabainisha kuwa uongozi
wa Elimu na mafunzo unafanywa na Wizara kadhaa, mashirika ya Umma na mashirika
yasiyo ya kiserikali.
Sheria mbalimbali zilizowezesha wizara na taasisi kubeba wajibu wa elimu na mafunzo
zina uhusiano mdogo na sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978. (Ripoti ya Tume ya
Rais ya Elimu, 1982) Sheria hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 1995 ili kujumuisha
maeneo mengine ya elimu na mafunzo, pamoja na uongozi, utawala na fedha.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
24
Ibara ya 4.3 katika Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inaeleza kuwa madaraka na
utoaji uamuzi katika uongozi na utawala wa elimu na mafunzo vimebaki kwenye ngazi
ya wizara. Mwaka, 2009 usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari ulihamishiwa
katika serikali za Mitaa. (Waraka wa Elimu Na. 13 wa Mwaka 2009). Usimamizi huu
unaendana na Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) kwamba
‘Wizara zinazo wajibika na elimu na mafunzo zitakasimu madaraka yao ya uongozi na
utawala wa elimu na mafunzo kwa vyombo vya chini vya jamii’.
Viongozi na watawala wa elimu kwenye ngazi za taifa, Mkoa, Halmashauri na asasi
wawe na uzoefu na sifa za juu kitaaluma na kitaalamu na wawe na ujuzi katika
uongozi na utawala wa kielimu. Katika kuimarisha usimamizi na uongozi katika elimu,
utoaji wa mafunzo ya kujenga uwezo umetiliwa mkazo kwa kila ngazi ya elimu
(Updated SEDP, 2007).
2.4 Usimamizi na Uendeshaji
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inashughulika na masuala ya uandaaji wa sera,
mitaala, kuweka viwango, usimamizi wa ubora wa elimu, itolewayo na kufanya
ufuatiliaji na tathmini. Serikali iliamua kugatua majukumu ya usimamizi na uendeshaji
wa shule za sekondari kwenda katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na utekelezaji
wake ulianza rasmi tarehe 1 Julai, 2009. Lengo la mabadiliko hayo ni kuboresha
huduma ya utoaji wa elimu na kusogeza huduma hiyo karibu zaidi na wananchi.
Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) imeeleza katika ibara ya 4.3.6 kuwa
‘Bodi na Kamati za asasi za elimu na mafunzo zitawajibika katika uendeshaji, kupanga
maendeleo, nidhamu na fedha za asasi zilizochini ya mamlaka yao’.
Kiongozi cha Mkuu wa shule ya Sekondari (1997) kinaeleza kuwa ‘Bodi ya shule ni
chombo muhimu ambacho kila shule inapaswa kuwa nacho ili kufanikisha lengo la
elimu ya Sekondari nchini. Kwa mujibu wa sheria ya Elimu Na 25 ya mwaka 1978 na
rekebisho lake Na.10 la mwaka 1995. Bodi ya Shule imepewa mamlaka ya kusimamia
uongozi na uendeshaji wa mipango yote ya maendeleo ya shule; kusimamia nidhamu
ya walimu, wanafunzi na masuala ya fedha za shule.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
25
Kiongozi cha Mkuu wa shule ya Sekondari (1997) kinaelekeza kuwa uongozi na
utawala unaopaswa kuwepo katika kila shule ya sekondari ni Mkuu wa shule, Makamu
Mkuu wa Shule na Mwalimu Mwandamizi Taaluma. Chini ya Mwalimu mwandamizi
Taaluma watakuwepo viongozi wafuatao: Mwalimu Mshauri Mafunzo na Kazi, Wakuu
wa idara za Masomo, Walimu wa Masomo Walimu wa Madarasa na Mwalimu
Mwandamizi Malezi na Utamaduni. Aidha, chini ya Mwalimu Mwandamizi Malezi na
Utamaduni watakuwepo viongozi wafuatao: Mwalimu Mlezi wa nyumba/Hosteli,
Mratibu wa Michezo. Pia shule zitakuwa na Mwalimu Mwandamizi Uzalishaji Mali na
Mwalimu wa Zamu
2.5 Ugharamiaji wa Elimu
Ugharamiaji wa Elimu na Mafunzo nchini kwa ujumla ni jukumu la Serikali. Aidha,
jamii, wazazi/walezi, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine wa elimu
huhusishwa katika kugharamia elimu. Serikali pia inapata fedha za nje kwa Washirika
wa Maendeleo kwa ajili ya kugharamia elimu kupitia njia tatu zifuatazo; misaada ya
bajeti (General Budget Support- GBS), Mifuko ya pamoja (Basket funds) na Misaada
ya miradi ya Maendeleo (Direct Project Funds) (Andiko la MMES, 2004). Kwa ajili ya
kupima ufanisi na athari kutokana na rasilimali na matumizi ya fedha za umma,
serikali inatumia mfumo wa matumizi wa muda wa kati (Medium – Term Expenditure
Framework -MTEF).
Ugharamiaji wa elimu umeendelea kuwa mojawapo ya vipaumbele vya serikali.
Asilimia ya Bajeti ya sekta ya elimu kutoka kwenye bajeti kuu ya Taifa imeendelea
kupanda na kushuka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, 2000/01 hadi 2010/11 kama
ilivyobainishwa katika Jedwali Na. 2.1
Jedwali Na 2.1 Mgawo wa Bajeti ya Sekta ya Elimu 2000/01 -2010/11
Mwaka wa Fedha
2000/2001
2001/2002
2002/2003
2003/2004
2004/2005
2005/2006
2006/2007
2007/2008
2008/2009
2009/2010
2010/2011
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
26
% Sekta ya Elimu
katika Bajeti kuu ya
Taifa
16.7 22.1 18.8 18.7 15.1 18.8 18.3 18.3 19.8 18.3 18.9
% Sekta ya Elimu
katika GDP 2.7 3.6 3.8 4.0 3.6 4.2 5.3 5.3 5.8 6.2 -
Chanzo; URT, 2010 (Basic Education Statistics in Tanzania)-Takwimu za Elimu
Katika kipindi hicho kiwango cha juu cha mgawo wa bajeti ya sekta ya elimu kilifikia
22.1% mwaka wa fedha 2001/02 na kimeendelea kushuka na kufikia 17.6% mwaka
wa fedha 2010/11. Aidha, kiwango kinachotengwa kwenye sekta ya elimu kutoka
kwenye Pato la Taifa (GDP) kimeendelea kuongeza kutoka 2.7% mwaka 2000/2001
na kufikia 6.2%, mwaka 2009/2010 ( (BEST 2010, PETS 2010).
Hata hivyo, mwenendo wa mgawo wa fedha katika sekta ya elimu tangu mwaka wa
fedha 2000/01 hadi 2010/11 unaonesha kuwa asilimia kubwa inaelekezwa kwenye
Elimu ya Msingi, Elimu ya Mfumo usio rasmi na Taasisi nyingine za Elimu na Huduma
Saidizi (62.2%) na kufuatiwa na Ufundi na Elimu ya Juu (26.5%) na kwa upande wa
elimu ya sekondari ni (9.8%) kwa mwaka 2010/11 (BEST 2010).
2.5.1 Upelekaji na Matumizi ya Fedha Shuleni
Shule zote za serikali za msingi na sekondari zinapaswa kupelekewa fedha kupitia
mfumo wa ugawaji fedha za serikali (Government Grants System). Fedha
zinazopokelewa shuleni zimegawanyika katika mafungu mawili; fedha za ruzuku
(Capitation Grants) na fedha za maendeleo (Development Grants). Halmashauri
zinapeleka fedha shuleni kupitia kwenye akaunti za shule yaani Akaunti ya Maendeleo
na Akaunti ya matumizi ya kawaida (School Development and Recurrent Accounts)
ambapo kila shule inapaswa kufungua akaunti hizo kama ilivyoelekezwa katika
Waraka wa Elimu Na 13 wa mwaka, 2009.
Akaunti ya maendeleo inahifadhi fedha zote za maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa
madarasa na maabara; ujenzi wa nyumba za walimu; na vifaa vya kudumu. Akaunti
hii pia inapokea fedha kutoka kwa wahisani mbalimbali. Akaunti ya matumizi ya
kawaida ni kwa ajili kukusanyia fedha zote zinazohusika na matumizi ya kawaida
(Other Chargies) ya kila siku ya shule pamoja na makusanyo ya ada za wanafunzi.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
27
Katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES I & II) serikali
inapeleka fedha katika shule za sekondari kutoka Hazina kwa kupitia katika
Halmashauri husika. Miongozo ya fedha za MMES II, 2010 inaelekeza kuwa,
Halmashauri zinapaswa kupeleka fedha za ruzuku katika kila shule ya sekondari kwa
kiwango cha sh. 25,000/= kwa kila mwanafunzi kwa mwaka. Taarifa ya OWMTAMISEMI
(April, 2011), inafahamisha kuwa mgawo wa fedha za ruzuku zilizopelekwa
kwenye shule za sekondari za Serikali ni Sh. 10,883/= kwa kila mwanafunzi kwa
mwaka.
Mwongozo kuhusu matumizi ya fedha za ruzuku (SEDP II, 2010), unaeleza kuwa
jumla ya fedha za ruzuku zitakazopelekwa kwenye kila shule, 50% itatumika
kununulia vitabu vya kiada na 50% itatumika kununua vifaa vingine vya kufundishia
na kujifunzia. Matumizi ya fedha hizo yanaidhinishwa na Bodi za shule kutokana na
mpango kazi wa shule uliothibitishwa.
2.6 Ufuatiliaji na Tathimini ya Elimu
2.6.1 Ngazi ya Kitaifa (Wizara na Taasisi zake)
Lengo la ufuatiliaji na tathimini ni kubaini mafanikio na udhaifu na kufanya
marekebisho ili malengo ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo yaliyowekwa
yaweze kufikiwa. Ufuatiliaji na tathimini ya mara kwa mara huimarisha majadiliano
kati ya wadau na kuinua ubora wa matokeo tarajiwa na kuharakisha ukamilishaji wa
shughuli zote zilizokusudiwa katika kutekeleza programu na miradi ya elimu (SEDP II
June, 2010).
Katika mfumo wa ufuatiliaji na tathimini ya elimu, ipo Seksheni ya Ufuatiliaji na
Tathmini chini ya Idara ya Sera na Mipango ya WEMU. Seksheni ya Ufuatiliaji na
Tathmini inahusika na utoaji wa utaalamu na huduma katika utekelezaji, ufuatiliaji na
tathimini ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
28
Programme ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP 2008 - 17) inaeleza ufuatiliaji na
tathimini itafanyika ili kuhakiki utekelezaji wa shughuli kulingana uwepo wa thamani
ya fedha iliyotumika. Aidha, imeelezwa kuwa ufuatiliaji utajikita katika kuweka mkazo
kuangalia ubora wa taarifa za utekelezaji zitakazokusanywa, kuhifadhiwa na
kuchambuliwa. Katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari
(MMES) awamu ya kwanza na awamu ya pili, ufuatiliaji na tathimini ya utekelezji wa
mpango huu unapaswa kufanyika kwa kufuata muundo wa utawala wa WEMU na
OWM-TAMISEMI ili kuzuia mapungufu yoyote yanayoweza kujitokeza wakati wote wa
utekelezaji wake (SEDP II, 2010).
Taarifa za ufuatiliaji na tathmini katika ngazi ya taifa zinathibitisha kuwa ufuatiliaji
umefanyika kikamilifu katika ngazi ya elimu ya msingi, hususan katika utekelezaji wa
MMEM (Education Sector Performance Report, 2008).
2.6.2 Ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa
Majukumu ya Sekretariati za Mikoa ni kufuatilia na kutoa ushauri wa kitaalamu na
kusimamia utekelezaji wa MMES katika Halmashuri na shule zote katika mkoa husika.
Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji hushiriki katika kuanzisha shule mpya
pamoja na ufuatiliaji wa usimamizi na uendeshaji wa shule katika Mamlaka zao.
Halmashauri huandaa mipango ya shule ambapo mikoa huratibu mipango hiyo.
Jukumu la Uongozi wa elimu ngazi ya kata ni kuhamasisha jamii katika kuchangia
rasilimali za uendelezaji wa elimu katika maeneo yao. Kwa ujumla Mamlaka hizi,
pamoja na kusimamia uendeshaji wa shule katika maeneo yao, hutakiwa kufuatilia na
kuandaa taarifa za utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo na kuwasilisha taarifa
hizo kwenye OWM-TAMISEMI na WEMU.
2.6.3 Ukaguzi wa Shule
Ukaguzi wa utekelezaji wa mtaala ni jukumu la Idara ya Ukaguzi wa shule. Idara ya
ukaguzi wa shule ipo chini ya WEMU na ilianzishwa rasmi mwaka 1978 (Kiongozi cha
Mkaguzi wa shule, 2006-MoEVT). Majukumu ya Idara ya ukaguzi wa shule ni
kuhakikisha kuwa sera, sheria, kanuni na viwango vya utoaji elimu vilivyowekwa
kitaifa vinatekelezwa na vinazingatiwa ipasavyo katika shule za awali, msingi,
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
29
sekondari na vitengo vya elimu maalumu, vituo vya ufundi stadi, elimu ya watu
wazima na vyuo vya Ualimu (Hotuba ya bajeti ya WEMU 2009/2010 p.43). Imeelezwa
katika Kiongozi cha Mkaguzi wa shule (2006), kuwa Ukaguzi wa shule umegawanyika
katika aina tatu, nazo ni ukaguzi wa jumla wa shule, ukaguzi wa kufuatilia na ukaguzi
maalumu.
Ukaguzi wa jumla ni wa mambo yote yanayohusu shule kama sehemu ya kufundishia
na kujifunzia kulingana na mpango wa jumla wa maendeleo ya shule. Inategemewa
kuwa kila shule itakaguliwa walau mara moja katika kipindi cha miaka mitatu. Katika
ukaguzi wa jumla wa shule kila mkaguzi anatarajiwa kukagua shule 30 (za
sekondari/vyuo au msingi) kwa kila mwaka. Aidha ukaguzi wa kufuatilia una lengo la
kuona kiwango cha utekelezaji wa ushauri uliotolewa katika ukaguzi uliopita na
ukaguzi maalumu unalenga katika kupata taarifa mahsusi kuhusu mambo mbalimbali
ya kielimu. Baada ya ukaguzi, wakaguzi wa shule hujadiliana na walimu kuhusu
mazuri na mapungufu yaliyojitokeza. Ukaguzi wa shule unafuatiwa na uandishi wa
taarifa ambayo inatumwa kwa wadau wa shule husika (Kiongozi cha Mkaguzi wa
Shule, 2006).
Huduma za ukaguzi wa shule hazijatolewa kwa ukamilifu kutokana na upungufu wa
nyenzo za kufanyia kazi pamoja na ufinyu wa rasilimali nyinginezo (Tume ya Rais ya
Elimu, Februari, 1982). Kimsingi imedhihirika kuwa taasisi za elimu ambazo
hukaguliwa mara kwa mara zimekuwa na maendeleo mazuri kitaaluma, kiuongozi,
kinidhamu na kimazingira (Waraka wa Elimu Na. 1 wa mwaka 1998). Aidha, ongezeko
la idadi ya shule za msingi na za sekondari limeongeza mahitaji ya rasilimali watu,
fedha na nyenzo nyingine za kufanyia kazi. Kutokana na hali hiyo, katika taarifa
mbalimbali zikiwemo za Tume ya Kero ya rushwa, Sekta ya Elimu ya Mei, 1997, vikao
vya viongozi wa Wizara ya Elimu na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, ilionekana
kuwa upo umuhimu wa kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule ili iweze kufanya kazi
zake ipasavyo (Waraka wa Elimu Na. 1 wa mwaka 1998).
Kumekuwepo kiwango kidogo cha ukaguzi wa shule na kutotekelezwa maoni ya
taarifa za ukaguzi wa shule. Matokeo ya utafiti kuhusu kushuka kwa kiwango cha
ufaulu wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ya mwaka 2008 (WEMU, 2008)
yamebainisha kuwa Ofisi za Ukaguzi wa Shule zimeshindwa kukagua idadi ya shule
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
30
zilizopangwa kwa kila mwaka. Hali isiyoridhisha ya Ukaguzi wa Jumla wa Shule
(Whole school Inspection) inaoneshwa katika jedwali Na. 2.1
Jedwali Na 2.2 Idadi ya Shule/Taasisi zilizokaguliwa mwaka 2009/10
Aina ya Shule/Taasisi Idadi ya
shule/Taasisi
(2009)
Maoteo ya
idadi ya
shule za
kukaguliwa
Idadi ya
Shule/Taasisi
zilizokaguliwa
Asilimia ya
ukaguzi
Shule/Madarasa ya Awali
41,154 5,137 2,570 50.0
Shule za Msingi 15,727 6763 3,406 50.4
Vituo vya Ufundi 352 151 55 36.4
Shule/Madarasa ya Elimu
Maalumu 284 115 56 48.7
Vituo vya EWW 15,500 6,187 2,588 41.8
Shule za Sekondari 4,102 1,664 1,258 75.6
Vyuo vya Ualimu 75 77 27 35.1
Chanzo: BEST, 2010
Takwimu za WEMU zinaonesha kuwa kuna jumla ya wakaguzi wa shule za sekondari
116 waliopo katika Kanda na makao makuu, ambapo wanahitajika 252 hivyo kuna
upungufu wa wakaguzi 136 sawa na asilimia 54 (BEST, 2010). Zipo sababu
mbalimbali zinazosababisha Idara ya Ukaguzi wa Shule kushindwa kutekeleza
majukumu yake. Sababu zifuatazo zimebainika kuchangia hali hiyo: Kiasi cha fedha
zinazotengwa/zinazotolewa hazitoshelezi na kutokuwepo kwa vitendeakazi hasa
vyombo vya usafiri. Aidha, imebainika kuwa kuna ufuatiliaji mdogo wa taaluma ngazi
ya Halmashauri na kutotekeleza taarifa za ukaguzi wa shule hali iliyosababisha
kushuka kwa ufaulu katika Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi na sekondari. Sababu
za kutokufuatilia kwa ukamilifu ni pamoja na kukosekana kwa usafiri wa uhakika
(Taarifa ya Utafiti Kuhusu Kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa Mtihani wa Kuhitimu
Elimu ya Msingi, Mwaka 2008: uk. 26).
Idara ya ukaguzi wa shule inaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi, ingawa
Serikali imendeelea na jitihada za kuhakikisha kuwa wakaguzi wa shule wanatekeleza
majukumu yao kwa ufanisi. Katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali imeanzisha
utaratibu wa ukaguzi wa shule kwa kuzingatia makundi ya ubora ambapo shule zilizo
chini ya kiwango zitakaguliwa mara nyingi zaidi ili kuinua kiwango chake cha ubora.
Kwa mantiki hiyo Idara hii inatakiwa iimarishwe zaidi ili iweze kufuatilia na kuimarisha
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
31
viwango vya ubora wa elimu inayotolewa katika zekta nzima ya elimu. (Taarifa ya
Utafiti Kuhusu Kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya
Msingi, Mwaka 2008)
2.6.4 Ngazi ya Shule
Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na rekebisho lake Na. 10 la mwaka 1995 na
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 zinaeleza kuwa shule zote za sekondari
zinatakiwa kusimamiwa na Bodi za Shule ambapo wajumbe wake huteuliwa kwa
kuzingatia kanuni za uteuzi wa Bodi za Shule (The School Board Establishment Order,
1979 na GN. Na. 137 ya 1979). Aidha, kila shule ya sekondari inayo Timu ya
Menejimenti ambayo inaundwa na Mkuu wa Shule, Makamu wa Mkuu wa shule,
Mhasibu wa Shule, Mwalimu Mwandamizi Taaluma na Mwalimu Mwandamizi Nidhamu.
Tafiti za kielimu kuhusu ufaulu wa wanafunzi zinadhihirisha kuwepo uhusiano wa
ufuatiliaji kwa upande mmoja na mafanikio ya shule na kiwango cha ufaulu wa
wanafunzi kwa upande mwingine. Shule zenye mafanikio ni zile ambazo Wakuu wa
shule hufuatilia na kusimamia kwa karibu taaluma na mchakato wa ufundishaji na
ujifunzaji (Taarifa ya Utafiti Kuhusu Kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa Mtihani wa
Kuhitimu Elimu ya Msingi, Mwaka 2008: uk. 26). Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa, shule
zenye kiwango kidogo cha ufaulu ni zile ambazo kuna kiwango Kidogo cha Ukaguzi
wa Shule na kutotekelezwa maoni ya Taarifa za Ukaguzi wa Shule, kutokuwapo kwa
ufuatiliaji wa mara kwa mara kutoka ngazi ya Halmashauri na pale ambapo jamii
hazijahamasishwa kushiriki kikamilifu katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao
shuleni.
Kutokana na changamoto nyingi zinazoikabili Idara ya ukaguzi wa shule, WEMU katika
utaratibu wake wa kuimarisha ukaguzi wa shule, imeandaa Mwongozo wa Usimamizi
wa shule kwa lengo la kuwawezesha wakuu wa shule na waratibu elimu kata, kama
wakaguzi wa ndani na wa karibu na shule, kuzisimamia ziweze kujiletea maendeleo
kitaaluma. Aidha, Wakuu wa Shule wanalo jukumu pia la kufuatilia ufundishaji na
ujifunzaji ndani ya shule kwa kufanya ukaguzi wa ndani wakati wote wa shule. Zaidi
ya hayo, katika ngazi ya shule, Timu za Menejimenti hutoa ushauri kwenye Kamati za
Maendeleo za Kata kuhusu Maendeleo ya ujenzi wa shule. Hivyo, Timu za Menejimenti
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
32
za shule, kwa kushirikiana na Bodi za Shule zina jukumu la kuhakikisha utekelezaji wa
Sera ya Elimu na Mafunzo inatekelezwa kwa ukamilifu na kuandaa taarifa za
utekelezaji za shule na kuziwasilisha kwenye Halmashauri zao (SEDP II, 2010)
2.7 Mtaala na Utekelezaji
Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inaeleza kuwa kila mfumo wa elimu ni lazima uwe
na mitaala ya shule kukidhi mahitaji ya kielimu katika taifa husika. Mtaala
umegawanyika katika maeneo manne muhimu ambayo ni malengo na madhumuni ya
mtaala; maudhui au mada; vitendo vya kufundishia na kujifunzia; na upimaji au njia
za kupima mafanikio. Aidha, Taasisi ya Elimu ya Tanzania itawajibika kwa maandalizi,
maendeleo, utoaji, ufuatiliaji na tathmini ya mitaala ya elimu ya awali, msingi,
sekondari na ualimu (Sera ya Elimu na Mafunzo 1995, uk. 38-42).
2.7.1: Utayarishaji wa Mitaala
Mitaala huandaliwa na kuendelezwa ili kufikia malengo ya elimu katika ngazi zote na
kuboreshwa ili kukidhi mabadiliko na mahitaji mbalimbali ya jamii husika (TIE, 2008).
Osaki (1996) anaeleza kwamba tokea 1968 hadi 1996, kulikuwa na jitihada ndogo
kwa Taasisi ya Elimu kutafsiri falsafa ya Elimu ya Kujitegemea ya 1967 kwenye
masomo kama Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Pia, maudhui ya msingi katika
mitaala ilibakia ni ile ile bila kuzingatia ubunifu, umakinifu (critical thinking), na udadisi
ambayo imeonesha katika maandiko yaliyotayarishwa na kuanza kutumika bila hata
kupitia katika hatua ya kujaribiwa.
Mwaka 2003, Taasisi ya Elimu Tanzania ilitayarisha Mwongozo wa Ukuzaji Mitaala
(National Curriculum Development Framework-NCDF) (TIE, 2003) kuhusu namna
ambavyo mitaala ya Tanzania inavyotayarishwa na kutekelezwa. Mwongozo huu
ulitayarishwa ili kutumiwa na serikali na wadau wote wa elimu katika utekelezaji wa
mitaala. Aidha kwa elimu ya sekondari, maeneo ya ufundishaji na ujifunzaji katika
mitaala ni Lugha, Maarifa ya jamii, Sayansi, Teknolojia na Hisabati. Pia mwongozo
(NCDF, 2003) umeonesha mchakato/hatua za kufuata wakati wa kuboresha mtaala
ambazo zinajumuisha:-
 Kufanya tathmini ya awali (assessment) ya mtaala uliopo;
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
33
 Kubadilisha mtaala kwa kuboresha mihtasari, vitabu (kiada na ziada), vifaa;
zana na vifaaa vya masikizi maono;
 Kujaribisha mtaala na vifaa vya kufundishia na kufanya maboresho;
 Utekelezaji wa mtaala mpya katika shule; na
 Ufuatiliaji na tathmini ya mtaala ulioboreshwa.
Mchakato wa kurekebisha mtaala nchini Tanzania hujumuisha kazi ya kufanya utafiti
kwa kushirikisha wataalamu na wadau mbalimbali. Kulingana na maelezo ya Waziri
wa Elimu na Utamaduni (Juni, 2005) na utafiti wa TET wa mwaka 2003-2004,
mchakato wa kurekebisha mtaala ulihusisha washiriki katika ngazi mbalimbali kama
vile: Viongozi wakuu wa kielimu kitaifa; Wanasiasa na watumishi wa serikali;
Wahadhiri wa vyuo vikuu; Wakaguzi wa shule; maafisa mitihani; Walimu wa
sekondari, Wanafunzi; Wanapaneli wa masomo yote; Wakufunzi wa vyuo vya ualimu;
wakuu wa wilaya; Maafisa Elimu wilaya; Wakurugenzi watendaji wa wilaya, manispaa
na majiji; Viongozi wa madhehebu na mashirika ya dini; Viongozi wa mashirika yasiyo
ya kiserikali; na Viongozi wa Taasisi za wenye ulemavu. Wahusika na wadau hawa au
baadhi yao hutumika pia wakati wa kufanya tathmini ya mtaala ili kubaini mapungufu
na mikakati ya kuuboresha.
2.7.2: Uboreshaji wa Mitaala
Mwongozo wa ukuzaji mitaala (NCDF, 2003) unaonesha kwamba kuna mzunguko wa
mtaala (curriculum circle) kwa kila ngazi ya elimu. NCDF Uk.20 unaeleza kwamba
urefu wa mzunguko wa mtaala ni sawa na idadi ya miaka ya kukamilisha ngazi husika
ya elimu, mfano kwa sekondari ni miaka sita. Muda zaidi ya huu unapaswa kupita
kabla ya mtaala husika haujafanyiwa maboresho. Lengo la kubadilisha mitaala ni
kuingiza maarifa mapya ya kielimu na kiteknolojia, kuondoa maudhui na njia za
kufundishia zilizopitwa na wakati ili kukidhi mahitaji ya kitaifa.
Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE, 1991) ilifanya tathmini ya kitaifa kuhusu ubora wa
mitaala ya Elimu ya Msingi, Sekondari na Ualimu mwaka 1991. Matokeo yalionesha
kwamba mitaala ya masomo ilikuwa na mapungufu katika ngazi za elimu ya msingi,
sekondari na vyuo vya ualimu. Mapungufu yalitokana na kutofikiwa kwa malengo kwa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
34
sababu ya walimu kutumia njia ya mhadhara katika ufundishaji, kuwepo kwa mada
nyingi za mitaala, upungufu wa walimu, miundombinu, vifaa, vitabu na maabara.
Kufuatana na moduli ya Mtaala wa Sekondari wa Tanzania Bara (Secondary
Education Curriculum for Tanzania Mainland) (TIE, 2008), mitaala ya Tanzania
imebadilishwa na kuboreshwa kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 2.3
Jedwali Na. 2.3 Miaka ya mabadiriko ya mtaala na sababu zake
Na Mwaka Sababu ya Mabadiliko
1 1963 Kuingiza historia za kimila na fasihi katika elimu.
2 1976 Kukidhi utekelezaji wa dhana ya Elimu ya Kujitegemea
iliyoainishwa katika Azimio la Arusha mwaka 1967.
3 1979 Kuanzisha masomo ya michepuo.
4 1984 Kuingiza masuala ya kijamii
5 1996/1997 Kuingiza elimu ya mazingira na mahitaji ya Taifa na kimataifa
6 2005 na
2007
Mtaala uliboreshwa kwa sababu zifuatazo:
(i) Mtaala wa mwaka 1997 ulikamilisha mzunguko wake wa
kutumika kwa kipindi cha miaka 6 na zaidi;
(ii) Kuzingatia matakwa ya sera na programu za kielimu;
(iii) Kuzingatia matakwa ya soko huria kama vile ajira
katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi;
(iv) Mapendekezo ya tafiti za kielimu;
(v) Mahitaji ya Sayansi na Teknolojia;
(vi) Mahitaji na matakwa ya jamii kwa sasa; na
(vii) Kuingiza masuala Mtambuko.
Chanzo: Unit One: The revised O-level and A-level secondary education Curriculum
(TIE, 2008).
Maeneo yaliyoboreshwa katika mtaala wa shule za sekondari mwaka 2005 na 2007
yamezingatia Ujuzi (competences) katika ufundishaji na ujifunzaji; Njia na mbinu
shirikishi zinazomjali mwanafunzi na zinazomjengea ujuzi; Upimaji wenye kumjali
mwanafunzi; Kutorudia mada/maudhui yanayofanana katika masomo tofauti;
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
35
Kuanzishwa kwa somo jipya la TEHAMA; na kuongezwa mada za masuala mtambuko;
Mpangilio na mtiririko wa maudhui katika ngazi tofauti na ufaraguzi (improvisation) wa
zana za kufundishia na kujifunzia.
2.7.3: Mafunzo Kabilishi (Orientation) ya Mtaala
Mafunzo kabilishi ya mitaala iliyoboreshwa hutolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania kwa
walimu na wadau wengine ili kufanikisha utekelezaji wa mitaala katika shule na vyuo.
(TET, Februari, 2011). Taarifa ya TET, (2011) katika kipindi cha mwaka 2007 hadi
2010 inaonesha kuwa mafunzo kabilishi juu ya mtaala ulioboreshwa yalitolewa kwa
walimu 833 wa shule za sekondari zisizo za serikali katika mikoa ya Dar es Salaam,
Tanga na Dodoma. Aidha taarifa hiyo inaeleza TET ilitoa mafunzo kabilishi kwa
walimu 40 wa shule za sekondari za serikali mwezi Februari 2011 katika mikoa ya
Mwanza, Mtwara, Iringa, na Arusha ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo
ya Sayansi, Hisabati na Lugha.
Aidha, mwaka 2010, mafunzo ya wakufunzi wa vyuo vya ualimu wa ngazi ya
stashahada yalitolewa kwa wakufunzi 72 juu ya utekelezaji wa mitaala iliyorekebishwa
na matumizi ya mbinu shirikishi. Pia, mwaka 2010, kulikuwa na mafunzo kwa washiriki
12 (wakuza mitaala saba, Afisa wa WEMU mmoja, ADEM wawili, na TEWW wawili),
yaliyohusu matumizi ya TEHAMA katika kujenga ujuzi wa kutengeneza maudhui ya
kielektroniki kwa masomo ya sekondari. Utafiti uliofanywa na Meena (2009),
unathibitisha kuwa mafunzo kabilishi yanapewa umuhimu mdogo kwa kusema
“Serikali imeweka uzito mdogo kwenye elimu ya mafunzo kabilishi ya walimu
na kwamba walimu wanahitaji kujifunza kuhusu mitaala wakiwa kazini kwa
kuzifanya shule ziwe ‘taasisi za kujifunzia’”
2.7.4: Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji Mitaala
2.7.4.1: Tathmini ya Utekelezaji Mitaala
Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE- Secondary Education Curriculum for Tanzania
Mainland, 2008) inaeleza misingi na taratibu ambazo tathmini ya mitaala hufanyika
nchini Tanzania. TET inaeleza kwamba mitaala inatakiwa kufanyiwa tathmini katika
hatua mbalimbali wakati wa utekelezaji ili kubainisha mafanikio, mapungufu na
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
36
changamoto. Inasisitizwa kwamba ni muhimu TET ikafanya ufuatiliaji na tathmini ya
utekelezaji wa mtaala ipasavyo kwa nia ya kubaini matatizo yanayojitokeza.
Tathmini ya mtaala imeelezwa kuwa ni mchakato wa kufanya uchunguzi wa mtaala ili
kupata mrejesho utakaosaidia kutoa maamuzi yatakayopelekea kufanya marekebisho,
maboresho ya mtaala kulingana na malengo ya taifa. Aidha, wanaopaswa kushiriki
katika tathmini ya mtaala ni WEMU, TET, Mashirika yasiyo ya kiserikali,
Asasi/Mashirika ya elimu na wadau wengine. TET (2008) inaeleza zaidi kuwa kuna
aina tatu za tathmini za mitaala. Tathmini ya awali (Situational Evaluation) ambayo
hufanyika kabla ya utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa. Tathmini hii inalenga
kutambua mahitaji yanayohitajika kabla ya kuanza kutekeleza mtaala shuleni.
Tathmini endelezi (Formative Evaluation) hufanyika kwa mpangilio maalum wakati
mtaala unatekelezwa shuleni kwa lengo la kubaini mafanikio, matatizo na mapungufu.
Tathmni hii hufanyika katika ngazi ya taifa, wilaya/mkoa/kanda na katika ngazi ya
shule. Wahusika wakuu ni walimu, maafisa elimu, wakaguzi wa shule, asasi na
wataalamu binafsi.
Tathmini tamati (Summative Evaluation) hufanyika wakati wa mwisho wa mzunguko
wa mtaala (curriculum review circle). Kwa Tanzania tathmini hii inapaswa kufanyika
angalau baada ya miaka minne kwa sekondari ya kawaida (Secondary O-level) na
miaka miwili kwa sekondari ya juu (Secondary A-Level). Tathmini hii hufanyika pia
wakati wowote ikiwa kuna ulazima kutokana na mahitaji ya kijamii, kisiasa,
kimaendeleo, kushuka kwa kiwango kikubwa cha ubora wa elimu, pamoja na
mabadiliko katika Sera ya Elimu nchini.
TET, 2003 inaeleza kuwa katika ngazi ya shule walimu na wanafunzi wanapaswa
kufanyiwa tathmini. Tathmini hii inafanyika kwa mwalimu kujitathmini na kumtathmini
mwanafunzi wake, na pia mwanafunzi kujitathmini na kumtathmini mwalimu wake.
2.8 Mitihani
2.8.1: Mitihani Ngazi ya Shule
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
37
Kwenye kila ngazi ya elimu, hutolewa aina mbalimbali ya mazoezi na mitihani
inayotungwa na mwalimu ili kutosheleza makusudio mbalimbali ya kielimu (URT: ETP,
1995). Mwaka 1976 iliamuliwa kuanza kutumia mazoezi endelezi (Continuous
Assessment) ambapo kila shule huendesha mitihani na majaribio mbalimbali na
kuhifadhi alama za mwanafunzi kulingana na mwongozo wa mazoezi endelezi
uliotolewa na NECTA (NECTA: Guidelines on the Conduct and Administration of
Continuous assessment in Secondary Schools and teacher Training Colleges, 1990).
Kulingana na mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi, kuanzia mwaka 1990,
majaribio yatatumika badala ya utaratibu wa awali wa kutumia mazoezi na majaribio
katika mchakato wa kutayarisha alama za mazoezi endelezi. Kwa madhumuni ya
mazoezi endelezi, mwongozo unaelekeza kuwa, kila shule itaandaa jaribio moja kwa
kila mwisho wa muhula, ambapo Baraza la Mitihani linaweza kuhitaji kupatiwa nakala
za majaribio hayo. Ili kukidhi matakwa ya mazoezi endelezi, mwongozo unaelekeza
kuwa kutakuwa na jumla ya majaribio manne katika shule za sekondari ambapo
mtihani wa Kidato cha 2 utakuwa sehemu ya mazoezi endelezi (WEMU: Waraka wa
Elimu Na. 5 1999).
Majaribio mengine ambayo yatakuwa sehemu ya mazoezi endelezi ni yale ya kila
mwisho wa muhula Kidato cha 3 na jaribio la mwisho wa muhula wa kwanza Kidato
cha nne (NECTA: Guidelines on the Conduct and Administration of Continuous
assessment in Secondary Schools and teacher Training Colleges, 1990). Wakuu wa
shule wanatakiwa kutunza alama za kila mwanafunzi ambazo zitatakiwa kujazwa
kwenye fomu maalumu ya NECTA kwa madhumuni ya mazoezi endelezi. Imewekwa
wazi katika mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi kuwa, wakuu wa shule
watawasilisha NECTA alama za matokeo ya mtihani wa Kidato cha 2 na alama za
muhula wa kwanza na wa pili Kidato cha 3 na muhula wa kwanza Kidato cha 4 katika
kipindi cha miezi mitatu kabla ya mitihani husika kufanyika.
Katika ngazi ya shule kutakuwepo pia upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi kwa
kutumia Projekti. Kulingana na mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi,
ufundishaji na ujifunzaji pamoja na tathimini ya maendeleo ya taaluma kwa njia ya
projekti, hulazimika kufanyika kutokana na matakwa ya mfumo wa elimu na maamuzi
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
38
ya kisiasa ambayo yamekuwa msingi wa mabadiliko katika mitaala ya shule. NECTA
huhimiza upimaji kwa kutumia Projekti kama njia ya kuimarisha ujifunzaji na kupima
mafanikio katika ujenzi wa uwezo na ujuzi wa wanafunzi (NECTA: Guidelines on the
Conduct and Administration of Continuous assessment in Secondary Schools and
teacher Training Colleges, 1990).
2.8.2: Mitihani ya Taifa
Kulingana na Sera ya Elimu na Mafunzo (URT ETP, 1995 p. 44) sera zifuatazo
zitatumika kuongoza mitihani kwenye ngazi ya kanda na taifa: itakuwepo mitihani ya
kitaifa mwishoni mwa Darasa la VII, Kidato cha 4, Kidato cha 6 na kozi za mafunzo ya
Ualimu za Cheti na Stashahada. Aidha, mitihani ya Darasa la VII, Kidato cha 4 na
Kidato cha 6 itaashiria kuhitimu katika ngazi ya elimu ya msingi na sekondari na
matokeo ya mitihani hii yatatumika kwa uchaguzi wa wanafunzi watakaoendelea na
elimu ya juu na mafunzo zaidi, na pia kwa kutolea cheti cha kuhitimu elimu ya ngazi
inayohusika. Baraza la Mitihani la Tanzania litawajibika kutunga, kudhibiti, kuendesha
na kusimamia mitihani ya taifa ya Darasa la VII, Kidato cha 4 Kidato cha 6 na
mafunzo ya Ualimu ya Cheti na Stashahada (URT: ETP, 1995 )
Sera ya Elimu na Mafunzo 1995 imeeleza kuwa, katika ngazi ya elimu ya sekondari,
upo Mtihani wa Taifa wa kidato cha pili ambao hutumiwa kwa kubashiri maendeleo
halisi na kwa ajili ya kupata upimaji wa kuendelea katika elimu ya sekondari ya ngazi
ya kawaida.
2.8.3: Muundo wa Mitihani
Waraka wa Elimu Na. 1 wa mwaka 2006 umefafanua masomo ya msingi na masomo
chaguzi ambayo wanafunzi wanatakiwa kusoma na kufanyia mitihani kwa Kidato cha
4. Aidha, Mwongozo kuhusu muundo wa mitihani, ambao unajumisha masomo yote
yanayotahiniwa unatoa msaada kwa watumiaji na walimu kuhusu taratibu za mitihani
hususani matumizi ya chati ya maelekezo (Table of Specifications) katika kuandaa
mitihani (NECTA, Certificate of secondary Education Examination Format, February,
2008).
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
39
NECTA hupeleka nakala ya mwongozo wa mitihani kwa wakuu wa shule na vituo
vyote vya mitihani ili kusaidia wanafunzi na walimu kujiandaa kwa mitihani. Kulingana
na mwongozo huo, Muundo wa mitihani umegawanyika katika sehemu tano ambazo
ni: utangulizi, malengo ya jumla, ujuzi wa jumla, utaratibu wa mitihani (examination
rubric) na maudhui ya mtihani. Unyeti wa muundo wa mitihani unasaidia watunzi
(examination setters) na warekebishaji (moderators) wa mitihani, walimu na
wanafunzi katika kukabili mahitaji na ukamilishaji wa mtaala pamoja na ufahamu wa
maarifa na ujuzi (NECTA, Certificate of secondary Education Examination Format,
February, 2008).
2.8.4: Uendeshaji wa mitihani
Sera ya Elimu na mafunzo 1995 inafafanua kuwa, Baraza la Mitaihani la Tanzania
litawajibika kutunga, kuthibiti, kuendesha na kusimamia Mitihani ya Taifa ya Darasa la
VII, Kidato cha 4, Kidato cha 6 na Mafunzo ya Ualimu ya Cheti na Stashahada (URT:
ETP, 1995). Aidha NECTA itahusika pia na kutunga, kudhibiti, kuendesha na
kusimamia Mtihani wa Maarifa (Qualifying Test) kwa watahiniwa walio nje ya mfumo
wa shule. NECTA huendesha mitihani katika misimu mitatu ambapo mwezi Oktoba
mitihani ya maarifa na ya Kidato cha 4, mwezi Februari mitihani ya Kidato cha 6 na
mwezi Mei mitihani ya Stashahada na Cheti cha ualimu, stashahada za juu za ufundi
na mwezi Septemba mtihani wa kuhitimu Darasa la VII (NECTA WEBSITE, May 2011,
NECTA: The Examinations Regulations, 2006).
2.8.5: Utungaji
Kulingana na NECTA WEBSITE, May 2001, watungaji wa mitihani wanatakiwa wawe
wamebobea kitaaluma katika masomo husika ambayo yanatahiniwa. Aidha,
wanatakiwa wawe wanafundisha na uzoefu wa kufundisha katika ngazi wanayotahini
kwa muda usiopungua miaka mitatu. Website hiyo inafafanua kuwa, kila mwaka,
Baraza la mitihani la Tanzania hupeleka fomu ya kupata orodha ya watungaji wa
mitihani katika shule zote ambapo wakuu wa shule hutakiwa kutuma taarifa za siri
kuhusu uwezo na uaminifu wa mwalimu katika kutunza siri na kuonesha namana
anavyojituma kazini. Baada ya kupata taarifa za siri za walimu, NECTA huteua walimu
wa kutunga mitihani ambao hutakiwa kuandaa jozi mbili za karatasi za mtihani. Aidha,
barua za uteuzi wa watungaji wa mitihani humwelekeza mtunzi mambo ya kuzingatia
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
40
wakati wa kutunga maswali ya mtihani na pia huambatanishwa na muundo wa
mtihani ili arejee ipasavyo.
Kimsingi watungaji wote ambao wanateuliwa kutunga mitihani wanatakiwa wapatiwe
mfunzo ya msingi na mbinu za uandaji wa maswali mazuri ya mitihni. Hata hivyo
imeonekana kuwa hali hiyo haifanyiki na watungaji wa mitihani hutegemea utaalamu
kama walimu na uzoefu wao kazini (NECTA WEBSITE, May 2011).
Baada ya kupokea karatasi za mitihani kutoka kwa watungaji karatasi hizo hufanyiwa
marekebisho (moderation). Kwa kawaida marekebisho ya karatasi za mitihani
hufanywa na paneli ya watu 2-3 kwa kila somo. Karatasi za mitihani zinaandaliwa
zikionesha maelekezo kwa watahiniwa kuhusu idadi ya maswali wanayotakiwa kujibu
kwa kila somo na alama zinazotolewa kwa kila swali. Kama ilivyo kwa watungaji wa
mitihani, NECTA huteua warekebishaji baada ya kupokea taarifa za siri za walimu hao.
Kwa kawaida, wajumbe wa paneli za kurekebisha masomo ni watunga mitaala,
wakaguzi wa shule, wahadhiri katika vyuo vikuu na au walimu wazoefu ambao
hawashiriki kufundisha watahiniwa kwa wakati huo. NECTA 2011, imeeleza kuwa
warekebishaji wa mitihani hutakiwa kuzingatia kuwa mitihani inalingana na mihtasari
na suala la kuaminika (Reliability) na uhalali (Validity) umezingatiwa wakati wa
kuandaa mitihani. Aidha, wakati wa kurekebisha mithihani, huwasilishwa jozi tatu za
karatasi za mitihani kwa kila somo (NECTA WEBSITE, May 2011).
Baada ya kukamilisha kazi ya kurekebisha karatasi za mitihani, NECTA hurudufisha na
kuiandaa kwa ajili ya kuisambaza kwenye vituo vya mitihani. Website ya NECTA
inaonesha kuwa kazi ya kurudufisha na kuandaa katarasi za mitihani husimamiwa na
Idara ya Chapa na Uchapishaji wa mitihani ambapo jukumu la kuisafirisha mitihani
hiyo kwenda mikoani ni la Idara ya Kusimamia na Kuendesha Mitihani (Departmend of
Examinatios Administration). Aidha, usambazaji wa mitihani hufanyika kwa kutumia
misafara inayotumia barabara, reli, bahari na ndege. Katika hatua hii suala la ulinzi na
usalama wa mitihani hupatiwa umuhimu wa kipekee ambapo vyombo vya usalama
vya serikali hushirikishwa. Misafara kwa njia ya barabara hushirikisha Afisa wa
Mitihani, Askari mwenye siraha, Afisa usalama na dereva kutoka NECTA.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
41
Kulingana na Website NECTA, misafara ya kupeleka mitihani kutoka ofisi za NECTA
huishia katika makao makuu ya Mikoa ambapo Afisa Mitihani hukabidhi mitihani
kwenye Kamati ya Mitihani ya Mkoa. Mitihani hupokelewa na kuhifadhiwa katika
chumba madhubuti (Strong room) cha mkoa na kulindwa na askari mpaka
itakapopelekwa wilayani.
Kamati ya Mitihani ya Mkoa husafirisha na kukabidhi mitihani kwa Kamati ya Mitihani
ya Wilaya. Kama ilivyo katika mkoa, mitihani inahifadhiwa katika vyumba maalumu
vyenye usalama na vinalindwa na maaskari wenye silaha. Kutoka katika ngazi ya
wilaya, mitihani hukabidhiwa kwa wakuu wa shule na wasimamizi wa nje wa mitihani
(external supervisors) na kuhifadhiwa katika vyumba vyenye usalama katika maeneo
yao na italindwa na askari wenye silaha.
2.8.6: Usahihishaji na Utoaji wa Matokeo
Sera ya Elimu na Mafunzo imeeleza kuwa, kutokana na mitihani kuathiri maisha ya
watu, malalamiko hayatakosekana kuhusu utungaji, uendeshaji, usimamizi,
usahihishaji, uandaaji wa matokeo; upangaji wa madaraja, tuzo pamoja na utoaji
matokeo. Mchakato wa kusahihisha na kutoa matokeo ya watahiniwa umegawanyika
katika hatua tatu ambazo ni: kwenye vituo vya mitinani, kwenye vituo vya usahihishaji
na ofisi za NECTA (NECTA: Examinations Processing, July, 1986).
Karatasi za Mitihani za watahiniwa hupokelewa kutoka kwenye vituo vya mitihani na
kupelekwa kwenye vituo vya usahihishaji na alama za matokeo kupelekwa ofisi za
NECTA kwa maandalizi ya matokeo ya watahiniwa kwa madaraja mbalimbali ili kutoa
matokeo ya watahiniwa (NECTA: Examinations Processing, July, 1986).
Kulingana na taratibu za mitihani za NECTA, katika Vituo vya Mitihani, orodha za
watahiniwa huandaliwa, alama za mazoezi endelezi na projekti huingizwa kwenye
fomu za mazoezi endelezi na majumuisho ya alama za mazoezi hufanyika. Katika vituo
vya usahihishaji, usahihishaji wa karatasi za mitihani za watahiniwa hufanyika kwa
kutumia paneli za masomo na alama za mtihani wa mwisho hukokotolewa kwa
kiwango cha asilimia 50. Katika Ofisi za NECTA, kimsingi, alama za mazoezi endelezi
hukokotolewa na kujumishwa na alama za mtihani wa mwisho ili kupata alama za
matokeo kwa watahiniwa (NECTA: Examinations Processing, July, 1986).
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
42
Kulingana na taratibu za mitihani (NECTA, 1986), matokeo ya mwisho ya mtihani wa
Taifa wa Kidato cha 4 yanatolewa kwa kutumia viwango vya ufaulu (Gredis) A, B, C, D
na F ambapo A-Ubora uliotukuka, B-Vizuri sana, C-Vizuri, D-inaridhisha na F-feli.
Uzito wa ‘gredi’ hizo ni A – 1 (krediti), B – 2 (krediti), C – 3 (krediti), D – 4 (kufaulu),
F – 5 (feli). Uzoefu unaonyesha kuwa Gredi hizi zinatolewa kwa kuzingatia mlolongo
wa alama zifuatazo: A (81-100), B (61-80), C (41-60), D (21-40), F (0-20). Hata hivyo
rejea kutoka NECTA (Juni, 2011) zinaeleza kuwa Kamati ya Kutunuku ya NECTA
hubaini viwango vya ushindi katika mwaka husika baada ya kulinganisha viwango vya
ushindi kwa miaka mbalimbali iliyopita ilikilinganishwa na uwezo wa ufaulu wa
watahiniwa wa mwaka husika. Aidha, kulingana na kanuni za kutoa ushindi wa alama
kwa mtihani wowote unaoendeshwa na NECTA, hakuna mtahiniwa yeyote
atakayeweza kupata gredi A katika somo kama atapata alama chini ya 70. Vilevile
hakuna mtahiniwa atakayepata gredi D endapo atapata alama chini ya 30.
Aidha, matokeo yatatolewa kwa kutumia madaja ya ufaulu (Divisions) I, II, III IV na 0
kwa kuzingatia masomo saba yenye ufaulu wa juu ukijumuisha yale ya msingi (core
subjects). Daraja la I (alama 7 – 17), Daraja la II (alama 18 – 20), Daraja la III
(alama 21 – 25) na Daraja la IV (alama 26 – 32). Daraja la 0 (alama 33-35) inaashiria
kufeli.
2.8.7: Mchango wa CA na Project katika Mitihani ya Taifa
Kabla ya mwaka 1976, Tanzania ilitumia mitihani ya mwisho kama njia pekee ya
kupima na kutathimini watahiniwa. Aidha, mfumo uliokuwa unatumika wakati wa
kikoloni ulikosolewa na wadau wa elimu kutokana na kutokuwa thabiti katika kupima
mafanikio ya jumla ya kielimu ya mwanafunzi w Kitanzania. Kwa hiyo, mwaka 1976,
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) lilianzisha mfumo wa kutumia mazoezi
endelezi (Continuous Assessment) kama njia ya kutatua kasoro na mapungufu
yaliyokuwepo katika mfumo wa upimaji uliokuwa unatumia mtihani mmoja wa mwisho
pekee (NECTA: Guidelines on the Conduct and Administration of Continuous
assessment in Secondary Schools and teacher Training Colleges, 1990, Lisu, H.S,
2008).
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
43
Kulingana na mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi (NECTA: 1990), ufaulu wa
mwanafunzi utapimwa kwa kutumia alama za mazoezi endelezi (CA) na alama za
Projekti ambazo zitajumuishwa kwenye mtihani wa mwisho Kidato cha 4. Aidha,
Mwongozo umeweka wazi kuwa mchango wa alama za mazoezi endelezi katika tuzo la
mwisho wa elimu ya sekondari Kidato cha 4 ni asilimia 45 na mchango wa Projekti
utakuwa asilimia 5 hivyo, kuwa na jumla ya alama asilimia 50 (NECTA: Examinations
Processing, July, 1986).
Mapitio ya machapisho yanaonesha kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa upimaji
wa kutumia CA, hakuna jitihada za kutosha zilizofanyika katika kuelimisha umma juu
ya mchango wa mazoezi endelezi (CA) katika matokeo ya mwisho ya mtahiniwa.
Aidha, mfumo huo hauoneshi njia zinazotumika katika kuandaa mazoezi hayo ya
darasani na namna gani mazoezi hayo yanasimamiwa na kuchambuliwa (Lisu, H.S,
2008). Taarifa ya utafiti uliofanywa na Lisu, H. S, 2008, inathibitisha kuwa wadau wa
elimu wakiwemo maafisa wa NECTA, walimu, wazazi, na wanafunzi hawajui
kiwango/mchango wa CA katika mtihani wa mwisho wa kuhitimu elimu ya sekondari.
Taarifa hiyo, pia imeonesha kuwa pamoja na juhudi za NECTA kupeleka vitabu vya
mwongozo wa NECTA wa mazoezi endelezi katika kila shule, vijitabu hivyo vilibakia
katika ofisi za taaluma na kuhifadhiwa kama nyaraka za siri na kwa matumizi ya
viongozi wachache tu. Aidha imeoneshwa kuwa alama za mazoezi endelezi zilikuwa
zina tolewa kwa upendeleo kwa baadhi ya wanafunzi. Kutokana na mapitio ya
machapisho imebainika kuwa alama za mazoezi endelezi (CA marks) na alama za
mtihani wa mwisho Kidato cha 4 hazijumulishwi na kutafuta wastani. Mchakato wa
kupata alama ya mwisho ya mtahiniwa inahusisha ukokotoaji wa kiwango sanifu cha
alama (standardization of raw marks) kabla ya kupata alama ya mwisho.
2.9: Upatikanaji na Usambazaji wa Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
2.9.1: Vitabu vya Kiada na Ziada
Miaka ya 1980, Shirika la Vifaa vya Elimu yaani “Tanzania elimu Supplies (TES) “chini
ya Wizara ya Elimu na Utamaduni lilikuwa na jukumu la kusambaza vitabu na vifaa
vya shule nchini (Tume ya Rais ya Elimu, 1982). Kuanzia Januari mwaka 1992 Serikali
ilipitisha sera ya upatikanaji na usambazaji wa vitabu vya shule na vyuo nchini
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
44
ambayo ilifuta Waraka no. EDTT/8/184 wa mwaka 1970 uliohusu “Uuzaji wa Vitabu
vya Kiada vinavyotayarishwa na Wizara ya Elimu”. Sera hii ilianzisha utaratibu wa
upatikanaji na usambazaji wa vitabu vya kiada na ziada kufanyika na makampuni ya
kibiashara ya uchapishaji kwa mtindo wa ushindani. Taasisi ya Elimu ilielekezwa
kubaki na majukumu ya ukuzaji mitaala kama lengo la muda mrefu, hii ni pamoja na
serikali kubaki na jukumu la kupitisha vitabu kwa matumizi ya shule na vyuo vya
ualimu.
Utekelezaji wa sera hii uliendana na utayarishaji wa utaratibu wa kuhakiki na kupitisha
vitabu vya kiada vya shule na vyuo kwa kufuata Waraka wa Elimu Na. 2 wa Agosti
1998 uliojulikana kama “New Approval System for Educational Books”. Waraka huu
ulikuwa na lengo la kuhakikisha ubora wa vitabu vitumikavyo shuleni. Mwaka 1998,
Kamati ya kutathimini Machapisho ya Kielimu (Educational Materials Approval
Committee -EMAC) ilianzishwa na Wizara ya Elimu. EMAC ipo chini ya uenyekiti wa
Kamishna wa Elimu na inaundwa na Sekretariati na wataalamu/ walimu mahiri wa
masomo (Book Evaluators). Taarifa ya EMAC (2011) inaeleza kuwa kufikia Aprili 2011
EMAC imetoa idhibati kwa aina za vitabu 248 vya elimu ya sekondari katika lugha ya
Kiingereza, ambapo aina 218 vya kiada na 30 vya ziada. Aidha, ithibati ilitolewa kwa
aina 65 ya vitabu vya sekondari katika lugha ya Kiswahili ikiwa 20 vya kiada na 45 vya
ziada vilivyoandikwa na wandishi tofauti na wachapishaji mbalimbali.
Vitabu vyote vya kiada vilivyopitishwa na EMAC vimeandikwa kufuata mtaala
ulioboreshwa mwaka 2005 na 2007. Shule zinapaswa kununua na kutumia vitabu vya
kiada na ziada vilivyopewa ithibati na EMAC (Miongozo ya MMES II, 2010). Shule
huagiza na kuvinunua kutoka maduka ya vitabu au kampuni za wachapishaji vitabu
moja kwa moja au kwa kuletewa shuleni kutoka makao makuu ya Wizara ya Elimu
kwa kupitia kwa Maafisa Elimu wa mikoa na Wilaya. Mpango wa Elimu ya Sekondari
(SEDP II, June 2010) umeonesha kuwa katika kipindi cha 2004 – 2009 wadau
wamekuwa wakitoa msaada wa vitabu kwa ajili ya shule na maktaba nchini ikiwa ni
pamoja na shirika la USAID lililotoa msaada wa vitabu 456,830, vya shule za
sekondari.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
45
Kulingana na Sera ya Elimu na Mafunzo 1995, ibara ya 5.4.6, kila shule inapaswa
kuwa na vitabu vya kutosha, maktaba na wakutubi wenye utaalamu. Hata hivyo hali
halisi inaonesha kuwa maktaba za shule ni chache kwani hadi mwaka 2009, ni
maktaba 57 tu zilikuwa zimejengwa kati ya maktaba 2,406 zilizokuwa zimepangwa
kujengwa chini ya mpango wa MMES (SEDP II, 2010).
2.9.2: Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
Ubora wa utoaji wa elimu unaimarishwa na upatikanaji na utumiaji wa zana na vifaa
vya kufundishia na kujifunzia. Vifaa hivi vinajumuisha machapisho (textual materials)
kama vitabu, ramani na chati. Aidha, vifaa vingine ni vile visivyochapishwa (non
textual materials) kama vile tufe, modeli na vifaa vya masikizi na maono.
Sera ya Elimu na Mafunzo (1995, Kifungu 4.5.3) inaelekeza kwamba shule zote za
sekondari zinapaswa kuwa na zana na vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia
ambavyo vipo katika idadi inayotosha mahitaji ya shule. Changamoto katika mchakato
wa ufundishaji wa masomo shule za sekondari ni upungufu mkubwa wa vifaa vya
kufundishia na kujifunzia (SEDP II, 2010). Kulingana na Mtaala wa Sekondari kwa
Tanzania Bara uliotayarishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (2008), mwalimu
anatazamiwa kuwa mbunifu wa kutengeneza na kufaragua vifaa vya kufundishia na
kujifunzia kwa kutumia vitu vipatikanavyo katika mazingira ya shule.
2.9.3: Maabara, Vifaa na Madawa ya Maabara
Ufundishaji wa masomo ya Sayansi unazingatia sana vitendo ili wanafunzi wapate
maarifa, stadi na ujuzi unaotakiwa katika mitaala. Maabara za sayansi zilizosheheni
vifaa yakiwemo madawa ndiyo nyenzo muhimu katika kuwezesha ufanyaji wa vitendo
kwa wanafunzi na walimu. Umuhimu huo umesisitizwa katika Sera ya Elimu na
Mafunzo (1995) na Mpango wa Mkakati wa Kati (Medium Term Strategic Plan,
2007/08-2009/10) wa WEMU uliobainisha lengo la kuweka vifaa vya kutosha katika
maabara za sayansi katika shule za sekondari.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
46
Kulingana na taarifa ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Idara ya Sekondari
(2008), mahitaji ya maabara za sayansi yalikuwa 9,420 kwa shule 3,140 za sekondari
za serikali. Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 77 ya shule za serikali hazina
maabara za sayansi kama ilivyooneshwa katika jedwali Na.2.4
Jedwali Na 2.4 Hali ya Maabara katika shule za Serikali Tanzani mwaka
2008
Aina ya shule
Idadi ya
Shule
Shule
zenye
Maabara
Hali ya maabara katika shule
Zilizo na
Hali
nzuri
Zinazohitaji
matengenezo Upungufu
Shule za Kitaifa 90 90 - 90 -
Shule za Jamii 3,051 639 36 603 2,412
Jumla 3,141 729 36 693 2,412
Asilimia 100% 23% 1% 22% 77%
Chanzo: Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Idara ya Sekondari, Disemba 2008
Kila shule ya sekondari inatakiwa iwe na maabara za masomo ya sayansi. Taarifa za
WEMU kwa mwaka 2010 zinaonesha kuwa Katika shule za sekondari 4,266 za serikali
na zisizo za serikali, kulikuwa na maabara za Baiolojia 670, Kemia 804, Fizikia 760 na
Kompyuta 1,540 hali inayoashiria upungufu wa maabara.
2.10: Mazingira ya Shule
Mazingira ya shule yanahusu jumla ya vitu vyote vilivyopo na vinavyotendeka nje na
ndani ya darasa katika shule. Mazingira hayo, ni pamoja na miundo mbinu, samani
zake na huduma za jamii.
2.10.1: Miundombinu na Huduma za Kijamii
Tume ya Rais (1982) ilibaini ongezeko kubwa la shule bila kuwepo na miundombinu
iliyokamilika. Kutokana na hali hii, Tume hiyo ilipendekeza kuwepo kwa kitabu cha
Mwongozo kitakachosaidia viongozi kuwa na msimamo mmoja kuhusu aina ya
majengo, madarasa na vitu vingine vya lazima kwenye shule za msingi, sekondari na
vyuo vya ualimu.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
47
Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inabaini pia ongezeko la shule kutokana na
misukumo ya kisiasa au kwa ushindani miongoni mwa wazazi, mashirika yasiyo ya
kiserikali au uongozi katika wilaya na kusajili shule bila kuzingatia mahitaji ya kiwango
cha chini kilichowekwa kwa ajili ya majengo ya shule za sekondari iliyotolewa kwenye
Mwongozo wa uanzishaji shule. Katika Ibara ya 5.4.3. Sera inaelekeza kuwa:
Wamiliki na viongozi wote wa shule za sekondari watahakikisha kuwa majengo, vifaa,
zana na vifaa vya kufundishia ambavyo ni vya lazima kwa kufundishia na kujifunzia
kwa ufanisi kwa kiwango cha juu na bora vinapatikana katika idadi inayotosheleza na
vinakarabatiwa mara kwa mara. (uk.31).
Mwaka 2001, Idara ya Sera na Mipango ilitoa Mwongozo wa Majengo na Samani
kuhusiana na ujenzi wa shule za sekondari. Majengo haya ni pamoja na: Jengo la
Utawala (unajumuisha ofisi ya Mkuu wa shule pamoja na msaidizi wake, ubao wa
matangazo ya shule, vyoo vya utawala, ofisi ya walimu), madarasa, nyumba za
wafanyakazi, vyoo, maabara, maktaba, mabweni, bwalo la kulia chakula, jiko na stoo,
chumba cha kupumzikia wagonjwa (sick bay), viwanja vya michezo na barabara
zinazopitika. Aidha vipimo vya ukubwa wa kila jengo viliainishwa.
Mwaka 2007, WEMU ilielekeza mambo ya kuzingatia katika kuanzisha shule za
sekondari za kutwa zinazojengwa kwa nguvu za wananchi kuhusiana na miundo
mbinu. Mwongozo ulielekeza Halmashauri kuzingatia mahitaji yafuatayo: madarasa
mawili, jengo la utawala moja, vyoo matundu mawili kwa watumishi, matundu
matano kwa ajili ya wanafunzi (wasichana matundu matatu na wavulana matundu
mawili), maabara ya sayansi moja, stoo mbili za vifaa na nyumba tatu za walimu. Hii
ilikuwa hatua ya muda mfupi iliyochukuliwa na Serikali kusaidia wananchi kuanzisha
shule katika maeneo yao, ili kukabili hitaji la kuwa na shule zaidi za sekondari. Pamoja
na kuchukua hatua hizi, mategemeo ya serikali ni kwamba shule zilizoanzishwa kwa
njia hii, zitajiimarisha kadri siku zinavyokwenda na kuhakikisha zinaendelea
kujitosheleza katika mahitaji yote yaliyoainishwa mwaka 2007.
2.10.2: Samani
Samani huenda sambamba na mahitaji ya wanafunzi na walimu. Samani hizi ni
pamoja na madawati na viti kwa ajili ya madarasa, meza, mbao za darasani, mbao za
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
48
matangazo, viti, makabati, meza za chai, na samani za majengo yote mengine katika
shule. Katika mwaka 2001, Idara ya Sera na Mipango (WEMU) ilitoa Mwongozo wa
Samani kuhusiana na ujenzi wa shule za sekondari. Mwongozo huo ulianisha samani
za kila jengo ambazo zinaendana na mahitaji ya wanafunzi pamoja na walimu wao.
Aidha, uchaguzi wa samani unatakiwa uzingatie umri, ulemavu pamoja na kiwango
cha elimu inayotolewa katika shule husika.
Mwaka 2007 WEMU ilielekeza samani (madawati 80 na viti 80, meza za darasani mbili
na viti viwili) kwa shule ya mikondo miwili zilizokuwa zinajengwa kwa nguvu za
wananchi.
2.11. Uandaaji na Upatikanaji wa Walimu
Walimu ni Nguvu Kazi muhimu katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Mafunzo
ya walimu humuandaa mwalimu kitaalamu na kitaaluma. Kada ya walimu nchini
Tanzania imegawanyika katika sehemu kuu tatu: cheti, stashahada na shahada.
Mafunzo ya walimu yamegawanyika katika sehemu kuu mbili: Mafunzo Tarajali (Preservice)
na Mafunzo Kazini (In-service).
2.11.1: Mafunzo Tarajali
Mafunzo tarajali ni mafunzo ya awali ambayo hutolewa kwa mwanachuo anaye
andaliwa kuwa mwalimu katika ngazi yoyote ya elimu kulingana na sifa alizonazo. Sifa
na muda wa mafunzo ya Ualimu katika ngazi zote za elimu zimekuwa zikitofautiana
kutoka kipindi kimoja hadi kingine kulingana na mahitaji ya wakati huo.
Mara baada ya uhuru, Wizara ya Elimu iliamua kupanua elimu ya sekondari, ili kuweza
kupata watumishi wa sekta mbali mbali za maendeleo ya uchumi. Kwa hali hiyo
Serikali ilihitaji walimu wa kutosha ili waweze kuwaandaa wataalamu hao katika
kiwango cha sekondari. Kutokana na ukosefu wa walimu wa kutosha, muda wa
mafunzo ya Ualimu katika ngazi ya Stashahada ulipunguzwa kutoka miaka miwili na
kuwa na mwaka mmoja chuoni na miezi sita ya mazoezi nje ya chuo. Waombaji wa
kozi hii walikuwa wahitimu wa Kidato cha 6. Aidha, wanafunzi wa Chuo Kikuu,
walishawishiwa kuchukua mafunzo ya Ualimu. (Tume ya Rais ya Elimu, 1982, 5.7 uk.
225).
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
49
Tume ya Rais ya Elimu ya mwaka 1982 ibara ya 3.116 ilipendekeza kwamba ’Walimu
wa sekondari na vyuo vya ufundi wawe na Stashahada na Shahada wakati wale wa
ufundi sadifu wawe wenye cheti cha elimu ufundi mchundo (Full Technician
Certificate’ F.T.C.) Lengo kwenye shule za sekondari kuwe na walimu wenye shahada.
uk. 147. Katika miaka ya 70, sifa za waliojiunga na Stashahada ilikuwa mhitimu wa
Kidato cha 6, na kupata ufaulu si chini ya ‘Subsidiary’ mbili. Muda wa mafunzo ulikuwa
miaka miwili. Kutokana na upanuzi wa shule za sekondari, mwishoni mwa miaka ya 80
hadi mwaka 1991, Wizara ya Elimu ilianzisha utaratibu ambao uliruhusu wanafunzi
waliofanya vizuri Kidato cha 4 kuingia Kidato cha 5 na na mafunzo ya Ualimu. Vyuo
hivyo vilikuwa Mkwawa, Korogwe, Shinyanga na Monduli. Mwanafunzi alisoma kwa
miaka mitatu na baada ya hapo alipata cheti ngazi ya Stashahada na kwenda
kufundisha shule za sekondari. Hii ilikuwa jitihada ya makusudi ya Serikali kuhakikisha
kwamba wanaandaa walimu wenye ubora kitaalamu na kitaaluma.
Mwaka 2005, WEMU ilielekeza uimarishaji wa sifa na muda wa waliotaka kujiunga na
Kozi ya Stashahada ya Ualimu kuwa na sifa zifuatavyo: awe amehitimu Kidato cha 6,
na kupata ‘Principal Pass’ 2 au zaidi. Muda wa mafunzo kuwa miaka miwili. (Facts
About Basic Education in Tanzania, Final draft 2005).
Hata hivyo, Maelekezo ya Kamishna katika barua kumb.Na TTDB/85/483/01/25
mwaka, 2009 inaelekeza sifa zinazokinzana na zile za awali za 2005. Sifa za
wanaojiunga na mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada kuanzia tarehe 1, Julai ni
‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika masomo yanayofundishwa shule za
sekondari. Waraka huo pia unaelekeza Sifa kwa wanaojiunga na mafunzo ya
Stashahada ya Ualimu kwenye fani ya Ufundi kuwa itaendelea kuwa cheti cha Elimu
ya ufundi mchundo (FTC). Kwa lengo la kutoa fursa kwa wahitimu wenye ufaulu mzuri
katika masomo ya Sayansi na Hisabati, wasio na cheti cha Elimu ya ufundi mchundo
wamepewa nafasi kujiunga na Stashahada ya ualimu wa kawaida. Utafiti uliofanyika
na WEMU, 2006 umeonesha umuhimu wa kuboresha sifa za chini za kuingia katika
vyuo vya ualimu na kuimarisha kipindi cha mafunzo (The Teacher Management
Development Strategy 2008 - 2013). Kati ya mwaka 2004 -2007, Wizara ya Elimu
iliandaa Walimu wa Leseni 10,000 waliohitimu kidato cha 6. Walimu hawa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
50
waliandaliwa kwa kupewa mafunzo ya muda mfupi (induction course) ya wiki 4
ambayo yalilenga kuwapa kwa kiasi kidogo mbinu za kufundishia na kujifunzia na
uongozi katika elimu kabla ya kuruhusiwa kufundisha. Ngodu, 2007 anaielezea dhana
ya walimu wa leseni (Licensed Teachers) kuwa ni walimu ambao hawajasomea kozi ya
ualimu isipokuwa wanayo taaluma ya masomo kwa maana wamemaliza kidato cha
sita au wamesomea shahada zisizo za elimu. Uandaaji wa walimu hawa ni wa
dharura na ni njia mbadala ya kupata walimu kwa haraka kwa lengo la kupunguza
tatizo kubwa la walimu shuleni.
2.11.2: Mafunzo Kazini
Mafunzo kazini (In-service) ni mafunzo ambayo hutolewa kwa mwalimu aliyefuzu kozi
ya ualimu kwa lengo la kuimarisha na kuendeleza utaalamu na taaluma yake. Katika
kuimarisha na kuendeleza utaalamu na taaluma yake, mwalimu hupata fursa ya
kujifunza mambo mapya yanayojitokeza kulingana na wakati, kwa mfano, mabadiliko
ya mtaala wa shule, dhana na nadharia za ufundishaji na ujifunzaji, mabadiliko ya
jamii, sayansi na teknolojia. Aidha mafunzo kazini, humfanya mwalimu kwenda na
wakati. Tume ya Rais ya Elimu (uk. 232) inaelekeza mafunzo kazini huendeshwa kwa
mtindo wa kozi fupi au ndefu, semina, warsha na ziara za kielimu zenye malengo ya
kuinua viwango vya elimu, ujuzi na utaalamu wa walimu.
Sera ya Elimu (1995) katika ibara ya 5.5.10 inatamka ‘Mafunzo kazini na mafunzo
rejea yatakuwa ya lazima ili kuhakikisha ubora wa ualimu na utaalamu’. WEMU,
Februari 2006 katika utafiti wake kuhusu mfumo wa Elimu ya Ualimu katika Tanzania,
ilifanikiwa kuanzisha Mkakati wa Menejimenti na Maendeleo ya Walimu (MMEMWA)
ambapo moja ya lengo lake kuu ni kuhakikisha uwepo wa mafunzo kazini endelevu na
weledi kulingana na mahitaji ya utaalamu wa walimu. Malengo ya MMEMWA
yanajumuisha utafiti kuhusu mahitaji ya mafunzo kazini kwa ajili ya walimu, wakufunzi
na viongozi wa elimu kufikia mwaka 2009.
Kwa kupitia MMEMWA, Wizara imefanikiwa kuandaa na kutekeleza Mkakati wa Elimu
na Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Shule za Msingi (MEMK – WSM), 2009 – 2013.
Madhumuni ya mkakati huu ni kuimarisha utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu
baada ya mafunzo tarajali kwa lengo la kuhakikisha ubora wa ufundishaji na ujifunzaji
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
51
katika shule za msingi, pamoja na kukidhi mahitaji ya walimu kitaalamu na kitaaluma
(MWAKEM 2010).
Waraka Na.10 wa mwaka 2009 kuhusu mafunzo ya walimu kazini kwa walimu wa
shule za sekondari unaelezea umuhimu wa mafunzo kazini kama nyenzo muhimu ya
kumuongezea mwalimu maarifa, ujuzi na stadi za kumwezesha kufundisha kwa
umahiri. Aidha, waraka umeweka wazi mapungufu ya utaratibu wa mafunzo kazini
ambayo yamekuwa yanatolewa kwa baadhi ya maeneo na makundi ya walimu na
kutokuwa endelevu. Kutokana na hali hii, waraka unaelekeza mafunzo haya
kuendeshwa na Halmashauri husika kwa kuzingatia kuwa usimamizi na uendeshaji wa
shule za sekondari kwa sasa uko chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
2.11.3: Uwepo wa Walimu
Uwepo wa walimu wenye sifa ni moja ya kiashiria cha ubora wa elimu itolewayo.
Tume ya Rais ya Elimu (1982, uk. 230) inasema kwamba ubora wa walimu
hutegemea njia zinazotumika katika utayarishaji wao. Aidha, Tume inabaini kwamba
umuhimu wa kuwa na walimu bora haukuzingatiwa kikamilifu tangu nchi ilipojitawala.
Juhudi zilifanywa zaidi katika upanuzi wa elimu katika ngazi zote bila ya kuwa na
uwiano na ubora wa walimu wengi waliokuwa wanahitajika.
Utayarishaji na upungufu mkubwa wa walimu kwenye shule zilizoko vijijini na hasa
kwenye masomo ya ufundi, sayansi, hisabati, kiingereza na jiografia; kinyume na Sera
ya Elimu na Mafunzo, Ibara 5.4.5 inavyoelekeza: Wamiliki wa shule za sekondari
watahakikisha kwamba wanapata walimu wenye sifa zinazotakiwa, wanakuwa na
mazingira mazuri ya kufundishia, wanatoa mafunzo na wanawaendeleza walimu wao
kitaalamu. Sifa zinazostahili kama zilivyoanishwa na Sera ya Elimu na Mafunzo ni
walimu wenye Shahada na Stashahada kwenye shule za serikali na zisizo za serikali.
Walimu wa Stashahada wanapangiwa kufundisha Kidato cha 1 na 2 na walimu wa
Shahada wafundishe kuanzia Kidato cha 3 – 6.
Mwaka 2004, Serikali kupitia SEDP iliamua kuongeza usajili wa wanafunzi katika shule
za sekondari na wakati huo huo kuchukua juhudi za makusudi za kuinua ubora.
Kutokana na upungufu wa walimu uliokuwepo na ongezeko la uandikishaji wa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
52
wanafunzi, Serikali iliamua kuajiri walimu wa leseni. Taarifa ya utafiti uliofanywa na
Ngodu (2007) unaonesha kuwa idadi kubwa ya walimu hao wapatao 3,500
waliandaliwa mwaka 2006 na walisambazwa katika shule mbalimbali nchini. Utafiti
huo pia ulionesha kuwa wadau wengi walilalamikia ubora wa walimu hao kutokana na
muda mfupi wa mafunzo. Hata hivyo, kutokana na juhudi hizo Serikali iliweza
kufanikiwa kuongeza walimu 10,000 katika muda wa miaka minne kati ya mwaka
2004 – 2007.
Ili kuendelea kukabili ongezeko la shule za sekondari zikiwa na wanafunzi wengi bila
walimu wa kutosha, WEMU (2007) iliamua kuwa na mafunzo ya mfumo wa ‘two tier’
ambao uliruhusu wanachuo wa Stashahada kusoma mwaka mmoja chuoni na mwaka
wa pili kuwa shuleni.
Mmari (1979) anasema kuwa ubora wa ufundishaji wa shule za msingi unategemea
ubora wa mafunzo ya walimu waliyoyapata ambao pia hutegemea ubora wa
wakufunzi waliokuwa nao. Kigezo kimojawapo cha kujulisha ubora wao ni kujua sifa
ya mwalimu kitaaluma. Taarifa ya WEMU inaeleza kuwa kufikia mwaka 2010, kulikuwa
na jumla ya walimu 40,255 katika shule za sekondari za Serikali (30,256) na zisizo za
Serikali (10,269) BEST, 2010. Jedwali Na. 2.5 linaonesha sifa na idadi ya walimu wa
sekondari waliopo nchini.
Jedwali Na. 2.5 Idadi ya Walimu wa Sekondari kwa Sifa, Mwaka, 2010
Sifa za
Walimu
Shule za Sekondari za
Serikali
Shule za Sekondari
Zisizo za Serikali
Jumla
Me Ke JML Me Ke JML Me Ke JML
Shahada 3,418 2,360 5,778 3,248 884 4,132 6,666 3,244 9,910
Stashahada 11,494 6,678 18,172 3,171 828 3,999 14,665 7,506 22,171
Cheti 1 3 4 1 3 4 2 6 8
Nyingine 4,754 1,548 6,302 1,736 398 2,134 6,490 1,946 8,436
JUMLA
KUU
19,667 10,589 30,256 8,156 2113 10,269 27,823 12,702 40,255
Chanzo: Basic Education Statistics in Tanzania (BEST, 2010) uk. 115
Takwimu za kitaifa zilizokusanywa na OWM-TAMISEMI mwezi Machi 2011 zinaonesha bado
kuna upungufu mkubwa wa walimu katika masomo ya Mathematics na sayansi kama
inavyoonekana katika Jedwali Na. 2.6.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
53
Jedwali Na 2.6: Takwimu za Mahitaji, Uwepo na Upungufu wa Walimu
katika Shule Sekondari kwa Masomo ya Sayansi na Mathematics, 2011.
Masomo Biology Chemistry Mathematics Physics
Mahitaji 8,846 8,012 10,508 8,009
Waliopo 2,558 2,429 2,544 1,915
Upungufu 6,288 5,583 7,964 6,094
Asilimia ya Upungufu 71.1 69.7 75.8 76.1
Chanzo: Takwimu za Mahitaji ya walimu, OWM-TAMISEMI Machi, 2011
Mafunzo ya Ualimu hadi sasa yanaendeshwa katika vyuo 68 vilivyosajiliwa. Kati ya
hivyo, 34 ni vya serikali na 34 visivyo vya serikali. Vyuo 19 vya serikali viko katika
ngazi ya Stashahada. Changamoto iliyopo kulingana na maoni ya Ngodu (2009) ni
kwamba vyuo vya ualimu vilivyopo vina uwezo mdogo wa kudahili walimu tarajali wa
kutosheleza mahitaji ya nchi na wenye sifa stahili ya kuweza kuinua ubora wa elimu.
Takwimu zinaonesha kuwa ongezeko la wahitimu wa shahada katika vyuo vya ualimu
haliendani sambamba na ongezeko la uandikishwaji wa wanafunzi katika shule za
sekondari.
Kielelezo Na.2.1 Idadi ya walimu wa Stashahada waliohitimu na kufaulu
Mwaka 2005 – 2009
Chanzo: Basic Education Statistics in Tanzania (BEST, 2010) uk. 89
2.11.4: Upanuzi wa Mafunzo ya Walimu Tarajali Katika Ngazi ya Shahada
Ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu, mwaka 2007 Serikali ilichukua hatua
za kuanzishwa Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kinadahili idadi kubwa ya walimu
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
54
tarajali. Sanjari na uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Dodoma, iliamuliwa kuanzishwa
kozi ya ualimu katika vyuo vikuu vingine vya umma kama vile Chuo Kikuu cha Kilimo
cha Sokoine na Chuo Kikuu cha Mzumbe. Pia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilipanua
matawi ya vyuo vikuu viwili vya Elimu vya Mkwawa (MUCE) na Dar es Salaam
(DUCE). Taarifa ya utekelezaji WEMU inaeleza kuwa idadi ya walimu tarajali
watakaohitimu katika vyuo vikuu inakadiriwa kuwa 11,000 kwa mwaka (Hotuba ya
Bajeti, WEMU 2010/11).
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
55
SURA YA TATU: MWONGOZO WA UTAFITI
3.1. Utangulizi
Mwongozo wa utafiti unaonesha mchakato wa utafiti ulivyofanyika wakati wa
kukusanya data na taarifa za utafiti kutoka kwa wajibuji mbalimbali katika eneo la
utafiti. Sura hii inabainisha kuhusu eneo na walengwa wa utafiti, uchaguzi wa
sampuli, aina na matumizi ya zana za utafiti. Pia, imeainisha mchakato wa utafiti na
uchambuzi wa data na taarifa.
3.2. Mbinu ya Utafiti
Utafiti huu umetumia aina mbili za mbinu katika ukusanyaji na uchambuzi wa data
ambazo ni maelezo stahilifu ya wajibuji (qualitative) na takwimu (quantitative). Aidha,
dhana ya ufaulu wa Kidato cha 4 ilitafsiriwa kwa kuhusisha viashiria mbalimbali kama
vile mitaala, upimaji, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, usimamizi na uendeshaji,
ufuatiliaji na tathmini, uwepo wa walimu na mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji
kama inavyoonekana katika Kielelezo Na. 3.1. Viashiria hivyo vilitumika katika
kuandaa zana za utafiti
Kielelezo Na.3.1 Viashiria vya Kiwango cha Ufaulu www.JamiiForums.com
Rasimu 2
56
3.3. Eneo la Utafiti
Utafiti huu ulifanyika katika kanda zote 11 za elimu na kuhusisha mikoa ya Dar es
Salaam, Pwani, Singida, Ruvuma, Manyara, Shinyanga, Lindi, Mara, Kagera, Rukwa na
Tanga. Maeneo mengine yaliyohusika ni ofisi za Ukaguzi wa Shule Kanda pamoja na
ofisi ya elimu ya mkoa husika. Aidha, Taasisi ya Elimu (TET), Baraza la Mitihani la
Taifa (NECTA), Chuo Kikuu cha Dar na Chuo Kikuu Huria (OUT), TEN/MET na
TAMONGSCO zilihusika katika utafiti. Pia, utafiti ulihusisha vyuo vya ualimu, ofisi za
elimu za Halmashauri na ukaguzi wa shule wilaya, ofisi za Tume ya Utumishi (TSD) na
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya. Vilevile, ofisi za waheshimiwa Wabunge,
Madiwani, Mashirika yasiyo ya kiserikali katika Halmashauri na madhehebu ya dini
zilihusishwa.
3.4. Uchaguzi wa Sampuli
Jumla ya mikoa 11 ilihusishwa katika utafiti ili kupata uwakilishi kitaifa. Uchaguzi wa
Mikoa ulizingatia uwepo wa shule za sekondari zilizofanya vizuri na vibaya katika
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 zikijumuisha shule 88 za serikali na 44
zisizo za serikali. Jumla ya Halmashauri 22 zilihusishwa, mbili kutoka kila mkoa, moja
iliyofanya vizuri na nyingine iliyofanya vibaya katika Mtihani wa Taifa ya Kidato cha 4
mwaka 2010. Shule sita kutoka kila Halmashauri za utafiti zilichaguliwa na kuhusika
katika utafiti huu ambazo ni 4 za serikali na 2 zisizo za serikali.
Uchaguzi wa shule hizo kwa kila Halmashauri ulifanywa kwa kuzingatia kiwango cha
ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Shule za serikali
zilizochaguliwa zilijumuisha shule mbili zilizofanya vizuri na mbili zilizofanya vibaya
katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Vile vile, shule mbili zisizo za
serikali zilizochaguliwa moja iliyofanya vizuri na moja iliyofanya vibaya. Uchaguzi wa
shule ulifanywa kwa lengo la kupata uwakilishi wa shule zenye viwango tofauti vya
ufaulu. Jumla ya shule za sekondari zilizohusishwa katika utafiti ni 132, zikiwemo 12
kutoka katika kila Halmashauri.
Utafiti huu ulijumuisha wajibuji 3,037 kati ya 3,894 sawa na 80.0% kutoka kwenye
makundi 29. Walioshirikishwa katika utafiti huu walikuwa Wakaguzi wa shule wa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
57
Kanda 41, Wakaguzi wa shule Wilaya 22, Maafisaelimu Mikoa 11, Maafisaelimu wa
Halmashauri wa Msingi 21 na Sekondari 21, Maafisa wa TAMONGSCO 8, TEN/MET 6,
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) 23, na Tume ya Utumishi wa Umma wilaya (TSD)
22. Aidha, wengine ni pamoja na Wajumbe wa Bodi za Shule 82, Wakuu wa Shule za
Sekondari 132, Walimu wa kawaida 613, Walimu waliosahihisha mtihani wa Taifa
mwaka 2010 ni 162, Wakufunzi wa vyuo vya ualimu 28, wahadhiri wa vyuo vikuu 4,
wanachuo wa vyuo vya ualimu 44 na vyuo vikuu 4, Waheshimiwa Wabunge 17,
Waheshimiwa Madiwani 43, Wazazi/Walezi 95, Wanafunzi wa kidato cha 3 na 4 ni
1140, wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2010 ni 401 na viongozi wa madhehebu ya
dini 40. Utafiti huu pia ulilenga kupata taarifa kutoka kwa maafisa mitihani wa Baraza
la Mitihani la Tanzania (NECTA) 12 na wakuza mitaala wa Taasisi ya Elimu Tanzania
14 (Rejea Kiambatisho Na.3.5). Uchaguzi wa sampuli ulikuwa wa makusudi ambapo
wajibuji katika kila kundi ulizingatia uzoefu, nafasi zao kazini na jinsia katika taasisi
husika.
3.5. Zana za Utafiti
Taarifa na data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia Dodoso, Hojaji na Majadiliano ya
Pamoja. Pia, taarifa za data zilipatikana kwa kupitia Maandiko mbalimbali yakiwemo
ya kisera, Programu, Mipango, Nyaraka za kielimu na Ripoti za utafiti.
Dodoso za aina nne zilitumika kukusanya taarifa za utafiti toka kwa Wakaguzi wa
shule wa Kanda, Wakuu wa shule, Wakurugenzi wa TET na Wakuu wa Idara za
mitihani NECTA. Vilevile, Hojaji zilitumika kukusanya taarifa kutoka katika makundi
nane ya wahadhiri wa vyuo vikuu, wakufunzi wa vyuo vya ualimu, wanachuo wa vyuo
vikuu na vyuo vya ualimu, Maafisa Elimu mkoa, Maafisa Elimu wa Halmashauri Msingi
na Sekondari, Wakaguzi wa shule wa wilaya, Tume ya Utumishi wa Umma, Chama
cha Walimu Tanzania, Madhehebu ya Dini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali,
Waheshimiwa Wabunge, Madiwani, Wazazi/Walezi, Wajumbe wa Bodi za Shule na
wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Aidha, Mahojiano ya Pamoja yalitumika
kupata taarifa kutoka katika makundi sita ya wakuza mitaala, maafisa mitihani,
TAMONGSCO, TEN/MET, walimu wa masomo, walimu walioshiriki kusahihisha Mtihani
wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 na wanafunzi wa Kidato cha 3 na 4 mwaka
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
58
2011. Kiambatisho Na.3.5 kimeainisha aina ya zana ya utafiti, idadi ya wajibuji
waliohusika katika kila eneo la utafiti.
3.6. Utaratibu Uliotumika Kufanya Utafiti
Mchakato wa kufanya utafiti ulianza kwa kuteua Kikundi Kazi ambacho kiliandaa
hadidu za rejea na zana za utafiti zilizojaribiwa katika Manispaa ya Temeke. Kikundi
Kazi kiliwasilisha na kupokea maboresho ya hadidu za rajea na zana za utafiti kwenye
Menejimenti ya WEMU na OWM-TAMISEMI.
Jumla ya Watafiti 44 waliteuliwa kutoka WEMU na OWM-TAMISEMI kushiriki katika
semina elekezi ya maandalizi ya utafiti kabla ya kwenda kukusanya data katika
maeneo husika. Watafiti wanne walipangwa kukusanya data na taarifa katika kila
mkoa wakisaidiwa na mtafiti msaidizi mmoja kutoka kila Halmashauri iliyokuwa
kwenye sampuli. Mchakato wa kupata taarifa kutoka kwa wajibuji kutoka katika
maeneo mbalimbali ya utafiti unaelezwa kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo:-
3.6.1.Kukusanya Taarifa Kutoka Ngazi ya Taifa
Watafiti walikusanya data kutoka katika taasisi na asasi mbalimbali za kiserikali na
zisizo za kiserikali zilizochaguliwa ili kupata tarifa zenye taswira ya kitaifa kuhusu
kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Watafiti
walikusanya taarifa kwa kuwahoji wahadhiri wanne na wanachuo wanne wa vyuo
vikuu. Pia mahojiano ya pamoja yalifanyika kwa wakuza mitaala kumi, maafisa
mitihani wanane, maafisa nane wa TAMONGSCO na maafisa sita wa TEN/MET. Aidha,
Wakurugenzi wanne wa TET na Wakuu wa Idara wanne wa NECTA walijaza dodoso.
Taarifa za kitaifa pia zilikusanywa kwa kupitia maandiko mbalimbali.
3.6.2.Kukusanya Taarifa Kutoka katika Kanda, Mkoa na Halmashauri
Zana zilizotumika kupata data na taarifa kutoka katika Kanda za elimu, mikoani na
Halmashauri zilikuwa ni dodoso na hojaji. Dodoso ziligawiwa kwa Wakaguzi wa shule
wa Kanda wanne kwa kila Kanda ya elimu na Wakuu wa shule za sekondari 12 zilizopo
katika mkoa, ambapo ni shule sita kwa kila Halmashauri. Katika ngazi ya mkoa,
watafiti walitumia hojaji kupata taarifa kutoka kwa Afisaelimu Mkoa, wakufunzi wawili
na walimu tarajali wanne wa vyuo vya ualimu.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
59
Aidha, katika ngazi ya Wilaya na Halmashauri, waliohojiwa ni mkurugenzi wa
Halmashauri, Afisa Elimu Halmashauri (Sekondari), Afisa Elimu Halmashauri (Msingi),
Mkaguzi Mkuu wa Shule Wilaya, Afisa wa Tume ya Utumishi wa Umma (TSD), Afisa
wa CWT Wilaya, Viongozi wawili wa madhehebu ya dini, afisa wa shirika lisilo la
serikali, Mheshimiwa Mbunge na Diwani na wajumbe wawili wa Bodi za shule.
3.6.3.Kukusanya Taarifa Kutoka Shuleni na katika Jamii
Katika ngazi ya shule na jamii, watafiti walitumia hojaji kwa wahitimu wa watano wa
Kidato cha 4 kwa kila shule husika. Mkuu wa shule katika kila shule husika alijaza
dodoso na kutoa takwimu muhimu za shule. Aidha, mahojiano ya pamoja yalihusisha
walimu kutoka kila shule husika. Wanafunzi 10 wa kidato cha 3 na 4 mwaka 2011
walihusishwa kwenye mahojiano ya pamoja kwa kuzingatia ushiriki wa wanafunzi
wenye mahitaji maalumu na jinsi. Walimu walioshiriki kusahihisha Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4 mwaka 2010 walihusishwa katika mahojiano ya pamoja.
3.7. Uchambuzi wa Data
Data na taarifa mbalimbali kutoka shuleni, halmashauri na mkoa ziliunganishwa na
kupata taarifa ya kila mkoa husika. Hatua zilizofuatwa katika mchakato wa uchambuzi
na uandishi wa ripoti ya utafiti zilihusisha kuunganisha majibu ya kila swali kwa kila
zana kitaifa. Pia, majibu ya maswali ya kila zana kwa kila lengo mahsusi yaliainishwa,
yaliwekwa pamoja na kupangwa katika mtiririko wa uandishi kwa kila lengo mahsusi.
Aidha, taarifa zilichambuliwa, zikapangwa na kisha kutafsiriwa na ripoti ya utafiti
kuandikwa. Ripoti imeandikwa kwa kujadili masuala yaliyojitokeza kwa kila suala
muhimu na kuwasilishwa kwa kutumia idadi halisi na asilimia. Katika ripoti baadhi ya
taarifa na takwimu zimeoneshwa katika grafu, mihimili na majedwali.
3.8. Maadili ya Kufanya Utafiti
Utafiti huu ulizingatia taratibu na maadili katika hatua zote za ukusanyaji wa data,
uchambuzi na uandishi wa ripoti. Maadili yote ya utafiti katika ofisi na taasisi zikiwemo
shule za sekondari zilizofanyiwa utafiti yalizingatiwa, ikiwa ni pamoja na uhuru wa mtu
kushiriki katika utafiti, kutunza siri na mambo ya faragha yanayowahusu washiriki
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
60
(wajibuji). Utayari wa wajibuji katika kufanya utafiti ulipatikana kupitia viongozi na
wao wenyewe.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
61
SURA YA NNE: MATOKEO YA UTAFITI NA UCHAMBUZI WA DATA
4.1. Utangulizi
Sura hii inahusu uwasilishaji, uchambuzi na tafsiri ya data na taarifa zilizokusanywa
kutoka kwa wajibuji katika maeneo mbalimbali yaliyohusishwa katika utafiti.
Uwasilishaji wa data na taarifa umezingatia masuala yanayoendana na malengo
mahsusi na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti yamejadiliwa katika maeneo makuu
yafuatayo: Usimamizi na uendeshaji wa elimu; Utayarishaji na utekelezaji wa mitaala;
Mfumo na taratibu za Mitihani ya Taifa; Mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa
elimu; Mfumo wa utayarishaji na uwepo wa walimu; na Mazingira na vifaa vya
kufundishia na kujifunzia.
Utafiti ulilenga kuchambua kiwango cha ufaulu cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4
mwaka 2010. Mapitio ya maandiko na makala yameonesha kwamba kiwango cha
ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka kila mwaka tangu
mwaka 2007 (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na 2010 (50.4%) (BEST, 2010 &
NECTA, 2011). Kielelezo Na. 4.1 imeonesha mwenendo wa kushuka kwa ufaulu wa
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2006-2010.
Kielelezo Na. 4.1: Kiwango cha Ufaulu cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4
Mwaka 2006-2010
Chanzo: The National Examinations Council of Tanzania, Examinations Results
Statistics 2007-2010
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
62
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 yameonesha kuwa asilimia
49.6 ya watahiniwa wote hawakufaulu mtihani huo. Utafiti huu umeweza kubaini
sababu mbalimbali zinazochangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu ambapo wajibuji
walieleza kwa kutumia zana za Mahojiano ya pamoja, Hojaji na Dodoso. Kwa kupitia
zana za Hojaji na Dodoso, jumla ya wajibuji 1,092 walibainisha sababu za kushuka
kwa kiwango cha ufaulu cha Mtihani wa Taifa wa kidato cha 4 mwaka 2010 kama
ilivyooneshwa kwenye Kielelezo 4.2. Aidha, kwa kutumia mahojiano ya pamoja
wajibuji 1,945 walibainisha sababu mbalimbali za kushuka kwa kiwango cha ufaulu
ambapo usimamizi na uendeshaji wa elimu ulitajwa kwa kiwango kikubwa kuwa ni
chanzo cha tatizo.
Utafiti huu pia ulilenga kupata maoni mbalimbali juu ya kuinua kiwango cha ufaulu
cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Maoni yaliyopatikana kwa wajibuji
yameainishwa katika kila eneo kuu lililojadiliwa kwa kuzingatia malengo mahususi na
maswali ya utafiti.
Kielelezo Na. 4.2: Sababu za kushuka kwa Ufaulu cha Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4 Mwaka 2010
Chanzo: Data za Utafiti, 2011
Ufunguo:
A. Matatizo katika utekelezaji wa
mitaala
B. Upungufu wa walimu na
wafanyakazi wasio walimu
C. Matatizo ya usimamizi na
uendeshaji wa elimu
D. Mazingira yasiyoridhisha ya
ufundishaji na ujifunzaji
E. Mapungufu katika uendeshaji
wa mitihani ya kitaifa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
63
4.2. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu
Usimamizi na uendeshaji wa elimu ni lazima uwe na mfumo mzuri wa utendaji na
mawasiliano katika ngazi zote ili kufikia malengo ya utoaji wa elimu. Kwa kawaida
usimamizi na uendeshaji unazingatia miundo na mifumo iliyo rasmi katika ngazi zote
za elimu. Aidha, jukumu la usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini inahusisha
mifumo isiyo rasmi ikijumuisha wazazi/walezi, jamii na wadau mbalimbali wa elimu.
4.2.1.Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Ngazi Mbalimbali
Utafiti huu umebaini kuwa usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini unakabiliwa na
matatizo na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na watendaji wenye dhamana
ya kutekeleza jukumu hilo kutowajibika na kukosa umakini katika utendaji. Hali hii
inajionesha katika ngazi mbalimbali za usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini.
Ngazi hizo ni shule, kata, Halmashauri, mikoa na kitaifa. Kutokana na matokeo ya
utafiti, usimamizi na uendeshaji wa elimu umejadiliwa kwa kuhusishwa na masuala ya
kisiasa katika elimu, mmomonyoko wa maadili, mwamko duni wa jamii na ugharamiaji
wa elimu.
a) Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Shule na Kata
Uongozi wa shule unajumuisha wakuu wa shule, walimu, wajumbe wa bodi za shule
na serikali za vijiji/mtaa. Kila kundi lina wajibu wake katika kuhakikisha kuwa kanuni
na taratibu za uendeshaji shule zinazingatiwa ipasavyo. Aidha, ngazi hii ya usimamizi
inahusika na uhamasishaji wa wananchi katika kuchangia maendeleo ya shule na
elimu kwa ujumla (Kiongozi cha Mkuu wa shule: WEMU, 1997).
Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa yapo matatizo ya kiuwajibikaji kwa bodi za
Shule, wakuu wa shule na walimu wenyewe katika kutekeleza majukumu yao ya
msingi. Hali hii husababisha wanafunzi kutofundishwa kikamilifu kama ilivyopangwa
katika mihtasari na mihula ya shule. Aidha, utafiti umebaini kwamba kutokuwajibika
kwa bodi za shule kumezifanya baadhi ya shule kuwa na migogoro ya umiliki wa
maeneo ya shule kwa muda mrefu na hivyo kuingiza shule katika uhasama na jamii
inayoizunguka.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
64
Aidha, utafiti umeonesha kuwa bodi za shule hazisimamii uendeshaji wa shule
ipasavyo ikiwa ni pamoja na; nidhamu ya walimu na wanafunzi, mapato na matumizi
ya fedha ya shule na kuhamasisha upatikanaji wa raslimali katika shule. Madhara ya
bodi ya shule kutowajibika kunasababisha matumizi mabaya ya fedha inayotengwa
kwa ajili ya maendeleo ya elimu; wakuu wa shule na walimu kutotulia vituoni na
kutofuatiliwa kwa walimu katika uteketekelezaji wa majukumu yao ya ufundishaji na
ujifunzaji wa wanafunzi. Hoja ya walimu kutotekeleza majukumu yao pia ilidhihirishwa
na majibu ya mmoja wa wanafunzi katika majadiliano ya pamoja kuwa
“.....walimu hawafundishi, hivyo hatuna budi kwenda bondeni kula matango
mwitu“
Usemi huu unamaanisha wanafunzi kwenda kupata masomo ya ziada ya kulipia
(tuition) ambayo hawana uhakika na maudhui yake.
Utafiti umebaini kuwa Wakuu wa Shule wameshindwa kufuatilia ipasavyo mahudhurio
na utendaji kazi wa walimu walio chini yao, hali inayosababisha wanafunzi
kutofundishwa ipasavyo na hivyo kushindwa kufaulu mitihani ya taifa. Aidha, wakati
wa mahojiano ya pamoja na wanafunzi, mmoja wa wanafunzi alilalamika kwa
kusema:
“Baadhi ya walimu hututumikisha kazi za nje wakati wa vipindi darasani na
wengine hugawa kazi za kufanya darasani bila kutoa mwongozo wa namna ya
kuifanya kazi hiyo“.
Huu ni uthibitisho wa usimamizi usioridhisha wa utekelezaji wa mitaala ambapo
wanafunzi hutumia muda wa masomo kufanya kazi ambazo hazihusiani na ujifunzaji.
Pia mikakati ya wakuu wa shule ya kutumia walimu wa muda (part-time teachers)
wenye elimu ya kidato cha nne au sita bila taaluma ya ualimu kunaibua maswali
yanayohusishwa na kushuka kwa ufaulu. Vilevile, matokeo ya utafiti yamebainisha
kwamba baadhi ya walimu hufanya biashara wakati wa saa za kazi badala ya kuandaa
na kufundisha vipindi ipasavyo. Hali kadhalika, majukumu ya Waratibu Elimu Kata ya
kusimamia na kufuatilia ufundishaji na ujifunzaji hayatekelezwi ipasavyo.
Matokeo ya utafiti kuhusu usimamizi na uendeshaji wa elimu shuleni yanaonesha
kuwepo kwa usimamizi usioridhisha tofauti na ilivyoainishwa katika Sheria ya Elimu
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
65
Na. 25 ya Mwaka 1978 na rekebisho lake Na. 10 la mwaka 1995 na Kiongozi cha
Mkuu wa Shule (1997). Hali hii inaathiri uendeshaji wa shule, ufundishaji na ujifunzaji.
b) Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu Katika Mkoa na Halmashauri
Usimamizi na uendeshaji wa elimu katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri umeelezwa
kuwa umechangia katika kushuka kwa kiwango cha ufaulu. Utafiti umebaini kuwa
ufaulu duni unachangiwa na mgawanyo wa walimu usiozingatia mahitaji katika shule;
shule kutokaguliwa mara kwa mara na kutofanyiwa kazi kwa mapendekezo na ushauri
unaotolewa katika taarifa za ukaguzi wa shule.
Hali kadhalika, wingi wa wanafunzi darasani usio na uwiano na idadi ya walimu
wanaohitajika (1:40) na upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia husababisha ugumu wa ufundishaji na ujifunzaji hivyo baadhi ya shule
hulazimika kuendeshwa kwa mfumo wa awamu mbili (double session). Aidha, kuwepo
kwa mfumo wa awamu mbili hupunguza muda wa ufundishaji na ujifunzaji kwa vile
haiwezekani kuwa na vipindi 8 kwa siku kama ilivyoelekezwa katika Kiongozi cha
Mkuu wa Shule. Katika mfumo huo, wanafunzi hufundishwa vipindi 7 kwa siku na
hivyo kupoteza dakika 40 za kujifunza kwa kila siku za masomo sawa na vipindi 194
kwa mwaka.
Wanafunzi walieleza kwamba kutochanganywa kwa wanafunzi kutoka kata tofauti
katika shule moja kumesababisha kutokuwa na ushindani wa kitaaluma miongoni
mwao. Hali hii inasababisha wanafunzi kutobaini mabadiliko ya kimazingira kati ya
shule za msingi na sekondari hivyo kuathiri ujifunzaji wao.
c) Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Wizara
Baada ya zoezi la ugatuaji 2008, WEMU imebaki na jukumu la kuandaa sera, mitaala,
uthibiti wa viwango vya ubora wa elimu, ufuatiliaji na tathmini ya mipango ya elimu
ambapo jukumu la usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari umehamishiwa
OWM-TAMISEMI (WEMU, Hotuba ya Bajeti, 2010).
Wadau wa elimu waliohusishwa katika utafiti walibainisha sababu za kushuka kwa
ufaulu zinazotokana na usimamizi na uendeshaji wa elimu usioroidhisha; kusajiliwa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
66
kwa shule zisizotimiza vigezo vinavyotakiwa; kuajiriwa kwa walimu wasio na sifa;
kutoshughulikiwa kwa matatizo ya walimu. Hali inaathiri utoaji wa elimu bora nchini.
Utafiti umeonesha pia kuna tatizo katika taratibu za uteuzi wa viongozi wa elimu
katika ngazi mbalimbali wakiwemo Maafisaelimu na Wakuu wa Shule ambapo baadhi
yao huteuliwa bila kuwa na sifa za kiuongozi na hivyo kuwa chanzo cha migogoro
shuleni kwa kushindwa kudhibiti nidhamu ya wanafunzi na walimu.
Usimamizi na uendeshaji wa elimu katika ngazi ya Wizara umeonekana kuwa na
mapungufu kwa kuajiri walimu wa leseni na kutowaendeleza kitaalamu. Hali hii ni
kinyume na Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 seksheni 49 inayosisitiza leseni
kutolewa kwa muda maalum. Aidha, Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inaeleza kuwa
walimu wa sekondari wawe wenye stashahada na shahada. Pia, imebainishwa kuwa
usajili wa shule na uteuzi wa viongozi wa elimu wakiwemo wakuu wa shule hauzingatii
vigezo vinavyotakiwa na hivyo kuathiri ubora wa elimu nchini.
d) Michango ya Wadau wa Elimu katika Usimamizi na Uendeshaji wa
Elimu ya Sekondari
Serikali imekuwa ikihamasisha watu binafsi, mashirika ya kidini, taasisi zisizo za
kiserikali na wadau wengine kutoa michango mbalimbali katika sekta ya elimu.
Mojawapo ya michango hiyo ni kuanzisha na kumiliki taasisi za utoaji wa elimu katika
ngazi zote. Utafiti umebaini kuwa mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali zikiwemo
taasisi za kidini na watu binafsi wameanzisha na kumiliki shule za msingi, sekondari,
vyuo na vyuo vikuu hapa nchini.
Aidha, matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa kuna ushirikiano mkubwa kati ya shule
na jamii katika kuinua kiwango cha taaluma shuleni. Wazazi/walezi hufuatilia kwa
karibu taarifa ya maendeleo ya taaluma ya watoto wao na kuhudhuria vikao na vipindi
maalum ili kuzungumza na wanafunzi juu ya mahudhurio na nidhamu. Pia
wazazi/walezi wanachangia gharama za uendeshaji wa elimu kwa kulipa ada na
michango muhimu ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama za chakula. Vilevile, shule
hutuma taarifa za maendeleo ya watoto kwa wazazi/walezi na vikao vya bodi za shule
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
67
hushirikisha wazazi katika kusimamia taaluma na maadili shuleni. Michango ya
mashirika/taasisi zisizo za kiserikali na jamii imeoneshwa katika Kielelezo 4.3
Kielelezo Na. 4.3 Michango ya Wadau wa Elimu katika Asilimia
Chanzo: Data za Utafiti, 2011
Kielelezo Na 4.3 kinaonesha kuwa taasisi/mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii
wanachangia zaidi katika eneo la taaluma shuleni kwa asilimia 21.6, maadili shuleni
asilimia 18.3% na ushauri kuhusu bajeti ya elimu asilimia 16.1. Katika eneo la
taaluma, utafiti umebaini kuwa mchango wa wadau hao umejikita katika kuboresha
mazingira ya kujifunzia na kufundishia kama vile kununua vitabu, kuhamasisha
mafunzo kuhusu mitaala, elimu ya UKIMWI, mafunzo elekezi kuhusu sheria za kazi,
michango ya tafiti na ya kuendeleza taaluma shuleni. Pia, katika suala la maadili,
taasisi za kidini zinatoa mafundisho ya dini kwa walimu, wanafunzi na jamii kwa lengo
la kurekebisha mienendo isiyokubali katika jamii.
Vilevile, utafiti umeonesha taasisi/mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii wanachangia
kwa kiasi kidogo katika maeneo ya uboreshaji wa miundombinu na huduma muhimu
shuleni kwa asilimia 6.5%, usimamizi wa utekelezaji wa miongozo mbalimbali ya
serikali asilimia 4.5, usimamizi wa haki na maslahi ya walimu asilimia 3.1 na
kuhakikisha ikama ya walimu shuleni asilimia 2.8. Katika kuboresha miundombinu
ilifafanuliwa kuwa wadau hao hujenga na kuboresha majengo kama vile hosteli,
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
68
mabweni, maktaba, madarasa, ofisi za walimu, nyumba za walimu, umeme na samani
mbalimbali.
Hivyo, utafiti umebaini kuwa wadau wa elimu wana mchango mkubwa katika
usimamizi na uendeshaji wa elimu ya sekondari. Wadau wa elimu wamekuwa
wakifanya kazi kwa karibu sana na serikali kwa kusimamia na kulinda maadili,
kusimamia haki na maslahi ya walimu, taaluma na utekelezaji wa miongozo shuleni,
kuboresha miundombinu na huduma, kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi shuleni,
kuimarisha mahusiano baina ya shule na jamii, kuhakiki ikama ya walimu na kutoa
ushauri juu ya bajeti ya elimu.
Pamoja na ushirikiano huo, utafiti umebaini kuwa kuna changamoto zinazokwamisha
jitihada za wadau wa elimu ya sekondari nchini katika kufikia malengo ya utoaji wa
elimu bora. Changamoto hizo ni pamoja na Serikali kutoza kodi ya ongezeko la
thamani (Value Added Tax-VAT) kwa vyombo vya usafiri na vifaa vingine vya
uendeshaji wa shule na vyuo. Aidha, ilielezwa Serikali haiyafanyii kazi ipasavyo
mapendekezo ya tafiti yanayotolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali.
4.2.2.Mmomonyoko wa Maadili Katika Jamii
Mmomonyoko wa maadili katika jamii huathiri mwenendo wa nidhamu ya walimu na
wanafunzi shuleni. Utafiti umebaini kuwa mmomonyoko wa maadili kama vile
matumizi ya lugha mbaya kwa walimu, wanafunzi, wazazi/walezi na jamii; matumizi
mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kutozingatia
mafundisho ya dini yanaathiri maendeleo ya taaluma shuleni. Aidha, matumizi ya
dawa za kulevya, utoro, kujiingiza katika masuala ya mapenzi ni kati ya masuala
yaliyobainishwa kuchangia kushuka kwa maadili. Walimu walilalamikiwa kwa kutofuata
maadili ya kazi zao, mfano mmoja wa wanafunzi katika mahojiano ya pamoja alisema:
“…..walimu wanadiriki hata kuvuta sigara mbele ya wanafunzi……”
Uamuzi wa kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kwa makosa ya kawaida
umelalamikiwa pia kuwa umechangia kushuka kwa maadili kwa vile walimu hawana la
kufanya juu ya watoto wanaofanya makosa. Hali hii inamjengea mwanafunzi kiburi
kwa walimu.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
69
Matokeo zaidi yameonesha kuwa miongoni mwa watendaji katika sekta ya elimu
wameweka mbele maslahi yao binafsi kwa kukosa uadilifu na hivyo kuathiri utekelezaji
wa malengo yaliyopangwa. Aidha, baadhi ya wazazi wamekuwa wakijihusisha na
ununuzi wa mitihani kwa ajili ya kuwapa watoto wao na hivyo kuwajengea hali ya
kutojisomea kwa kutegemea mitihani bandia (fake). Kulingana na matokeo ya utafiti
ni dhahiri kwamba kuna mmomonyoko wa maadili kuanzia ngazi za familia, shule na
jamii kwa ujumla kinyume na sheria na kanuni za shule za sekondari kama
ilivyoainishwa kwenye Kiongozi cha Mkuu wa Shule (1997) ukurasa 42-43 na
mafundisho ya dini.
4.2.3.Mwamko Duni wa Jamii Katika Elimu
Katika utafiti huu, mwamko duni wa jamii ni mojawapo ya sababu iliyochangia
kushuka kwa kiwango cha ufaulu. Aidha, jamii kutoshiriki kikamilifu katika harakati za
maendeleo shuleni; kutokutoa karo na michango halali ya kuboresha taaluma; pamoja
na imani potofu ya kuona kuwa mtoto wa kike hatakiwi kusoma bali kuozwa ni mifano
ya mwamko duni wa jamii katika elimu. Vilevile utafiti umebaini kuwa, wazazi wengi
huwatumikisha watoto kazi za nyumbani na kuwahusisha katika kazi za kujiongezea
kipato cha familia badala ya kwenda shule. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa jamii
haijaelewa ipasavyo umuhimu wa elimu kwa watoto hasa wa kike. Pamoja na juhudi
za serikali kuhamasisha jamii na kutoa fursa na usawa wa elimu kwa watoto kama
ilivyoainishwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, bado jamii inadhani
kuwa jukumu la kuelimisha umma ni la Serikali pekee. Hivyo, juhudi za pamoja katika
utoaji wa elimu bado ni changamoto.
4.2.4.Siasa Kuingilia Masuala ya Kitaalam ya Kielimu
Utafiti ulibainisha kuwa maamuzi ya baadhi ya masuala ya kiataalam ya kielimu
hufanyika kisiasa na kusababisha kukiukwa kwa Mipango ya Elimu, kanuni na taratibu
za uendeshaji wa elimu kama vile matumizi ya fedha za shule. Wahojiwa walibainisha
kuwa uanzishaji wa shule nyingi za wananchi kwa mwaka 2006 usioendana na uwepo
wa walimu wenye sifa, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, huduma za jamii na baadhi
ya shule hizo kujengwa maeneo yaliyo mbali na makazi ya watu ni mojawapo ya
maamuzi yaliyotawaliwa zaidi na maamuzi ya kisiasa.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
70
Aidha, kumekuwepo na shinikizo la kisiasa kuhusu kusajiliwa kwa baadhi ya shule
ambazo hazikidhi viwango vilivyowekwa na serikali. Sababu nyingine zilizotolewa na
wajibuji waliohojiwa ni pamoja na wanasiasa kuwatumia wanafunzi na walimu kwa
mambo ya kisiasa kama vile wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Aidha, imebainishwa kuwa baadhi ya Waheshimiwa Madiwani huwakataa na
kuwaondoa baadhi ya wakuu wa shule na walimu katika shule zilizo katika maeneo
yao bila sababu za msingi. Kutofanyika kwa utafiti wa kina wakati wa maboresho ya
mitaala na kubadilisha muundo wa masomo ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa
kufanywa kisiasa.
Matokeo haya yanaonesha kuwa yapo mapungufu ya kiuendeshaji katika elimu
yanayotokana na mgongano wa maamuzi kati ya wataalamu na wanasiasa.
Migongano hiyo imesababisha ukiukaji wa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa
elimu nchini kama zilivyoainishwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sheria ya
Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na Kiongozi cha Mkuu wa Shule (1997).
4.2.5.Ufinyu wa Bajeti ya Elimu
Bajeti ndogo inayotengwa na serikali kwa ajili ya elimu nchini na matumizi ya fedha
yasiyoendana na thamani ya kazi yanasababisha kutokamilika kwa mipango ya kuinua
taaluma shuleni. Ilibainishwa kwamba ufinyu wa ruzuku za uendeshaji (capitation
grant) na maendeleo (development grant) ya shule umesababisha matatizo katika
uendeshaji wa shule. Bajeti ya Elimu ya sekondari kama inavyoonesha katika Kielelezo
Na. 4.4 inapungua tofauti na ongezeko la wanafunzi toka 524,325 (2005) mpaka
1,638,699 (2010) ambalo linasababisha ongezeko la mahitaji ya uendeshaji wa elimu
ya sekondari. Hali hiyo imeathiri upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia
na uboreshaji wa miundombinu kama vile maabara, maji, umeme ambavyo
vinachangia katika utoaji wa elimu bora. Ufinyu wa bajeti na matumizi yasiyozingatia
thamani ya fedha inathibitisha usimamizi na uendeshaji wa elimu ya sekondari
usioridhisha.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
71
Kielelezo 4.4: Asilimia ya Mgao wa Bajeti ya Elimu ya Sekondari katika
Sekta ya Elimu Mwaka wa Fedha 2004/05-2010/11
Chanzo: BEST, 2010
4.2.6.Maoni Kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu
a) Kuimarisha Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu
Ili kuleta ufanisi wa kitaaluma, ni muhimu kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa
elimu katika ngazi mbalimbali. Hii itawafanya walimu na viongozi wa elimu wawajibike
na kusimamia shughuli za utoaji wa elimu ipasavyo. Maoni mbalimbali yalitolewa na
Wakaguzi wa shule, Walimu, Wakuu wa shule, Wazazi/walezi, Wanafunzi, Wanasiasa
na wadau wengineo walioshirikishwa katika utafiti.
Katika kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu ilipendekezwa kwamba uteuzi wa
viongozi wa elimu wakiwemo Maafisaelimu na Wakuu wa Shule uzingatie sifa stahiki.
Aidha, ilishauriwa kuwa wakuu wa shule wawepo katika vituo vyao vya kazi na
wawajibike ipasavyo na wapewe mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa shule ili
kuleta ufanisi katika kazi. Pia, utaratibu wa kuwasimamisha masomo wanafunzi
wasiolipa ada au kushindwa kulipa michango mbalimbali uachwe, na michango
itolewe kwa kuzingatia waraka unaoongoza utoaji wa michango kwa shule za serikali.
Vilevile, Waratibu wa Elimu Kata wapewe mafunzo ya kusimamia elimu ya sekondari
ipasavyo na uteuzi wao lazima uzingatie taaluma na ujuzi.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
72
Aidha, masomo ya ziada yatolewe kwa wasio na uwezo darasani. Kuhusu usafiri wa
wanafunzi ilibainishwa kwamba mpango wa kuwa na vyombo vya usafiri kwa kila
shule ubuniwe. Vilevile, michezo shuleni iimarishwe ili kuwafanya wanafunzi wawe na
afya njema na wakue kiakili. Pia ilishauriwa kuwa shule ziwe na mpango wa motisha
kwa walimu, kama vile kuwaendeleza kitaaluma hususan walimu wa leseni ili kuleta
ufanisi na kujenga ari na morali ya kazi. Walimu walipendekeza kuwa huduma za
ushauri nasaha kwa wanafunzi ziimarishwe shuleni ili kuwaepusha na majanga
yakiwemo UKIMWI, ulevi na mimba. Maoni yaliyotolewa na wadau yanaonesha kuwa
kuna udhaifu katika uteuzi na uwajibikaji wa uongozi katika ngazi ya shule.
Ilipendekezwa kwamba uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha 1 katika shule za
wananchi uzingatie kuchanganya wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali ndani
na nje ya kata husika ili kuleta changamoto za ushindani na kuongeza chachu ya
maendeleo kitaaluma kwa ajili ya mabadiliko chanya ya kimtazamo. Ilishauriwa pia,
uandikishaji wa wanafunzi kuingia kidato cha kwanza uzingatie uwiano wa darasa 1:
wanafunzi 45. Vilevile, ilishauriwa kuwa, fursa ya chaguo la pili iondolewe kwa sababu
inahusisha wanafunzi wenye ufaulu mdogo wakiwemo wasiojua kusoma na kuandika.
Maoni hayo yanaonesha kuwa utaratibu wa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na Kidato
cha 1 una mapungufu ambayo yanachangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa
Mitihani ya Taifa.
Maoni yalitolewa kuwa, wajumbe wa bodi waelimishwe kuhusu majukumu yao ya kazi
na Afisaelimu Mkoa ahudhurie vikao vya bodi ili kuwa na maamuzi yanayofanana. Vile
vile bodi ya shule ichukue hatua za kinidhamu kwa walimu wanaobainika kwenda
kinyume na taratibu za shule kwa mfano, kuwachangisha fedha wanafunzi kwa ajili ya
masomo ya ziada. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa Bodi za shule hazitekelezi
majukumu yao ipasavyo.
Mapendekezo ya kisera pia yalitolewa kuwa mfumo wa elimu uangaliwe upya ili uweze
kumwandaa mhitimu kuwa mbunifu na mwenye kujitegemea. Hii ni pamoja na
kuimarisha masomo ya ufundi ili wahitimu waweze kujiajiri. Pia imeshauriwa kuwa
mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa yarudishwe kwa ajili ya kujenga uzalendo na utaifa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
73
kwa wahitimu. Vilevile, ilipendekezwa kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
idhibiti ada katika shule binafsi na kusimamia matumizi ya mtaala mmoja ili kuzuia
matabaka yanayojengeka. Aidha, tafiti za nje pekee zisitumike kubadili mfumo wa
elimu nchini. Ilishauriwa kuwa Idara ya Utumishi ya Walimu iimarishwe kwa ajili ya
kutoa huduma na maslahi bora ya walimu. Vilevile imebainika kuwa Masomo ya Elimu
ya msingi yapunguzwe na mkazo uwekwe kwenye KKK katika madarasa ya kwanza
hadi la tatu. Aidha, Somo la English Language liimarishwe katika ngazi ya Elimu ya
msingi na sekondari. Pia ilipendekezwa kuwa lugha ya kufundishia na kujifunzia iwe
moja katika ngazi ya msingi na sekondari.
Ilishauriwa viongozi wa elimu wafanye ziara za mara kwa mara na za kushtukiza
shuleni ili kujionea uendeshaji wa elimu unavyoendelea, Serikali idhibiti ufundishaji
holela wa masomo ya ‘tuition’ . Aidha, kuwepo na mfumo wa wazi wa tathmini ya
utendaji kazi (OPRAS). Kuhusu wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito ilipendekezwa
kuwe na mfumo unaowaruhusu kuendelea na masomo na kanuni za utoaji wa adhabu
zinazoendana na makosa ziangaliwe upya. Pia ilipendekezwa kuwa viboko virudishwe
shuleni kwani kukataza viboko kumeshusha nidhamu ya wanafunzi. Utafiti umebaini
kwamba maeneo mbalimbali ya kisera kuhusu mfumo wa elimu, maslahi ya walimu
na uongozi na uendeshaji wa elimu zina mapungufu ya kiutendaji.
b) Kuimarisha Mwamko wa Jamii Katika Elimu
Katika kuimarisha mwamko wa elimu kwa jamii wadau wote wahamasishwe ili
waweze kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya elimu nchini. Aidha, imependekezwa
kuwa jamii ihamasishwe kubaini vipaji vya watoto tangu wakiwa wadogo na
wahimizwe kusoma kwa bidii. Wazazi wahamasishwe kuchangia elimu ikiwa ni pamoja
na kulipa ada kwa wakati na jukumu lao kwa watoto wao hususani kuwasomesha
watoto wa kike na wale wenye mahitaji maalumu.
Maoni yaliyotolewa yanadhihirisha kuwepo kwa mwamko duni wa jamii katika
kuchangia maendeleo ya elimu. Aidha, suala la uhamasishaji wa jamii kuchangia
elimu linahitaji utayari na ushirikiano wa wanasiasa.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
74
c) Kukabiliana na Mmomyoko wa Maadili ya Walimu na Wanafunzi Shuleni
Kuhusu mmomonyoko wa maadili wajibuji walishauri kwamba, walimu wazingatie
kanuni, taratibu na maadili ya kazi yao. Pia wazazi, walimu, mashirika ya dini na
mashirika yasiyo ya kiserikali wahimize nidhamu ya wanafunzi kwa maendeleo ya
taaluma. Aidha, wanafunzi wanasihiwe kuhusu madhara ya kutumia madawa ya
kulevya, kuvuta sigara, na kwenda katika sehemu za starehe. Zaidi ya hayo walitoa
maoni kwamba hatua kali zichukuliwe kwa walimu na jamii wanaojihusisha kimapenzi
na wanafunzi, pia kianzishwe kitengo cha ushauri nasaha na unasihi ili kuwasaidia
wanafunzi kuwa na maadili mema. Walishauri kuwa jamii iwaheshimu walimu na
kuthamini kazi yao. Vilevile, ilipendekezwa kwamba adhabu ya viboko irejeshwe
shuleni. Maoni haya yanaonesha kuwa suala la maadili halishughulikiwi kikamilifu
katika uendeshaji wa elimu nchini. Madhara ya wadau wa elimu kutotilia mkazo suala
la maadili katika usimamizi na uendeshaji wa elimu kunasababisha kuwepo kwa jamii
na viongozi wasio na uzalendo, uadilifu na uwajibikaji katika kuleta maendeleo nchini.
d) Kuboresha Bajeti ya Elimu
Maoni yalitolewa kuwa ufinyu wa Bajeti ya Elimu na matumizi yasiyoendana na
thamani ya fedha inayotolewa husababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa
Mtihani wa Taifa. Vilevile, ilielezwa kuwa ruzuku ya maendeleo na uendeshaji wa
shule za sekondari ni ndogo hivyo ilishauriwa kuwa bajeti iongezwe ili kuwepo na
vitendea kazi vya kutosha na mishahara mizuri ya walimu. Aidha, fedha ya ruzuku ya
uendeshaji itolewe yote na ipatikane kwa wakati kama miongozo inavyoelekeza (SEDP
II, 2010). Walishauri kuwa, maeneo yenye changamoto nyingi za kielimu yapewe
kipaumbele katika mgao wa rasilimali watu na fedha, pia imesisitizwa kuwepo
usimamizi wa matumizi ya fedha yanayoendana na thamani ya kazi. Upatikanaji,
mgawanyo kulingana na mahitaji na matumizi ya fedha za ruzuku bado ni
changamoto katika uendeshaji wa elimu nchini.
e) Kuitumia Siasa katika Maendeleo ya Elimu
Maoni yaliyotolewa yameonesha kuwa jamii inathamini mchango wa wanasiasa katika
kuchochea maendeleo ya elimu. Ilishauriwa kuwa, Walimu na wanafunzi watumie
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
75
muda mwingi katika kufundisha na kujifunza badala ya kujishughulisha na masuala ya
kisiasa. Pia walisema, mambo muhimu ya kitaalamu kuhusu elimu yatokane na
ushauri wa wataalamu. Hivyo, maamuzi yote ya mipango na utekelezaji wa elimu
yatokane na tafiti na ushauri wa kitaalam.
4.2.7.Mapendekezo kwa Walioshindwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha
4 Mwaka 2010
Mapendekezo juu ya nini kifanyike kwa wanafunzi walioshindwa Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4 mwaka 2010 yalitolewa na wadau wa elimu 2,636 kati ya 3,037
waliohusishwa katika utafiti huu. Mapendekezo yaliyotolewa yamelenga katika
maeneo manne yaani kurudia mtihani kama watahiniwa wa kujitegemea, kukariri
darasa na kufanya mtihani kama watahiniwa wa shule, mtihani usahihishwe upya na
wahitimu kupatiwa mafunzo stadi kama inavyooneshwa katika Kielelezo Na. 4.5
Kielelezo Na. 4.5 Mapendekezo kwa Walioshindwa Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4 Mwaka 2010
Chanzo: Data za Utafiti, 2011
a) Kuwapa Mafunzo Stadi
Wadau waliohojiwa walipendekeza kuwa wahitimu wote walioshindwa wapatiwe
mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vinavyotambuliwa na VETA ikiwemo VETA
yenyewe. Mafunzo hayo yalenge stadi za maisha na ujasiriamali kama vile ufugaji,
uvuvi, useremala na stadi zingine za maisha ikiwemo elimu ya UKIMWI. Pia
ilipendekezwa kuwa serikali iimarishe vyuo hivyo na kugharamia mafunzo hayo.
b) Kupewa Fursa ya kurudia mtihani kama watahiniwa wa kujitegemea
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
76
Walipendekeza kwamba, wahitimu warudie mitihani kama watahiniwa wa kujitegemea
kulingana na utaratibu uliopo. Ilishauriwa kwamba miundombinu iboreshwe ili
watahiniwa waliopo katika mazingira magumu waweze kupata fursa ya kufanya
mtihani.
c) Kukariri Darasa na Kufanya Mtihani wa Taifa Kama Watahiniwa wa
Shule
Wadau walipendekeza kuwa watahiniwa waruhusiwe kukariri kuanzia kidato cha tatu
kama wanafunzi wa kawaida shuleni ili waweze kupata ujuzi wa kutosha kuweza
kufanya mitihani. Pia ilipendekezwa kuwa watakaokariri wasome masomo ya jioni
badala ya muda wa kawaida wa shule.
Suala la kukariri darasa katika mfumo wowote wa elimu linaonesha kutokuwepo kwa
ufanisi wa ndani (internal efficiency) katika ngazi husika ya elimu. Ili kuepuka kufeli
kwa watahiniwa wengi kama ilivyojitokeza katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha 4
mwaka 2010, kuna haja ya kuimarisha ufanisi wa ndani katika ngazi zote za elimu.
d) Kusahihisha Mitihani Upya
Mapendekezo yalitolewa kuwa zoezi la usahihishaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha
4 mwaka 2010 ilirudiwe kwa kuwa usahihishaji haukuwa makini. Aidha ilishauri
kwamba, uchunguzi wa usahihishaji wa mitihani hiyo ufanyike kubaini mapungufu
yaliyojitokeza.
4.3. Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala
4.3.1. Utayarishaji wa Mitaala
Mtaala ni orodha ya maarifa ambayo mwanafunzi anatarajiwa kuyapata na namna
yanavyopangiliwa ikiwa ni pamoja na fursa za kujifunza maarifa hayo (HakiElimu,
2011). Utayarishaji wa mtaala ni mchakato unaotakiwa kuwahusisha wadau wote wa
elimu. Vilevile, mabadiliko au maboresho ya mtaala yanatakiwa kuzingatia mahitaji ya
jamii husika. Aidha, Mihtasari ya masomo ni nyenzo muhimu ya mtaala katika
kupanga na kukamilisha mchakato wa kufundishia na kujifunzia na humsaidia
mwalimu kufahamu mada mbalimbali zinazotakiwa kufundishwa katika darasa na
somo husika.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
77
Jukumu la kuandaa mitaala ni la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na hufanywa
kulingana na mzunguko kwa kila ngazi ya elimu ambapo elimu ya msingi ni miaka
saba na sekondari ni miaka sita. TET huandaa, huboresha na kuchapisha mitaala na
mihtasari ya masomo ya elimu ya sekondari na vyuo vya ualimu na huhakikisha
kwamba inakuwepo shuleni. Utafiti umebaini kutokuwepo kwa ushirikishwaji toshelevu
wa wadau katika maandalizi ya mtaala hususan katika hatua za utayarishaji na
ujaribishaji wa mitaala (piloting). Kutojaribishwa kwa mtaala unaotumika
kumesababisha kutobainika kwa mapungufu yaliyopo kwa wakati. Hivyo mtaala
unaotumika una changamoto za utekelezaji unaothiri mchakato wa ufundishaji na
ujifunzaji. Hii inathibitisha kutozingatia hatua za utayarishaji wa mtaala kama
ilivyoinishwa katika Mwongozo wa Ukuzaji Mitaala-NCDF (TIE, 2003).
4.3.2. Uwepo wa Mihtasari Shuleni na Vyuoni
Mahitaji muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ni uwepo na upatikanaji
wa mihtasari ya masomo shuleni kwa ajili ya matumizi ya walimu na wanafunzi.
Utafiti umebaini kuwa jukumu la usambazaji wa mihtasari shuleni baada ya
kuchapishwa siyo la TET. Wakuza mitaala waliohojiwa walieleza kuwa TET haihusiki
na jukumu la usambazaji wa mihtasari ya masomo katika shule za sekondari nchini.
Aidha, waliongeza kuwa hakuna mwongozo unaobainisha msambazaji wa mihtasari
katika ngazi ya shule. Vilevile walithibitisha kuwa, mihtasari huwa inauzwa na TET
kwa wanaoihitaji na kwa shule pia.
Kielelezo Na.4.6: Upungufu wa Mihtasari
Chanzo: Data za Utafiti, 2011
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
78
Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa idadi ya mihtasari ya masomo iliyoboreshwa
mwaka 2005 na 2007 iliyopo katika shule za utafiti haitoshelezi mahitaji kama
inayooneshwa katika Kielelezo Na.4.6. Utafiti umebaini uwepo wa upungufu wa
mihtasari, ambapo masomo ya Mathematics na Geography yameongoza kwa kuwa na
upungufu kwa zaidi ya asilimia 50.
Aidha, katika vyuo vya ualimu, utafiti ulibaini kuwa asilimia 61.3 (62) ya waliohojiwa
juu ya uwepo na matumizi ya mihtasari iliyoboreshwa katika vyuo walisema, mihtasari
iliyoboreshwa ipo vyuoni lakini ni kwa ajili ya wakufunzi tu na asilimia 38.7 walisema
mihtasari haipo. Hata hivyo WEMU imeweka mihtasari ya mafunzo ya ualimu katika
tovuti (website). Hivyo utafiti umebaini kuwa, kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa
mihtasari na miongozo ya mitaala (curriculum documents) kutoka kwa mtayarishaji
mpaka kwa mtumiaji katika shule za sekondari.
4.3.3. Utekelezaji wa Mtaala
Utekelezaji wa mtaala ni jukumu la mwalimu shuleni. Matokeo ya utafiti yameonesha
kuwa wajibuji 152 kati ya 1,092 sawa na asilimia 14 wamebainisha kuwepo kwa
mapungufu katika utekelezaji wa mtaala na kwamba walimu wengi hawana maarifa
na stadi za kufundisha mtaala wa sekondari ulioboreshwa. Aidha, utafiti umebaini
kuwa dhana ya mtaala unaozingatia ujuzi haijaeleweka vizuri kwa wadau mbalimbali
wakiwemo baadhi ya wakuza mitaala na maafisa mitihani.
Mapungufu yaliyoainishwa na wajibuji ambayo yanakwamisha utekelezaji wa mtaala
kwa ufanisi ni pamoja na maboresho ya mitaala kufanywa bila kuwa na maandalizi ya
kutosha; kufanyika kwa kiwango kidogo cha mafunzo kabilishi; upungufu wa vitabu;
ukosefu wa fedha kwa ajili ya uchapaji na usambazaji wa vitabu; ubovu wa
miundombinu na uelewa mdogo wa lugha ya Kiingereza kwa walimu na wanafunzi.
Mapungufu hayo yamesababishwa na kutokuwepo kwa maandalizi ya kutosha kama
ilivyofafanuliwa katika mwongozo wa ukuzaji mitaala (NCDF TIE, 2003). Hali
inayosababisha tofauti ya uelewa baina ya walimu kuhusu mahitaji ya mtaala, hali
inayosababisha baadhi yao kutoutekeleza ipasavyo na hivyo kuwa chanzo cha
kushuka kwa kiwango cha ufaulu.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
79
4.3.4. Mafunzo Kabilishi kwa Ajili ya Mtaala Ulioboreshwa
Utafiti ulitaka kufahamu kuhusu mafunzo kabilishi yanayotolewa kwa walimu kwa ajili
ya mtaala ulioboreshwa na ulibaini kuwa, TET ndiyo yenye jukumu la kutoa mafunzo
hayo. Utafiti umebaini kuwa taarifa zilizotoka kwa wakaguzi wa kanda zote za elimu
kuhusu mafunzo kabilishi ni kwa walimu 1,088 ambao wametoka katika shule za
sekondari 192 tangu mwaka 2008 hadi 2010 na yalitolewa kwa walimu wa masomo
yote toka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Hii ni sawa na asilimia 2.7 ya idadi ya
walimu wote 40,517 kitaifa kwa mwaka 2010. Hali hii ilithibitishwa na walimu 613
(asilimia 92) ya waliohojiwa ambao hawakupata mafunzo kabilishi. Aidha, asilimia 8 ya
walimu waliopata mafunzo kabilishi walieleza kwamba mafunzo hayo yalitolewa
kupitia Chama cha Hisabati Tanzania, TAHOSSA na kutoka kwa walimu wenzao. Hii
iliungwa mkono na wakaguzi wa shule na wakuu wa shule waliobainisha kuwa
mafunzo kabilishi hayajafanyika kwa walimu wengi na kwamba walimu wana utayari
mdogo wa kutumia mihtasari iliyoboreshwa.
Taarifa ya TET, (2011) katika kipindi cha mwaka 2007 hadi 2010 inathibitisha kuwa
mafunzo kabilishi juu ya mtaala ulioboreshwa yalitolewa ni ya kiwango kidogo kwa vile
ni walimu 833 tu waliopata mafunzo kabilishi kitaifa. Hali hii inaashiria ugumu wa
walimu kutekeleza kwa ufanisi mitaala ya sekondari ya 2005 na 2007 na hivyo
kuwafanya wanafunzi kutofaulu mitihani ya Taifa.
Hivyo basi watekelezaji mitaala kama vile walimu, wapewe mafunzo kabilishi ili
kuwaimarisha katika utendaji kazi wao. Hii ni pamoja na kupata fursa ya mabadiliko
ya mtaaala na kupata dhana na nadharia za ufundishaji na ujifunzaji (Moduli ya Ujuzi
wa Kufundisha kwa Umahiri: WEMU, 2010).
4.3.5. Maoni Kuhusu Utekelezaji wa Mtaala
Ilipendekezwa kuwa mafunzo kabilishi yatolewe kwa walimu na wakufunzi wakati wa
mabadiliko au maboresho ya mtaala. Ilisisitizwa kuwa Mihtasari ya masomo
isambazwe shuleni mapema kila inapotokea maboresho na mabadiliko ya mtaala
yazingatie mahitaji ya jamii. Vilevile, ilielezwa ni muhimu kuwepo na muendelezo wa
mtaala wa shule za msingi na sekondari. Aidha, mahusiano kati ya wakuza mitaala,
maafisa mitihani na walimu yaimarishwe wakati wa maboresho na utekelezaji wa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
80
mtaala ili kuleta ufanisi katika utoaji wa elimu. Pia ilipendekezwa kuwa mitaala ya
elimu ya ualimu iboreshwe hususan katika maeneo ya malezi na maadili. Waliongeza
kuwa mtaala wa elimu ya msingi uboreshwe hususan katika stadi za Kusoma,
Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Aidha, ilishauriwa kuwa mtaala wa ufundi utayarishwe kwa elimu ya msingi na
ufundishwe kwa wanafunzi wa shule za msingi ili kuwaongezea fursa za kuajiriwa,
kujiajiri au kuendelea na masomo.
4.4. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa
Mfumo na taratibu za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 unahusisha mchakato wa
utungaji, uhakiki, usambazaji, usimamizi, usahihishaji na upangaji wa madaraja.
Utafiti ulifanyika ili kuelewa ufahamu wa wadau juu ya mchakato na taratibu za
mtihani na athari zake katika ufaulu.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa taratibu za uendeshaji na usimamizi wa Mtihani
wa Taifa wa Kidato cha 4 Mwaka 2010 ni mojawapo ya sababu zilizotajwa
kusababisha kushuka kwa ufaulu. Aidha ilibainishwa kuwa, utungaji wa mtihani,
usambazaji na usimamizi; usahihishaji, upangaji wa madaraja; matumizi ya miongozo
na nyaraka; Mchango wa alama za mazoezi endelezi (Continuous Assesssment-CA) na
athari za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 ni masuala yaliyoathiri kiwango cha ufaulu.
4.4.1. Utungaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4
Utungaji wa mtihani wa taifa unapaswa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa na utaratibu
wa NECTA ulio kwenye mwongozo uitwao Certificate of Secondary Examination
Format, 2008. Aidha utungaji unapaswa kuzingatia mwongozo wa upimaji na utahini
wa mtaala ulioboreshwa.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa lugha ya Kiingereza inayotumika kufundishia
elimu ya sekondari ni kikwazo kwa wanafunzi katika kuelewa kwa kina maudhui ya
somo na maswali. Katika mahojiano na wahitimu wa kidato cha 4 mwaka 2010,
asilimia 46 ya wanafunzi waliohojiwa walieleza kuwa misamiati iliyotumika kwenye
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
81
mtihani wa taifa haikufanana na ile iliyotumika kwenye mitihani ya kawaida ya
darasani. Mwanafunzi mmoja alisisitiza:
“Suala la wingi wa misamiati migumu na maswali mengi yenye lugha ya
kuchenga na yenye maelezo marefu yanatuchanganya. Hata walimu
wanaingia darasani wanatufundisha somo la English kwa kiswahili”.
Uelewa mdogo wa lugha ya kufundishia ni changamoto kwa watahiniwa katika
kuelewa maswali ya mitihani ya taifa.
Katika majadiliano ya pamoja na walimu ilithibitishwa kuwa lugha ya kiingereza ni
tatizo kubwa kwa walimu na wanafunzi. Kutokana na majadiliano hayo ya pamoja
inadhihirisha kuwa lugha ya Kiingereza haitumiki ipasavyo katika mchakato wa
kufundishia na kujifunzia. Tatizo hili linasababisha wanafunzi kushindwa kuelewa
kinachoulizwa katika maswali ya mtihani, kushindwa kujieleza kwa ufasaha na
hatimaye kufanya vibaya katika mtihani. Wahitimu 131 (33%) kati ya 401 wa kidato
cha 4 mwaka 2010 walithibitisha kuwa mtihani ulizingatia vigezo vilivyoainishwa
kwenye miongozo ya mitihani (Examination Formats) iliyoandaliwa na NECTA. Aidha,
asilimia 12 walieleza kuwa maswali ya mtihani katika baadhi ya masomo yalifuata
muundo wa mtihani wa taifa wakati masomo ya Kiswahili, Kemia, Historia na Jiografia
hayakufuata muundo. Hali hii ilichangia wanafunzi kushindwa kujibu inavyostahili.
Walimu walioshiriki kwenye majadiliano ya pamoja walieleza kuwa mtihani ulilenga
kupima uwezo wa wanafunzi katika kufikiri na uelewa wa dhana, hii ni tofauti na jinsi
walivyofundishwa darasani ambapo ufundishaji ulizingatia wanafunzi kujibu maswali.
Mwalimu mmoja alisisitiza kwa kusema:
“Utungaji wa Mtihani ulizingatia mtaala ulioboreshwa tatizo ni maandalizi
mabovu ya wanafunzi kwa kuwa walimu wengi tunaowafundisha watoto
hatujaelewa vizuri ufundishaji unaozingatia ujuzi na ujenzi wa maana”.
Matokeo haya yanaonesha kuwa wanafunzi wengi hawakufanya vizuri katika mitihani
kwa sababu ulipima malengo ya mtaala unaozingatia ujuzi na ujenzi wa maana
(Competence Based Curriculum) badala ya ule unaozingatia maarifa (Content Based
Curriculum).
Baadhi ya walimu wakati wa majadiliano ya pamoja waliwalaumu watungaji wa
mitihani kwa kueleza kuwa baadhi ya maswali yalitungwa nje ya mihtasari
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
82
iliyoboreshwa. Masomo hayo ni History, Geography, Physics na Mathematics. Mwalimu
mmoja alinukuliwa kwa kusema:
“…mtihani wa Historia ulikuwa na swali lililoulizwa ambalo halikutokana na
mada zilizopo kwenye muhtasari. Mada hiyo ni “Factors contributing to the
rise of Oyo Empire.”
Hivyo, utungaji wa maswali katika mtihani nje ya muhtasari yanakiuka taratibu za
utahini.
TET na NECTA wana jukumu la kuhakikisha kuwa mitihani inayotungwa inaendana na
maudhui yaliyo katika mtaala husika. Maoni yaliyotolewa na TET na NECTA katika
utafiti yamethibitisha kwamba upo udhaifu katika utungaji wa mitihani na kwamba
utungaji hauendi sambamba na mtaala ulioboreshwa katika baadhi ya masomo.
Utafiti umebaini kuwepo kwa tatizo la utungaji wa mtihani wa taifa linalochangiwa na
matumizi ya lugha ya kufundishia na kujifunzia, walimu kutofahamu ufundishaji wa
mtaala ulioboreshwa na utunzi wa mtihani usioendana na mahitaji ya mihtasari.
4.4.2. Usambazaji na Usimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4
Usambazaji na usimamizi wa mitihani ni muhimu katika mchakato wa uendeshaji wa
mitihani na unahitaji maandalizi mazuri, uadilifu na umakini ili kuhakikisha kuwa
taratibu zinafuatwa na haki inatendeka kwa kila mtahiniwa. Matokeo ya utafiti
yamebainisha kuwepo kwa mazingira yasiyoridhisha ya usimamizi wa mitihani, uwepo
wa askari polisi wenye silaha na wasimamizi kutumia lugha ya vitisho au/na
kuwakaripia watahiniwa wakati wa mitihani. MaafisaElimu wilaya 32 (73%) kati ya 42
waliohojiwa walisema kuwa, utaratibu wa usambazaji na usimamizi wa mitihani uliopo
ni mzuri, hivyo umepunguza undanganyifu wa mitihani. Hata hivyo, imebainishwa
kuwa baadhi ya wanafunzi wanaotegemea uvujaji na wizi wa mitihani husababisha
wasijiandae ipasavyo kwa matarajio ya kufanya undanganyifu.
Kwa upande mwingine, walishauri kuwa ulinzi wa mitihani uimarishwe na posho ya
wasimamizi iongezwe ili kuendelea kuzuia mianya ya uvujaji wa Mitihani. Pia,
ilipendekezwa kujenga vyumba imara vya kuhifadhia mitihani (strong rooms) na
kumbi za kufanyia mitihani ili watahiniwa wafanyie mitihani katika eneo moja kwa
lengo la kurahisisha usimamizi. Vilevile walisisitiza kuwa fedha za usambazaji na
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
83
usimamizi wa mitihani zipelekwe mapema kwenye Halmashauri husika ili kurahisisha
maandalizi.
Vilevile, katika majadiliano ya pamoja na maafisa mitihani ilibainishwa kuwa baadhi ya
wasimamizi hawana sifa na hawafuati maelekezo ya usimamizi wa mitihani hivyo
kusababisha usumbufu kwa watahiniwa. Aidha, maafisa mitihani waliendelea kusema
kuwa watahiniwa wanaochelewa kujisajili husababisha usumbufu wa mwingiliano wa
namba za mtihani wakati wa usimamizi.
4.4.3. Usahihishaji wa Mtihani ya Taifa wa Kidato cha 4
Usahihishaji unapaswa kufanywa kwa uadilifu, uaminifu na umakini mkubwa ili kutoa
matokeo sahihi na ya haki kwa kila mtahiniwa. Katika mahojiano ya pamoja na walimu
wasahihishaji ilielezwa kuwa kutokuwepo kwa umakini katika zoezi la usahihishaji wa
mitihani kunatokana na malipo kidogo na kutumia muda mrefu wa kusahihisha kwa
siku. Wakuu wa shule na walimu wasahihishaji wa mitihani ya taifa walibainisha kuwa
baadhi ya wasahihishaji hawana sifa ya kusahihisha mitihani hiyo. Hii inadhihirisha
kuwa zipo kasoro za uteuzi wa wasahihishaji katika ngazi ya shule ambapo baadhi ya
wakuu wa shule huteua walimu wasio na sifa stahili. Mwalimu ambaye hajawahi
kusahihisha mtihani alisema:
“uteuzi unategemea maelewano kati ya mwalimu na mkuu wa shule au
kama unatoa pesa kwa mkuu wa shule unaweza kuchaguliwa hata kama
hilo somo unaloenda kusahihisha hulifundishi darasani. Baadhi ya wakuu
wa shule hujichagua wao wenyewe au kuchagua walimu kwa mazoea,
undugu na urafiki, pia kuna walimu wa kudumu kwenye usahihishaji”
Hali hii inathibitishwa na NECTA ambapo huwarudisha walimu wasio na sifa kutoka
katika vituo vya kusahihishia, hivyo kusababisha usumbufu na kuathiri mchakato wa
usahihishaji.
Walimu waliowahi kusahihisha mitihani, walibainisha changamoto ya utaratibu wa
malipo kwa wasahihishaji kuwa malipo ni madogo kiasi kwamba yanawavunja moyo
wasahihishaji na wakati mwingine kulazimika kusahihisha haraka ili wamalize karatasi
za watahiniwa kwa muda mfupi. Katika kutilia mkazo hoja hii mwalimu mmoja
alieleza:
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
84
“Malipo ya walimu wasahihishaji hufanywa kwa kuzingatia idadi ya
karatasi za watahiniwa zilizosahihishwa wakati tunapaswa kulipwa posho
ya siku nje ya kituo cha kazi (Per- diem)”.
Walimu wengine walieleza kuwa mazingira ya kazi ya usahihishaji ni magumu hususan
uchafu wa vyoo na malazi; na ubovu wa huduma za chakula zinazopelekea
kutokuwepo kwa utulivu unaohitajika katika kazi muhimu ya usahihishaji. Vilevile,
katika majadiliano ya pamoja walimu walionesha masikitiko yao kwa kusema kuwa
kuna vitisho na manyanyaso kutoka kwa maafisa wa NECTA. Hali hiyo hujenga hofu
kwa msahihishaji na wakati mwingine kumvunja moyo na kushindwa kufanya kazi
ipasavyo.
Pia, walimu waliosahihisha mitihani ya kidato cha 4 walionesha kutoridhishwa na hali
ya kutoruhusiwa kusahihisha mwongozo wa usahihishaji kabla ya kuanza kuutumia
hata kama una makosa. Vilevile ilielezwa kuwa, wakati mwingine hutokea mapungufu
katika mwongozo wa usahihishaji lakini fursa ya kurekebisha haitolewi ipasavyo kwa
wasahihishaji. Hata hivyo, Maafisa Mitihani walieleza kuwa miongozo ya usahihishaji
hujadiliwa na paneli za masomo husika kabla ya kuanza usahihishaji.
Matokeo ya utafiti yamebaini kwamba, NECTA huandaa miongozo ya usahihishaji
iliyosanifiwa ipasavyo na kupeleka kwenye vituo vya usahihishaji, viongozi wa vikundi
pamoja na wasahihishaji wote hupewa nafasi ya kupitia mwongozo wa somo husika ili
kuelewa swali na majibu stahiki kabla ya kufanya jaribio la usahihishaji (trial marking)
kwa lengo la kubaini uelewa wa kila msahihishaji. Baada ya majadiliano ya jaribio la
usahihishaji, wasahihishaji wote hupitia mwongozo wa usahihishaji na kupata
mwongozo wa usahihishaji ulioboreshwa (standardized marking scheme) ambayo
hutumika katika usahihishaji (NECTA, Juni 2011).
Hoja ya usahihishaji wa kutokuwa makini inatofautiana na hali halisi kuhusu umakini
wa usahihishaji kama ilivyoelezwa na wajibuji wa NECTA. Mkanganyiko huu unaweza
kutafsiriwa kwa kuzingatia mazingira yanayotawala zoezi la usahihishaji. Kwa mfano
utaratibu wa kulipa wasahihishaji kwa idadi ya ‘scripts’ walizosahihisha badala ya
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
85
posho ya kujikimu na muda mrefu wa usahihishaji kwa siku ni baadhi ya masuala
yanayoweza kuathiri umakini wa usahihishaji.
Matokeo ya utafiti, yanathibitisha kuwa kuna kasoro na ukiukwaji wa vigezo vya uteuzi
wa walimu wasahihishaji na mazingira magumu ya usahihishaji unaosababisha
usahihishaji usiokuwa makini na kupoteza haki za watahiniwa. Kutofautiana kwa
uwepo wa fursa ya kutosha katika kujadili miongozo ya usahihishaji katika paneli za
masomo husika kunaweza kuwanyima haki baadhi ya watahiniwa.
4.4.4. Mchango wa Alama za Mazoezi Endelezi (Continuous Assessment-
CA) Katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4
Kutokana na mwongozo wa NECTA, ufaulu wa mwanafunzi katika mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4 unapimwa kwa kutumia alama za mazoezi endelezi (45%), projekti (5%)
na alama za mtihani wa mwisho (50%).
Matokeo ya utafiti yamethibitisha kuwa CA zinazowasilishwa NECTA zinajumuisha
alama za mitihani ya mihula ya kidato cha 3 na kidato cha 4 muhula wa kwanza.
Walimu walieleza kuwa alama za CA zinazowasilishwa NECTA hazitumiki, iwapo
zingetumika kusingekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofeli (mass failure). Hata
hivyo mwalimu mmoja wakati wa mahaojiano ya pamoja alisema:
“Hakuna mwenye uhakika kama CA zinatumika, tunajiliuza kuwa ikiwa
zinatumika vizuri kwanini watoto wamefeli masomo na kupata daraja la zero”
Aidha, Maafisa Mitihani wa NECTA walithibisha kuwa mwongozo wa mchango wa CA
ni 50% (45% ni mazoezi ya darasani na mitihani ya mihula na wa taifa Kidato cha 2
na 5% ya kazi mradi/projecti) hautekelezwi ipasavyo kwa kuwa umebuniwa mfumo
mbadala ambao unazingatia vingezo vingine. Vigezo hivyo ni pamoja na kufanya
ulinganifu sanifu (standardization) kwa kutumia alama za mwisho za mtahiniwa
(Candidates’ Final Written Examination marks) kama ilivyofafanuliwa katika taarifa ya
Miaka 30 (1973-2003) ya NECTA (NECTA, 2004). Mchakato wa kuzitumia CA kwa
ulinganifu sanifu ni mgumu na haueleweki kwa wadau, hoja hii ilithibitishwa na
Maafisa Mitihani katika majadiliano ya pamoja kuwa hawaufahamu mfumo huo.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
86
Matokeo ya utafiti yameonesha kuwepo kwa changamoto zinahusu upatikanaji na
matumizi ya CA kwenye matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha 4. Miongoni mwa
changamoto hizo ni pamoja na shule kuchelewa kuwasilisha CA kwenda NECTA, CA
zinazowasilishwa kutokuwa na uhusiano wa karibu na alama za mtahiniwa za Mtihani
wa Taifa wa Kidato cha 4 na uelewa mdogo wa wadau kuhusu mchango wa CA
katika mtihani wa Taifa.
Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa NECTA haitumii CA kama ilivyoelekezwa katika
mwongozo (Continuous Assessment Guidelines on the Conduct and Administration of
Continuous Assessment in Secondary Schools and Teacher Training Colleges-1990).
Aidha udanganyifu wa CA pamoja na uhusiano mdogo wa alama za CA na alama za
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 katika shule nyingi unaathiri ufaulu wa watahiniwa.
4.4.5. Upangaji wa Madaraja Unaofanywa na NECTA
Matokeo ya mtihani yanatolewa kwa viwango vya ufaulu kwa kila somo na kwa kila
mtahiniwa. Viwango vya ufaulu hupangwa katika madaraja ya I, II, III, IV na 0. Ili
kupata maoni ya wadau wa elimu kuhusu namna upangaji wa madaraja katika
matokeo ya mitihani ya taifa ya kidato cha 4, wakuu wa shule, wahadhiri wa vyuo
vikuu na wanachuo wa vyuo vikuu, wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu tarajali,
walimu, wahitimu na wanafunzi walishirikishwa.
Jumla ya walimu 613 waliohusika katika majadiliano ya pamoja walieleza kuwa
upangaji wa madaraja unafaa na unawafanya watahiniwa kujitahidi ili waweze kupata
madaraja mazuri. Hoja hii pia iliafikiwa na wakufunzi na wanachuo kwa kushauri
yafanyike marekebisho kwa kupanua msambao wa madaraja na pia nafasi kati ya
daraja moja na jingine zifanane. Vilevile jumla ya wakuu wa shule 109 (82.6%) kati ya
132 walisema kwamba, upangaji wa madaraja unafaa na kwamba uendelee kama
ulivyo kwani madaraja yanaleta ushindani miongoni mwa watahiniwa na hata kujenga
nidhamu ya kusoma.
Aidha, wanafunzi 1140 wa kidato cha 3 na 4 walioshiriki katika mahojiano ya pamoja
walitofautiana kuhusu upangaji wa madaraja, baadhi yao waliafiki na wengine
kukataa utaratibu wa upangaji wa madaraja unaotumika. Wanafunzi ambao
hawakuafiki, walisema hawakubaliani na upangaji wa madaraja kwa sababu hautoi
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
87
haki kwa watahiniwa. Mfano kutoa adhabu kwa wale wanaofeli somo la Hisabati au
Kiswahili kwa kushushwa madaraja.
Utafiti pia umebaini kuwa kuna tofauti ya uelewa kuhusu alama za gredi zinazotolewa
kwa watahiniwa. Aidha, uzoefu wa miaka mingi unaonesha kuwa Gredi zinatolewa
kwa kuzingatia mlolongo wa alama zifuatazo: A (81-100), B (61-80), C (41-60), D (21-
40), F (0-20). Hata hivyo NECTA imethibitisha kuwa alama za gredi zinazotolewa kwa
watahiniwa huamuliwa na jopo la wasahihishaji wa somo husika kwa kuzingatia
kiwango cha ufaulu kwa mwaka husika na hivyo hakuna alama maalum zilizowekwa
kwa kila gredi. Pia NECTA ilibainisha kuwa gredi D huwa si chini ya alama 30 na A si
chini ya alama 70.
Kutokana na matokeo ya utafiti huu, wadau wengi wamekubaliana na upangaji wa
madaraja uliopo sasa. Hata hivyo, kutokuwepo kwa alama za gredi zenye ulinganifu
baina ya shule na NECTA kumeleta mkanganyiko wa matumizi ya alama na gredi,
hivyo kuathiri ufaulu wa watahiniwa. Aidha, wanafunzi na walimu wakati wa
majadiliano ya pamoja ya wamelalamikia utaratibu wa Baraza la Mitihani la Tanzania
kutoa adhabu kwa walioshindwa kufaulu masomo ya Mathematics na Civics kwa vile
unalazimisha wanafunzi kusoma masomo wasiyoyapenda na wasiyokuwa na uwezo
nayo. Hali hiyo inaonesha kuwa kuna mapungufu ya kuadhibu watahiniwa kwa
kuwateremsha daraja la I au la II kuwa la III kutokana na kufeli baadhi ya masomo
ya msingi na ya mchepuo. Hata hivyo kulingana na kanuni za mitihani za mwaka 2006
za NECTA, hakuna kipengele chochote kinachobainisha adhabu hiyo.
Pamoja na juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia
kama ilivyobainishwa katika Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari awamu ya
kwanza na ya pili, bado kuna changamoto za uwepo wa walimu wa kutosha na vifaa.
Hivyo, kuwaadhibu watahiniwa ni kinyume na uhalisia wa mazingira ya kufundishia na
kujifunzia yenye uhaba wa vifaa na walimu hususani kwa somo la mathematics.
Usimamizi na uendeshaji wa mitihani ya Taifa unaonesha mapungufu katika matumizi
ya CA na upangaji wa madaraja tofauti na ilivyoelekezwa na Sera ya Elimu na
Mafunzo, 1995 ibara ya 6.18 pamoja na Mwongozo wa NECTA wa Mazoezi Endelezi
wa 1990.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
88
4.4.6. Matumizi ya Miongozo na Nyaraka Mitihani
Utafiti huu ulilenga kubaini usambazaji na utekelezaji wa miongozo, nyaraka na
machapisho ya elimu na mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Ilibainishwa kwamba
nyaraka, miongozo na mihtasari ya masomo kutoka Wizara ya Elimu huwafikia wakuu
wa shule kupitia ofisi za maafisaelimu na mikutano ya TAHOSSA kwa ajili ya
utekelezaji. Aidha, jukumu la NECTA ni kusambaza shuleni miongozo na machapisho
yanayohusu uendeshaji wa mitihani ya Taifa kama vile muundo (format) na kanuni za
mitihani kupitia Maafisaelimu wa Mikoa.
Utafiti umebaini kuwa, asilimia 67 ya walimu 613 katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti
walieleza kuwa hupokea muundo na kanuni za mitihani na kuzitumia katika kutunga
mazoezi ya darasani na mitihani ya ndani. Hata hivyo asilimia 33 ya walimu walieleza
kuwa hawajawahi kuuona na kuutumia muundo wa mtihani wa Taifa kwa kuwa
machapisho na nyaraka zinazotoka NECTA zinakuwa na usiri mkubwa. Hayo
yalithibitishwa na mmoja wa maafisa mitihani wa NECTA kwa kusema:
“....Nimefundisha shule ya sekondari kwa muda wa miaka kumi na
sikuwahi kuiona format ya mtihani mpaka nilipofika NECTA......”
Hii inaonesha jinsi ambavyo baadhi ya walimu na wanafunzi hawapati fursa ya kuiona
na kuitumia miundo ya mitihani na miongozo katika shule za sekondari. Uwepo wa
Nyaraka na miongozo mbalimbali ya mitihani katika shule ni muhimu katika
kumwandaa mtahiniwa hivyo, wadau wote wanapaswa kupata na kutumia
machapisho hayo.
4.4.7. Athari za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 hutoa tathmini ya kati ya elimu ya
sekondari ya kawaida ili kupata picha ya maendeleo ya wanafunzi kitaifa kabla ya
mtihani wa kidato cha nne. Mojawapo ya malengo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha
2 ni kupata alama zenye uwiano wa kitaifa kwa ajili ya kupima maendeleo ya
wanafunzi ambazo zitatumiwa na NECTA ikiwa ni sehemu ya mazoezi endelezi ya
mwanafunzi (CA). Tangu mwaka 1999 hadi 2007, mtihani huu ulitumika kama kigezo
cha kuchuja wanafunzi kuingia kidato cha 3. Kuanzia 2008 mpaka sasa, Mtihani wa
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
89
Taifa wa Kidato cha 2 hautumiki kuchuja wanafunzi kuendelea na masomo ya kidato
cha 3. Utafiti umebaini kuwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 kutotumika kuchuja
wanafunzi kuingia kidato cha 3 umesababisha wanafunzi kutojishughulisha katika
kujifunza kwa kukosa changamoto na hatimaye wanafunzi wasio na uwezo kupata
fursa ya kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Hali hii pia inawafanya walimu
kutofundisha kwa bidii.
Aidha, kuna uhusiano wa kitakwimu wa viwango vya ufaulu kwa wanafunzi waliofanya
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 mwaka 2008 na baadaye kidato cha 4 mwaka 2010
kwa baadhi ya shule zilizofanyiwa utafiti. Mfano, katika shule ya sekondari Siera
iliyopo Manispaa ya Kinondoni, wanafunzi waliofanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha
2 mwaka 2008 walifaulu kwa asilimia 15.0 na walipofanya Mtihani wa Taifa wa Kidato
cha 4 mwaka 2010 walifaulu kwa asilimia 15.4. Hii inaonesha kiwango cha ufaulu wa
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 kinakaribiana na kile cha kidato cha 4 kama
inavyooneshwa katika Kielelezo Na. 4.7 na 4.8. Pia takwimu zinaonesha kuwa ufaulu
wa shule ya sekondari Maghang, Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 mwaka 2008 ni
asilimia 83.4 na asilimia 81.0 kwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kwa mwaka 2010.
Kielelezo Na. 4.7: Kiwango cha Ufaulu katika Shule Zilizofanya Vizuri
katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 Mwaka 2008 na cha 4 Mwaka 2010
Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
90
Takwimu hizo zinaonesha kuwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 hubashiri matokeo
ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Mtihani huu hutumika kutoa tathmini ya kati kwa
shule na kwa mwanafunzi, pia huongeza ari ya ufundishaji na ujifunzaji. Upo uhusiano
kati ya kufundisha, kujifunza na mitihani.
Kielelezo Na. 4.8: Kiwango cha Ufaulu katika Shule Zilizofanya Vibaya
katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 Mwaka 2008 na cha 4 Mwaka 2010
Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011
Mitihani humfanya mwanafunzi ajitahidi kurudia kwa makini yale aliyofundishwa, na
mwalimu hufundisha kwa kuzingatia kile kinachotakiwa katika mtihani. Hivyo, mtihani
hutoa msukumo wa kufundisha na kujifunza. Kwa hiyo, kutotumika kwa Mtihani wa
Taifa wa Kidato cha 2 kuchuja wanafunzi kuingia kidato cha 3 kumechangia kuathiri
ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010.
4.4.8. Maoni Kuhusu Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa
Wadau mbalimbali waliohusishwa katika utafiti huu walitoa maoni kuhusu sifa za
kujiunga na kidato cha 1; kuboresha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2; Kuimarisha
mitihani ya majaribio ya kujipima shuleni na kuimarisha utungaji, usimamizi,
usahihishaji, upangaji wa madaraja, mchango wa alama za CA na matumizi ya miongo
na nyaraka.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
91
a) Sifa za Kujiunga na Kidato cha 1
Ilipendekezwa kuwa alama za ufaulu katika kujiunga na kidato cha kwanza ziwe 125
(50%) badala ya kiwango kidogo cha ufaulu cha alama ya 100 (40%) kati ya 250 na
walioshindwa kupata alama za ufaulu wasiruhusiwe kujiunga na sekondari za binafsi.
Aidha, wanafunzi wa chaguo la pili wasichelewe kuandikishwa kwa kuwa ni moja ya
sababu zilizobainishwa kushusha kiwango cha ufaulu.
b) Kuboresha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2
Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 kutotumika
kama kigezo cha kuchuja wanafunzi kuendelea na kidato cha 3 huwafanya wanafunzi
wasiomudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kufikia hatua ya kufanya
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 na hatimaye kufeli.
Ushauri ulitolewa na wajibuji katika utafiti kwamba Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2
uendelee kutumika kama kigezo cha kumfanya mwanafunzi kuingia kidato cha 3 na
wastani wa kuimarisha alama hizo uwe 40 badala ya 30. Hali hii inaonesha kuwa
kuna umuhimu wa kuchuja wanafunzi katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2. Pia
utafiti kati ya waliofeli Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 na cha 4 ufanyike ili kubaini
kwa kina uhusiano uliopo.
c) Kuimarisha Mitihani ya Majaribio ya Kujipima Shuleni
Utafiti umebaini kuwa kuna mapungufu katika uendeshaji na tathmini ya mitihani ya
majaribio katika kumwandaa mwanafunzi kufanya mitihani ya kitaifa. Maoni yalitolewa
kuhusu kuwepo na utaratibu mzuri wa uendeshaji wa mitihani ya majaribio shuleni
ikiwemo mitihani inayoshindanisha shule kiwilaya, kimkoa au kikanda. Vilevile
imependekezwa kuwa uendeshaji wa mitihani ya majaribio (Mock examinations)
iangaliwe upya kwa vile haikidhi viwango na taratibu za uendeshaji. Pia, kuwepo na
mitihani ya kuchuja kwa kila darasa na kidato ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata
stadi muhimu kwa kila ngazi.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
92
d) Kuimarisha Utungaji, Usimamizi, Usahihishaji na Upangaji wa
Madaraja katika Mtihani wa Taifa
Wadau wa elimu waliohusika katika utafiti walitoa maoni kuwa mitihani itungwe
kutokana na mtaala ulioboreshwa ambao unalenga katika kupima ujuzi; Waliongeza
kwa kusema kuwa maelekezo na lugha inayotumika katika utunzi wa mitihani isiwe
ngumu ya kuwachanganya watahiniwa pia lugha rafiki itumike kwa wasimamizi wa
mtihani.
Sambamba na hilo, ilishauriwa kuwa muundo wa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi
ubadilishwe ili kuruhusu maswali ya kujieleza kwa lengo la kuimarisha taaluma na
kupunguza udanganyifu. Aidha, kipimo kingine cha ufaulu wa Mtihani wa Kumaliza
Elimu ya Msingi kitumike badala ya kutumia mtihani wa mwisho tu. Vilevile, wanafunzi
wanapomaliza mtihani nakala za karatasi za maswali zibaki shuleni kwa ajili ya rejea.
Kuhusu mitihani ya taifa ilishauriwa kuwa isahihishwe kikanda na wasahihishaji wa
mtihani wa kidato cha 4 waongezwe na wapewe muda wa kutosha ili wasahihishe kwa
umakini. Vilevile, vigezo vya kuchagua wasahihishaji viwekwe bayana na posho zao
ziboreshwe. Serikali iendelee kudhibiti uvujaji wa mitihani ili kujenga ari ya kujifunza
kwa wanafunzi na tathimini ya matokeo ya mtihani ijadiliwe kwa ngazi zote.
Vilevile, alama za mazoezi endelezi (CA) zitumike kulingana na miongozo na
maelekezo ya mihtasari; Muundo wa mtihani (format) uzingatiwe na kusambazwa
shuleni kwa wakati. Aidha, uhakiki wa wanafunzi wanaotaka kufanya mtihani ufanyike
kwa wakati muafaka. Zaidi ya hayo, ilishauriwa kuwa mitihani ya ‘altenative to
practical’ iondolewe. Pia walisisitiza kuwa, watahiniwa waelimishwe juu ya masharti ya
mitihani na adhabu zinazoandamana na ukiukaji wa masharti hayo.
Maoni yaliyotolewa na wadau yanaonesha kuwa ipo haja ya kufanya marekebisho
katika mchakato wa utungaji, usimamizi, usahihishaji, mchango wa alama za CA,
upangaji wa madaraja katika mtihani wa Taifa, matumizi ya mongozo na nyaraka za
mitihani na Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 na sifa na mitihani ya majaribio ya
kujipima shuleni.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
93
4.5. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu
Ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu ni muhimu ili kubaini ufanisi wake katika
kufanikisha na kutekeleza mtaala katika ngazi mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji.
Ufuatiliaji na tathmini ya mtaala wa elimu ya sekondari ulioboreshwa hufanyika katika
ngazi zote za usimamizi na utekelezaji kwa kuwahusisha wakuza mitaala, maafisa
mitihani, wakaguzi, walimu na wadau wengine wa elimu.
4.4.1 Ufuatiliaji na Tathmini ya Mtaala Ulioboreshwa
Ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa mitaala ni jukumu la Taasisi ya Elimu
Tanzania, chombo ambacho kisheria kina jukumu la kubuni na kutayarisha mitaala ya
elimu nchini. Matokeo ya utafiti yamebainisha kwamba asilimia 100 ya wajibuji wanne
wa dodoso walieleza kuwa tathmini zilizofanywa na TET katika shule nchini ni mbili
kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2000 hadi 2010. Tathmini ya kwanza ilifanyika
mwaka 2003 ambayo ilihusu tathmini ya utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Msingi na
tathmini ya pili mwaka 2004 ilihusu utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Sekondari.
Aidha, utafiti umebaini kuwa TET huwasilisha ripoti na taarifa za utekelezaji wa
mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali wa elimu kwa Wizara yenye
dhamana. Imeelezwa zaidi kuwa mapendekezo hayo ya wadau wa elimu hutumika
kuboresha Mitaala ya elimu nchini kama ilivyofanyika kwa mitaala ya sekondari ya
mwaka 2005 na 2007. Taarifa hii ya utafiti imeonesha wazi uchache wa tathmini za
mitaala zilizofanyika katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Kutofanyika tathmini kwa wakati kuhusu utekelezaji wa mtaala hakutoi fursa kwa
serikali na wadau wa elimu kubaini changamoto na matatizo katika utoaji wa elimu na
kuyapatia ufumbuzi, hivyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa mtaala.
4.4.2 Utaratibu wa Kufuatilia Maendeleo ya Ufundishaji na Ujifunzaji
Shuleni
Taarifa zilizotokana na dodoso lililojibiwa na wakuu wa shule za sekondari 132 zilieleza
kuhusu ufuatiliaji wa maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi pamoja na
utaratibu wa kufikisha taarifa kwa watahiniwa. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa
wakuu wa shule 68 (51%) kati ya waliohojiwa hufuatilia mchakato wa ufundishaji na
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
94
ujifunzaji kwa kukagua maandalio ya masomo, mpango wa kazi, matumizi ya zana,
mahudhurio ya walimu darasani, kukagua shajara na kuangalia kazi za wanafunzi
darasani. Pia wakuu wa shule hao walieleza kuwa wana utaratibu wa kuzungumza na
wazazi/walezi, walimu na wanafunzi kuhusu umuhimu wa maendeleo ya kitaaluma.
Aidha, asilimia 49 ya wakuu wa shule hawakueleza chochote namna wanavyofuatilia
maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi. Uchambuzi wa data hapo juu
umeonesha kwamba baadhi ya wakuu wa shule hawatekelezi kikamilifu usimamizi wa
taaluma shuleni.
Mkuu wa shule ni msimamizi mkuu wa taaluma shuleni, ana wajibu wa kuhakikisha
uendeshaji wa shughuli za kila siku za shule na kusimamia utekelezaji wa mitaala,
hivyo ni vema asimamie kikamilifu majukumu yake kama ilivyoainishwa katika
Mwongozo wa Usimamizi wa Shule (WEMU, 2010).
4.4.3 Ukaguzi wa Shule
Ukaguzi katika utekelezaji wa mtaala ni muhimu ili kubaini changamoto zake kwa
lengo la kuleta ufanisi na kuboresha elimu katika ngazi mbalimbali za ufundishaji na
ujifunzaji. Hivyo basi, jukumu la Ukaguzi wa Shule ni kusimamia na kuhakiki ubora wa
elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na vyuo vya Ualimu nchini. Ili
kufikia malengo ya utekelezaji wa majukumu yao, wakaguzi wa shule hufanya ukaguzi
wa jumla wa shule; ukaguzi wa kufuatilia na ukaguzi maalum (Kiongozi cha Mkaguzi
wa shule, 2006). Utafiti huu ulilenga kupata taarifa juu ya ukaguzi wa shule wa jumla.
Katika Kiongozi cha Mkaguzi wa shule imeelezwa kuwa kila shule itakaguliwa angalau
mara moja katika kipindi cha miaka mitatu. Katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti
imebainika kuwa shule 18 (13.53%) zilikaguliwa mara 3 hadi 4 kwa kipindi cha mwaka
2006 hadi 2010. Hali kadhalika shule 69 (51.88%) zilikaguliwa mara moja au mbili, na
shule 46 (34.59%) hazikukaguliwa kabisa. Angalia jedwali katika Kiambatisho Na. 4.1
Aidha utafiti umebaini kuwa, takwimu za ukaguzi wa shule zilizopatikana katika
Halmashauri 22 zilizofanyiwa utafiti zinaonesha kati ya mwaka 2006 na 2010 kiwango
cha ukaguzi wa shule cha kuridhisha kilifanyika katika Halmashauri za Sumbawanga
(100%), Tanga Jiji (91.3%), Mpanda (84%), Kinondoni (78.26%) na Babati
(75.76%). Hata hivyo, Halmashauri za Kilwa (12.50%) na Lindi (15.38%) zilifanya
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
95
ukaguzi wa shule kwa kiwango cha chini, wakati shule za Halmashauri za Karagwe,
Muleba, Bagamoyo, Maswa, Singida Vijijini na Manyoni hazikukaguliwa. Vilevile,
katika Halmashauri za Ilala na Mbinga takwimu hazikupatikana kama inavyooneshwa
katika Jedwali Na 4.1.
Jedwali Na.4.1: Idadi ya Shule za Sekondari Zilizokaguliwa katika
Halmashauri Zilizofanyiwa Utafiti, 2006 – 2010
Na. Kanda Halmashauri Idadi ya
shule
zilizoripotiwa
Idadi ya shule
zilizokaguliwa
Asilimia ya
ukaguzi
1
DAR ES
SALAAM
Kinondoni 46 36 78.26
Ilala 91 Hakuna takwimu -
2
ZIWA
MAGHARIBI
Karagwe 47 0 0
Muleba 41 0 0
3
KUSINI Kilwa 24 3 12.50
Lindi 26 4 15.38
4
KASKAZINI
MAGHARIBI
Babati 33 25 75.76
Mbulu 34 10 29.41
5
MARA Bunda 30 9 30.00
Musoma 24 10 41.67
6
MASHARIKI Mkuranga 30 7 23.33
Bagamoyo 34 0 0
7
NYANDA ZA
JUU
Sumbawanga 34 34 100.00
Mpanda 25 21 84.00
8
NYANDA ZA
JUU KUSINI
Songea[v] 28 6 21.43
Mbinga 61 Hakuna takwimu -
9
MAGHARIBI Bukombe 26 4 15.38
Maswa 38 0 0
10
KATI Singida Vijijini 61 0 0
Manyoni DC 30 0 0
11
KASKAZINI
MASHARIKI
Tanga Jiji 46 42 91.30
Lushoto 79 13 16.46
JUMLA 888 224
Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011
Utafiti umebaini kuwepo kwa kiwango kidogo cha ukaguzi wa shule na kutotekelezwa
kikamilifu kwa mapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa shule, hali inayosababisha
kutokuwepo kwa ufanisi wa usimamizi na utoaji wa elimu bora.
Vilevile, kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa shule asilimia
61.7 ya Maafisaelimu mikoa na Halmashauri pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri
waliohojiwa walithibitisha kuwa, maoni/mapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa shule
hufanyiwa kazi kwa kufanya ufuatiliaji katika shule husika ili kubaini mapungufu na
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
96
kujiridhisha kama mapendekezo ya ukaguzi yanatekelezwa. Ilielezwa kuwa Bodi za
Shule zinahusika katika utekelezaji wa mapendekezo hayo na kuweka mpango
mkakati ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza. Aidha, kuhusu masuala ya nidhamu ya
walimu, Ofisi za Elimu hushirikiana na TSD kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa
katika taarifa za ukaguzi wa shule.
Asilimia 73.17 (30) ya wakaguzi wa shule kanda walitofautiana na Maafisaelimu wa
mikoa, Wakurugenzi na Maafisaelimu wa Halmashauri kwa kueleza kuwa
mapendekezo ya taarifa za ukaguzi wa shule hayatekelezwi au utekelezaji wake ni wa
kiwango cha chini.
Matokeo ya utafiti yameonesha kuwepo kwa changamoto zinazohusu ukaguzi wa
shule ambapo shule hazikaguliwi kama ilivyoainishwa katika Kiongozi cha Mkaguzi wa
Shule (2006). Vilevile imebainika kuwa kiwango kidogo cha ukaguzi wa shule za
sekondari hali ambayo imesababishwa na ongezeko la shule ambazo haikwenda
sambamba na ongezeko la idadi ya wakaguzi wa shule na vitendea kazi. Idadi kubwa
ya wanafunzi iliyobainishwa inatofautiana na Waraka wa Elimu Na 16 wa Mwaka 2002
ambayo inapaswa kuwa 1:40, hivyo kuathiri uendeshaji wa elimu.
4.4.4 Maoni Kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu
Kutokana na matokeo ya utafiti, imebainika kuwa mfumo wa ukaguzi uliopo haukidhi
malengo tarajiwa. Hivyo, wajibuji walipendekeza kwamba ukaguzi wa shule
uimarishwe kwa kuwajengea uwezo wakaguzi na kuwapa raslimali za kutosha ili
wakague shule ipasavyo.
Mfumo wa Ukaguzi wa shule uliopo sasa ni kwamba ukaguzi wa shule za msingi upo
katika ngazi ya wilaya na wa sekondari katika ngazi ya kanda. Kutokana na upanuzi
wa shule za sekondari na uamuzi wa serikali kugatua usimamizi na uendeshaji wa
shule za sekondari kuwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa, kuendelea na mfumo
uliopo wa ukaguzi wa shule za sekondari hauwezi kuwa wa ufanisi. Hivyo, Ukaguzi wa
Shule katika ngazi ya wilaya uimarishwe ili kuwawezesha wakaguzi kukagua shule za
sekondari. Aidha, kuwe na ofisi za ukaguzi katika ngazi ya mkoa badala ya kanda ili
kusimamia utekelezaji wa ukaguzi ngazi ya Wilaya.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
97
4.6. Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu
Ufanisi katika elimu unazingatia uwepo wa raslimali watu wa kutosha na wenye sifa.
Uwepo wa walimu wa kutosha na wafanyakazi wengine wasio walimu kama vile
wahasibu, mafundi mchundo maabara (laboratory technicians) na wakutubi huchangia
katika utoaji wa elimu bora shuleni. Walimu bora na wenye sifa hutokana na mfumo
wa kuwaandaa tangu wakiwa katika mafunzo tarajali. Aidha, mafunzo kazini ni eneo
lingine linaloongeza ubora wa walimu hao kwa kuwaongezea stadi na ujuzi kulingana
na mahitaji ya mtaala.
4.6.1. Mfumo wa Utayarishaji wa Walimu
Utafiti umebaini kuwa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji wa walimu tarajali
pamoja katika vyuo hivyo umeelezwa kutokuwa fanisi kutokana na changamoto
mbalimbali, ikiwemo sifa za chini kwa wahitimu wanaojiunga na mafunzo ya
stashahada, upungufu wa miundo mbinu, vitabu, mihtsari na idadi kubwa ya walimu
tarajali isiyoendana mahitaji.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa asilimia 70 (56) ya wahadhiri, wakufunzi na
wanachuo waliohojiwa walibainisha sifa zinazotakiwa kudahili walimu tarajali za
principal pass 1 na subsidiary 1 hazimfanyi mwalimu anayeandaliwa kuwa mahiri.
Barua ya Kamishna yenye Kumb.Na TTDB/85/483/01/25, ya mwaka 2009 inaeleza sifa
za wanaojiunga na mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada ni ‘Principal Pass’ moja na
‘Subsidiary’ moja katika masomo mawili yanayofundishwa shule za sekondari. Kwa sifa
hizo ni wazi kuwa mwalimu anaeandaliwa hatamudu kufundisha masomo mawili
katika ubora unaostahili.
Aidha, utafiti ulibaini kuwa baadhi ya wadahiliwa wamekuwa wakitumia vyeti vya
kughushi na wengine hawana wito wa kazi ya ualimu kwa kuwa wanajiunga katika
mafunzo ya ualimu baada ya kukosa fursa nyingine walizotarajia.
Vilevile, matokeo ya utafiti yamebaini uwepo wa maandalizi yasiyotosheleza ya walimu
katika vyuo vya ualimu unaosababisha walimu wengi kufundisha kwa njia ya maswali
badala ya kuzingatia ujenzi wa dhana na vitendo kama mtaala unaozingatia ujuzi
(competence based curriculum) unavyoelekeza. Asilimia 67(54) ya wahadhiri,
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
98
wakufunzi na wanachuo waliohojiwa walisema kwamba wingi wa wanafunzi katika
mkondo mmoja husababisha kutokuwa na makusano ya kutosha (limited interaction)
kati ya wakufunzi na walimu tarajali na kuwalazimu wakufunzi kutumia ufundishaji wa
kipurure (Lecturing ). Mmoja wa wahadhiri aliongeza kwa kusema,
“Walimu wanaoandaliwa kwa mfumo huu hawawezi kuwa mahiri kutekeleza
mtaala ulioboreshwa ambao unasisitiza njia shirikishi”.
Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa, maandalizi ya walimu tarajali vyuoni hayafanyiki
ipasavyo kutokana na kukosekana kwa vitendea kazi na miundombinu na baadhi ya
wakufunzi kutokuwa makini katika kufundisha kwa kuzingatia mahitaji ya mtaala wa
ualimu ulioboreshwa. Hali hii inasababisha walimu wanaoandaliwa kutokuwa mahiri.
Utafiti pia umebaini kuwepo kwa uhaba wa vitabu na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia katika baadhi ya vyuo ambapo ilielezwa na wakufunzi na wanachuo
waliohojiwa kuwa vitabu havitoshelezi na hata vilivyopo haviendani na mtaala
ulioboreshwa. Wajibuji walibainisha kuwepo kwa upungufu wa mabweni kwa walimu
tarajali.
Aidha, kupungua kwa muda wa mazoezi kwa vitendo (Teaching Practice) kuwa wiki
nne kumeathiri kwa kiasi kikubwa ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, matokeo ya utafiti
yamebaini kuwa walimu tarajali wanaandaliwa kwa kiwango kidogo katika mada za
ufundishaji, namna ya kuandaa azimio la kazi, andalio la somo, namna ya kufanya
nukuu za somo na zana za kufundishia somo kwa kuzingatia mihtasari iliyoboreshwa.
Aidha, walieleza kuwa mitihani hutolewa kwa kutumia mihtasari ya zamani. Hali
kadhalika, ilielezwa kuwa hakuna moduli za mada za mafunzo ya ualimu zilizoandaliwa
na TET katika kukidhi mahitaji ya mihtasari mipya.
4.6.2. Ajira na Upangaji wa Walimu
Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa baadhi ya viongozi siyo waadilifu katika kupanga
walimu. Viongozi hao hupanga walimu bila ya kuzingatia mahitaji ya walimu katika
shule za mijini na vijijini. Hali hii inasababisha kutokuwepo kwa mgawanyo linganifu
wa walimu kati ya shule za mijini na zile za vijijini hivyo kusababisha sehemu zenye
mazingira magumu kuwa na upungufu wa walimu. Pia, katika baadhi ya Halmashauri
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
99
utafiti umebaini kuwa baadhi ya watendaji huwadai walimu rushwa ya ngono, hayo
yalidhihirishwa katika mahojiano ya pamoja na walimu, ambapo mwalimu mmoja wa
kike alibainisha:
“Baadhi ya watendaji wa Halmashauri wamekuwa na tabia ya kuwadhalilisha
walimu wa kike kwa kuwataka kimapenzi wanapotaka kupangwa katika shule
zenye mazingira mazuri ya kufanyia kazi“.
Hali hii inaleta athari katika malezi bora ya wanafunzi kwa baadhi ya shule kukosa
walimu hususani wa kike, mfano shule ya sekondari Wariku katika Halmashauri ya
Bunda wanafunzi wasichana walilalamika kuwa wanakosa mwalimu wa kike wa
kumweleza matatizo yao.
Waraka wa Elimu Na. 4 wa mwaka 2001 unatoa maelekezo kwa watendaji wa
Halmashauri kuondoa mrundikano wa walimu kwa shule za mijini. Utafiti umebaini
kuwa bado hakuna uwiano linganifu wa ikama ya walimu katika Halmashauri hali
inayo athiri ufundishaji na ujifunzaji. Utafiti umebaini kuwa hakuna uwiano mzuri wa
mgawanyo wa walimu unaozingatia jinsi na idadi ya masomo yanayofundishwa
shuleni. Katika mahojiano ya pamoja na walimu walilalamika kuwa, baadhi ya shule
zina walimu wengi wa somo moja wakati shule zingine hazina walimu masomo hayo
kabisa.
Jedwali Na. 4.2 linaonesha mahitaji, uwepo, upungufu na ziada ya walimu katika
masomo ya msingi kwa baadhi ya shule za sekondari za serikali za Mkoa wa Dar Es
Salaam zilizofanyiwa utafiti. Hali hii inathibitisha mgao wa walimu usiozingatia ikama,
mfano kuna ziada ya walimu katika baadhi ya masomo (idadi katika mabano) ya
Biology (4) , English (2), Geography (3) na Physics (2) katika shule ya sekondari ya
Jangwani wakati shule ya Mkera ina upungufu wa masomo hayo katika Halmashauri
hiyo hiyo ya Ilala.
Hata hivyo Maafisaelimu Mikoa, Wakurugenzi na Maafisaelimu wa Halmashauri
waliohojiwa walitofautiana na walimu kwa kueleza kwamba upangaji wa walimu
unazingatia mahitaji ya shule kimasomo (87%), jinsi na sifa ya ndoa (9%), hali ya
afya na mahitaji maalum ya mwalimu (2%) na kipaumbele kwa shule za pembezoni
(2%).
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
100
Jedwali Na 4.2: Mahitaji, Uwepo na Upungufu/Ziada ya Walimu katika
Baadhi ya Shule Sekondari za Serikali za Mkoa wa Dar Es Salaam
Shule
Mathematcs
English
Kiswahili
Biology
Chemistry
Civics
Physics
Geography
History
Jumla
Mkera
Mahitaji 4 4 4 4 4 4 4 4 4 36
Waliopo 3 2 3 3 2 2 2 2 2 21
Upungufu 1 2 1 1 2 2 2 2 2 15
Ziada 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0
Nyeburu
Mahitaji 4 4 4 4 4 4 4 4 4 36
Waliopo 1 6 5 4 7 4 3 6 4 40
Upungufu 3 0 0 0 0 0 1 0 0 4
Ziada 0 2 1 0 3 0 0 2 0 8
Jangwani
Mahitaji 12 10 7 9 9 6 6 10 8 77
Waliopo 11 12 8 13 10 7 8 13 7 89
Upungufu 1 0 0 0 0 0 0 0 1 2
Ziada 0 2 1 4 1 1 2 3 0 14
Azania
Mahitaji 13 11 8 8 8 8 9 8 9 82
Waliopo 11 8 12 9 10 7 9 9 7 82
Upungufu 2 3 0 0 0 1 0 0 2 8
Ziada 0 0 4 1 2 0 0 1 0 8
Kambangwa
Mahitaji 8 8 5 5 3 7 4 5 8 53
Waliopo 8 7 6 8 5 6 3 8 7 58
Upungufu 0 1 0 0 0 1 1 0 1 4
Ziada 0 0 1 3 2 0 0 3 0 9
Goba
Mpakani
Mahitaji 4 4 2 3 2 2 2 3 2 24
Waliopo 2 2 2 2 2 0 2 2 0 14
Upungufu 2 2 0 1 0 2 0 1 2 10
Ziada 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0
manzese
Mahitaji 8 8 4 5 5 3 5 5 5 48
Waliopo 8 8 7 7 4 3 2 4 6 49
Upungufu 0 0 0 0 1 0 3 1 0 5
Ziada 0 0 3 2 0 0 0 0 1 6
Salma
Kikwete
Mahitaji 6 5 4 4 4 4 4 4 4 39
Waliopo 3 4 4 1 1 1 1 5 5 25
Upungufu 3 1 0 3 3 3 3 0 0 16
Ziada 0 0 0 0 0 0 0 1 1 2
Chanzo: Takwimu za Utafiti 2011
4.6.3. Uwepo wa Walimu katika Shule
Uwepo wa walimu katika shule siyo sababu pekee ya kuinua kiwango cha ufaulu wa
wanafunzi, bali hutegemea pia utayari na ubora wa walimu. Utayari wa walimu
hutokana na kujengewa fursa na mazingira ya kuvutia ya kazi. Pamoja na jitihada za
serikali katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kama ilivyobainishwa
katika Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari awamu ya kwanza na ya pili,
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
101
bado kuna changamoto za uwepo wa walimu wa kutosha. Matokeo ya utafiti
yamebaini upungufu wa walimu katika shule za serikali na zisizo za serikali kama
ilivyooneshwa katika jedwali Na. 4.3.
Jedwali Na 4.3 Uwepo wa Walimu katika Baadhi ya Shule Zilizofanyiwa
Utafiti
Jina la Shule Aina
ya
Shule
Mkoa Wilaya Idadi
ya
walimu
Idadi ya
wanafun
zi
Uwiano wa
mwalimu na
mwanafunzi
Monica Mbega Serikali Ruvuma Mbinga 3 308 1:103
Ughandi Serikali Singida Singida(V) 3 382 1:127
Senani Serikali Shinyanga Maswa 3 178 1:59
Majebele Serikali Shinyanga Maswa 3 219 1:73
Iyogelo Serikali Shinyanga Maswa 4 362 1:91
Kireti Serikali Tanga Lushoto 2 292 1:146
Kisiju Serikali Pwani Mkuranga 4 501 1:125
Ikola Serikali Rukwa Mpanda 3 334 1:111
Mipingo Serikali Lindi Lindi (V) 2 59 1:30
Mtanga Serikali Lindi Kilwa 4 244 1:61
Chitengule Serikali Mara Bunda 6 853 1:142
Upendo Binafsi Tanga Lushoto 9 193 1:21
Mkwese Binafsi Singida Manyoni 7 83 1:12
Madunga Binafsi Manyara Babati 9 184 1:20
Rondo Seminary Binafsi Lindi Lindi (v) 8 168 1:21
Victoria Binafsi Mara Musoma(V) 14 158 1:11
Goldenland Binafsi Shinyanga Bukombe 10 376 1:38
Kikodi Binafsi Ruvuma Mbinga 10 334 1:33
Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011
Jedwali Na.4.3 linaonesha kuwa baadhi ya shule za sekondari za serikali zilizofanyiwa
utafiti zina wastani wa uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi zaidi ya 100
(1:100). Wastani wa uwiano huu haulingani na 1:40 unaotakiwa kitaifa hali
inayodhihirisha upungufu wa walimu. Kwa upande wa shule zisizo za serikali wastani
wa mwalimu kwa wanafunzi ni 1:11-1:38 hali inayoonesha kutokuwa na tatizo la
walimu. Hata hivyo wastani wa uwiano wa mwalimu kwa idadi ya wanafunzi kitaifa
katika elimu ya sekondari unaonesha kuwa mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi
51 (BEST, 2010) hali ambayo inaonesha kuwepo kwa upungufu wa walimu hivyo
kuathiri ufundishaji na ujifunzaji.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
102
Kuhusu sifa za walimu, matokeo ya utafiti yameonesha kwamba, katika shule 132
zilizofanyiwa utafiti kuna jumla ya walimu 1,917 wakiwemo 515 wenye shahada,
1,051 wa stashahada, 126 wenye cheti na 225 wa leseni. Hali ya uwepo wa walimu
wenye cheti na wa leseni katika shule za sekondari zilizofanyiwa utafiti inaonesha
tofauti kati ya matamko ya Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) na hali halisi kuhusu sifa
ya mwalimu wa sekondari ambayo inasisitiza kwamba, mwalimu wa stashahada
afundishe kidato cha 1-2. Kwa kawaida mwalimu wa shahada anatazamiwa
kufundisha kidato cha 3-6.
Jedwali Na 4.4 Jumla ya Mahitaji, Walimu Waliopo na Upungufu katika
Shule za Sekondari 132 Zilizofanyiwa Utafiti
Mahitaji
Waliopo
katika orodha
Waliopo
Vituoni
Walio Nje kwa
Ruhusa
Wagonjwa
Muda Mrefu
Watoro wa
Muda Mrefu
Walioazimwa
Upungufu
Asilimia ya
upungufu
2903 1917 1556 67 48 229 17
1347 46.40
Asilimia 81.17 3.50 2.50 11.95 0.89
Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011
Pia utafiti umebaini kuwa, kuna tofauti ya takwimu za walimu waliopo katika orodha
shuleni na idadi halisi ya waliopo. Jedwali 4.4 linaonesha walimu waliopo vituoni
katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti ni asilimia 81.17 (1556) kati ya walimu 1,917
waliopo katika orodha shuleni. Aidha, asilimia 11.95 (229) ya walimu hao ni watoro
wa muda mrefu na asilimia 46.4% (1347) ni upungufu wa walimu katika shule hizo.
Uwepo wa walimu watoro kwa muda mrefu unaashiria tatizo la usimamizi wa rasilimali
watu na hivyo kukwamisha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji.
Utafiti umebaini kuwa uhaba wa walimu umesababisha baadhi ya Walimu kufundisha
masomo wasio na ujuzi nayo. Mfano katika shule za sekondari za Mipingo yenye jumla
ya walimu 2 na Mtanga yenye walimu 4 katika Halmashauri za Lindi na Kilwa wa
masomo ya lugha na sanaa pia wanalazimika kufundisha masomo ya sayansi.
Kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 katika shule
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
103
hizo ni wa kiwango cha chini, ambapo shule ya Mipingo watahiniwa wote 12 walifeli
na shule ya sekondari Mtanga alifaulu Mtahiniwa mmoja kati ya watahiniwa 37.
Hali hiyo pia imethibitika katika baadhi ya shule zenye kiwango kidogo cha ufaulu
zilizofanyiwa utafiti kama inavyoonekana katika Kielelezo Na. 4.11. Shule hizo zina
idadi ya walimu chini ya 5 kinyume na maelekezo yaliyo katika Kiongozi cha Mkuu wa
Shule na Waraka wa Elimu Na. 10 wa mwaka 2004.
Kielelezo Na 4.11: Baadhi ya Shule Zilizofanya Vibaya katika Mtihani wa
Kidato cha 4 Mwaka 2010 na Idadi ya Walimu Waliokuwepo katika Kila
Shule - 2010
Chanzo: Takwimu za utafiti 2011
Aidha, katika mahojiano na wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2010, mhitimu
mmoja alisema:
“tangu tulipoanza kidato cha kwanza mpaka cha nne, hatukuwahi
kuwaona walimu wa baadhi ya masomo darasani hata mara moja.”
Hali hii inaonesha kuwa baadhi ya shule zina upungufu mkubwa wa walimu hivyo
husababisha wanafunzi kufanya mitihani ya taifa katika baadhi ya masomo bila
kufundishwa.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
104
Utafiti umeonesha kuwa ni dhahiri kuwa upo uhusiano kati ya uwepo wa walimu na
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika Mitihani ya Taifa ya elimu ya sekondari.
Vielelezo Na 4.11 na 4.12 vinathibitisha mahusiano hayo, ambapo Kielelezo Na 4.11
kinaonesha baadhi ya shule za sekondari zilizofanyiwa utafiti ambazo zina ufaulu wa
kiwango cha chini wakati Kielelezo 4.4 kinaonesha shule zenye ufaulu wa juu.
Kielelezo Na 4.12: Baadhi ya Shule Zilizofanya Vizuri katika Mtihani wa
Kidato cha 4 Mwaka 2010 na Idadi ya Walimu Waliokuwepo katika Kila
Shule - 2010
Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011
Matokeo ya utafiti yameonesha kuna upungufu mkubwa wa walimu kimasomo
hususani katika masomo ya English Language, Chemistry, Physics na Mathematics.
Katika shule za sekondari 132 zilizofanyiwa utafiti, somo la Mathematics, lina
mahitaji ya walimu 436 ambapo waliopo ni walimu 172 hivyo kuna upungufu wa
walimu 264 sawa na asilimia 60.6 kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 4.5.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
105
Jedwali Na 4.5: Mahitaji, Uwepo na Upungufu wa Walimu Kimasomo katika Shule
za Sekondari Zilizofanyiwa Utafiti
MASOMO
Biology
Chemistry
Civics
English
Geography
History
Kiswahili
Mathematics
Physics
Jumla
Mahitaji 327 332 290 341 305 289 264 436 319 2903
Waliopo katika Orodha 210 183 203 234 255 228 202 219 183 1917
Waliopo Vituoni 175 153 178 182 185 189 172 172 150 1556
Walio Nje kwa Ruhusa 8 9 3 13 14 12 3 3 2 67
Watoro wa Muda Mrefu 23 17 13 27 47 19 18 39 26 229
Wagonjwa Muda Mrefu 2 3 9 7 9 7 8 1 2 48
Walioazimwa 2 1 0 5 0 1 1 4 3 17
Upungufu wa Walimu 152 179 112 159 120 100 92 264 169 1347
Asilimia ya Upungufu 46.5 53.9 38.6 46.6 39.3 34.6 34.8 60.6 53.0 46.4
Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011
Vilevile, upungufu huo wa walimu wa somo la Mathematics unathibitisha kiwango
kidogo cha ufaulu wa somo hilo kama inavyoonekana katika Kielezo Na. 4.13 ambapo
kiwango cha ufaulu kimeshuka kutoka asilimia 31.2 (2007) na kufikia asilimia 16.09
(2011).
Kielelezo Na 4.13: Ufaulu wa Somo la Mathematics katika Mtihani wa
Kidato cha 4 Mwaka 2006-2010
Chanzo: NECTA, Examinations Results Statistics 2007-2010
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
106
Upungufu wa walimu katika baadhi ya masomo hususan wa masomo ya sayansi na
Mathematics umesababisha ongezeko la idadi ya vipindi kwa walimu waliopo na
kupunguza ufanisi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji na hivyo kuathiri
kiwango cha ufaulu
Utafiti umebaini sababu za upungufu wa walimu ni pamoja na walimu kutokwenda
katika maeneo waliyopangiwa, kuruhusiwa kiholela au kutoroka kwenda kujiendeleza
kimasomo, hususan walimu wa stashahada na wa leseni na upanuzi wa elimu ya
sekondari ambao haukwenda sambamba na utayarishaji wa walimu wa kutosha kama
ilivyoeleza na walimu katika mahojiano ya pamoja.
Aidha, utafiti umebaini pia baadhi ya shule hazina wataalamu wa maabara, wakutubi,
wahasibu, maafisa ugavi, makatibu muktasi na wahudumu. Hali hii imesababisha
baadhi ya walimu kufanya kazi za uendeshaji zaidi kuliko kufundisha na hivyo kuathiri
ufaulu wa wanafunzi. Hivyo, kuna upungufu wa walimu na wafanyakazi wasio walimu
tofauti na ilivyoainishwa katika Kiongozi cha Mkuu wa Shule ukurasa 52 na 54
mtawalia.
Kwa ujumla matokeo ya utafiti yameonesha kuwepo kwa upungufu mkubwa wa
walimu hasa katika shule za serikali hali ambayo hailingani na kanuni ya ikama ya
walimu. Hali hii imesababisha walimu wasio na sifa kufundisha sekondari na hivyo
kuwanyima wanafunzi fursa ya kujifunza kikamilifu.
4.6.4. Maoni ya Kuimarisha Ubora na Uwepo wa Walimu
Wajibuji mbalimbali walitoa maoni ya kuimarisha ubora na uwepo wa walimu.
Mapendekezo hayo ni pamoja na:-
a. Uwepo wa Walimu
Uwepo mkakati maalum wa kuandaa walimu wa kutosha na wenye sifa hususan wa
masomo ya Sayansi na Mathematics na kuajiri wataalamu wa kusaidia uandaaji wa
masomo ya Sayansi kwa vitendo. Pia, ilishauriwa kuwa Halmashauri ziruhusiwe kuajiri
walimu hao ili kurahisisha mgawanyo mzuri wa walimu kulingana na mahitaji ya kila
somo. Suala la kuajiri walimu wenye sifa linahusisha vyuo vya ualimu na vyuo vikuu
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
107
hivyo kuna umuhimu wa kuwa na mkakati maalum wa kuandaa walimu wa kutosha na
wenye sifa katika ngazi zote. Pia ilipendekezwa kuwatumia Walimu na Maafisa wa Elimu
wastaafu katika shughuli mbalimbali za elimu ili kusaidia kupunguza athari za upungufu wa
wafanyakazi na kutumia uzoefu wao kujenga uwezo wa wafanyakazi kwa gharama nafuu
b. Kuimarisha Ubora wa Walimu
Kuhusu Mafunzo ya Walimu Kazini, ilipendekezwa kwamba Serikali iboreshe Vituo vya
Walimu (TRCs) ili vitumike kuendeleza walimu kwa gharama nafuu. Ilipendekezwa
kwamba Halmashauri zisaidie kusomesha walimu wanaopata nafasi ya kusoma elimu
ya juu. Aidha walimu wasiende masomoni kwa wakati mmoja na kusababisha
upungufu mkubwa shuleni. Maoni yalitolewa na wadau kuwa, CWT igharamie
mafunzo ya walimu kazini ili wajengewe uwezo wa mbinu za kufundishia na kujifunzia
zinazolenga kuimarisha ushirikishaji wa wanafunzi. Mafunzo hayo pia yatawajengea
ubunifu na ujuzi katika kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira wanayofanyia
kazi (ufaraguzi).
c. Kuboresha Utendaji Kazi wa Walimu
Ilipendekezwa kuwa walimu wasibakizwe kituo kimoja cha kazi kwa muda mrefu ili
kubadili mazingira na kuwa na uzoefu unaolingana kwa walimu wote. Pia, walimu
wanaobadilishana vituo vya kazi wapangwe katika shule walikotoka walimu hao ili
kuziba pengo na wanaokwenda kusoma warudishwe katika vituo vyao vya kazi baada
ya masomo. Ufuatiliaji ufanyike ili kubaini walimu ambao hawajaripoti vituo vya kazi
na ikama ipangwe kulingana na masomo ya walimu.
Aidha, Halmashauri ziweke utaratibu wa kuhudumia walimu wapya kabla ya kupata
mishahara yao. Maoni hayo yamebaini kuwa walimu hawaridhishwi na utaratibu wa
upangaji vituo vya kazi, mapokezi wakati wa kuanza kazi na kukaa katika kituo kimoja
cha kazi kwa muda mrefu. Hali kadhalika, ubadilishanaji wa vituo vya kazi usioziba
mapengo umeonesha kutowaridhisha. Ilishauriwa pia walimu wasio na uwezo, walevi
na watoro waondolewe na wasiruhusiwe kuajiriwa tena nchini. Vilevile wahitimu wa
chuo kikuu wajaze mkataba wa kufundisha muda fulani ili wasitoke vituoni na kwenda
kujiunga na kazi nyingine. Aidha, Serikali iunde Bodi ya Walimu Tanzania
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
108
itakayoshughulikia viwango vya taaluma, maadili na utendaji wa walimu kama
ilivyopendekezwa katika Mkakati wa Maendeleo ya Elimu ya Ualimu (TDMS, 2008).
d. Kuboresha Mafunzo ya Walimu Tarajali
Ilipendekezwa mafunzo ya walimu tarajali yasiwe chini ya miaka miwili na muda wa
kufanya mazoezi ya kufundisha BTP uwe miezi miwili kwa mwaka wa kwanza na miezi
mitatu kwa mwaka wa pili ili wanachuo waandaliwe ipasavyo. Aidha, kwa ufumbuzi
wa muda mfupi, kuwepo kwa programu ya miezi mitatu ya mafunzo ya walimu tarajali
ili kupata walimu wa kutosha na mfumo wa mafunzo ya ualimu unaojumuisha elimu
ya juu ya sekondari na ualimu urejeshwe ili kutoa walimu mahiri na wenye ari ya
ualimu. Vilevile, walionesha umuhimu wa kujifunza kutoka nchi nyingine zinazofanya
vizuri kielimu.
4.7. Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
Mazingira ya utendaji wa kazi ya walimu hutegemea mwamko wa jamii, uhusiano wa
walimu na ushirikiano na jamii inayozunguka shule. Miundombinu ya shule kama vile
maabara na madarasa, vifaa vya kufundishia na kujifunzia vikiwemo vitabu vya kiada
na ziada vinavyoendana na mitaala ni miongoni mwa mahitaji katika mazingira ya
kufundishia na kujifunzia.
4.6.1 Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia
Ubora wa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji unahitaji walimu na wanafunzi kuwa
katika hali inayorahisisha kazi na majukumu yao. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa
baadhi ya walimu hupigwa na wanakijiji, hubakwa na kufanyiwa vitendo vya
kishirikina. Pia, imebainishwa kuwa walimu hawapewi mapokezi mazuri na nyumba
bora za kuishi wanaporipoti katika vituo vyao vya kazi.
Pia utafiti umebaini kuwa asilimia 61 ya wakuu wa shule 132 za sekondari
zilizofanyiwa utafiti wamesema kuwa mazingira mazuri ya kazi ni fursa inayowafanya
walimu waendelee kubaki kwenye vituo vyao. Aidha, asilimia 57 (12) ya Maafisa elimu
sekondari wa Halmashauri waliohojiwa walieleza kuwa mazingira mazuri yenye
huduma za kijamii kama maji, afya, usafiri, umeme, teknolojia ya habari na
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
109
mawasiliano ni fursa inayowafanya walimu kuwepo shuleni. Pia, matokeo ya utafiti
yanaonesha kuwa kati ya maafisa 44 wa ofisi za TSD waliohojiwa, asilimia 55 (24)
walieleza kuwa baadhi ya walimu hupoteza muda wa vipindi kufuatilia stahili zao ofisi
za TSD wilaya na wakati mwingine kukata tamaa na kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Hali ambayo inayodhihirisha ugumu wa mazingira ya kazi ya mwalimu. Hivyo ili kuinua
kiwango cha ufaulu, mazingira vutivu yanapaswa kuandaliwa kwa walimu ili waweze
kutimiza wajibu wao katika vituo wanavyopangiwa.
Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa chakula cha mchana hakitolewi kwa wanafunzi
katika shule nyingi za kutwa. Pia, baadhi ya shule zimejengwa mbali na makazi ya
walimu na wanafunzi na hivyo kuleta matatizo ya usafiri wa wanafunzi na walimu
mijini na vijijini. Kufuatia shida ya usafiri, mwanafunzi mmoja katika mahojiano ya
pamoja alisema
”….huku hakuna mabasi tunapanda vitengo.”
Usemi huo ukiwa na maana malori ya mchanga au “landrover” za wazi kama
zinavyotumiwa na vitengo maalum vya polisi. Aidha, ukosefu wa mabweni
umesababisha wanafunzi kuishi katika nyumba za kupanga ‘geto’ kama
inavyofahamika na wanafunzi ambako huishi bila usimamizi wa wazazi au walimu.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, uwepo wa mazingira mazuri ya kazi ni motisha
inayoweza kuwafanya walimu kubaki katika vituo vyao na kutimiza majukumu yao
kikamilifu. Pia, baadhi ya walimu wanatumia muda mwingi katika kufuatilia stahili zao
badala ya kuwa kazini. Kwa ujumla, hali hii husababisha walimu kukata tamaa na
kukosa morali ya kufundisha.
Pia, utafiti umeonesha kuwa fedha za ruzuku ya uendeshaji (Capitation Grant)
ambazo shule hununulia vifaa vya kufundishia na kujifunzia hutolewa chini ya kiwango
kinachotakiwa. Vile vile, fedha hizi huchelewa kutolewa toka Hazina hali ambayo
huathiri mwenendo wa manunuzi ya vifaa.
Kukosekana kwa mazingira mazuri ya kazi husababisha walimu kukata tamaa na
kukosa morali ya kufundisha. Vile vile, kutokuwepo kwa chakula cha mchana kwa
wanafunzi katika shule za kutwa, kunaathiri umakini wa wanafunzi katika ujifunzaji.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
110
Aidha, ni ukweli ulio dhahiri kuwa matatizo ya usafiri wa wanafunzi mijini na vijijini
yanawakosesha vipindi kila siku na hivyo kuchangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu.
Pia kutokutolewa fedha za kutosha kwa wakati kwa ajili ya kununulia vifaa vya
kufundishia na kujifunzia kunaathari katika mchakato wa utoaji wa elimu kufikia
malengo yaliyowekwa.
4.6.2.2 Uwepo wa Samani na Majengo katika Shule
Miongoni mwa miundombinu muhimu katika utoaji wa elimu kwa ufanisi ni pamoja na
madarasa, maabara, samani, mabweni/hosteli, nyumba za walimu, majengo ya
utawala na viwanja vya michezo. Takwimu zilizotolewa na wakuu wa shule 132
zilizofanyiwa utafiti zimeonesha kuwa upo upungufu mkubwa wa maabara kwa masomo ya
sayansi, maktaba, samani na miundombinu mingine kama inavyoainishwa kwenye Jedwali Na
4.6 na Kielelezo 4.6.1
Jedwali 4.6: Samani na Majengo Katika Shule za Sekondari 132
Miundombinu Mahitaji Uwepo Upungufu % Upungufu
Samani(Viti na Meza) 63,601 48,665 14,936 23.5
Hosteli/Bweni 1,900 840 1,060 55.8
Nyumba 3,150 881 2,269 72
Majengo Utawala 1,138 516 622 54.7
Madarasa 2,866 1,535 1,331 46.4
Maktaba 1,183 230 953 80.6
Maabara Kemia 1,128 229 898 79.6
Maabara Fizikia 1,099 383 716 65.2
Maabara Bayolojia 1,123 382 741 66
Kielelezo Na. 4.9: Asilimia ya Upungufu wa Miundombinu katika Shule
Zilizofanyiwa Utafiti
Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
111
Aidha, walimu katika hojaji walibainisha kuwepo kwa mlundikano wa wanafunzi katika
vyumba vya madarasa, maktaba na maabara hali inayothibitisha upungufu wa
miundombinu hivyo kuathiri ufundishaji na ujifunzaji. Vilevile, wanafunzi katika
mahojiano ya pamoja walibainisha athari ya ukosefu wa hosteli/mabweni shuleni
hupelekea wanafunzi kulazimika kutembea umbali mrefu kati ya shule na makazi yao.
Matokeo haya kwa ujumla yanaonesha hali isiyoridhisha katika suala la miundombinu
ya shule tofauti na ilivyoelekezwa na Sera ya Elimu na Mafunzo, 1995 na Mwongozo
wa Samani wa Wizara ya Elimu (2001).
4.6.2.3 Uwepo wa Vitabu vya Kiada na Ziada
Utafiti umebaini kuwa kuna upungufu wa vitabu vya kiada vinavyoendana na mtaala
ulioboreshwa kama inavyooneshwa katika Kielelezo Na 4.10. Aidha, utekelezaji wa Sera ya
upatikanaji na usambazaji wa vitabu ya Mwaka 1992 imekuwa na changamoto ingawa
serikali imeendelea kukasimu majukumu ya kununua vitabu shuleni.
Kielelezo Na. 4.10: Asilimia ya Upungufu wa Vitabu katika Shule
Zilizofanyiwa Utafiti
Chanzo: Data za Utafiti, 2011
Kielelezo Na. 4.10 kinaonesha kuwa upungufu wa vitabu vya kiada na ziada kwa
wastani wa asilimia 75.5 kwa shule zote zilizofanyiwa utafiti. Aidha, wajibuji
walionesha kuwa ununuzi wa vitabu huathiriwa na wanafunzi kutolipa ada na bei
kubwa ya vitabu.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
112
Wakuza mitaala waliohojiwa walieleza changamoto za ucheleweshaji wa uhakiki wa
vitabu na utoaji ithibati inayofanywa na Kamati ya kuhakiki ubora wa machapisho ya
kielimu (EMAC). Walimu wakuu walitoa changamoto ya upungufu wa vifaa vya
kufundishia pamoja na vitabu vya kiada vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa
kwa baadhi ya masomo, na kuwepo baadhi ya mada katika vitabu vya kiada
vilivyopewa ithibati na EMAC kutoendana na mahitaji ya mihtasari iliyoboreshwa.
Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa pamoja na shule nyingi kuwa na vitabu vichache,
baadhi ya vitabu hivyo haviendani na mtaala ulioboreshwa. Aidha, kukosekana kwa
mamlaka rasmi ya kusambaza vitabu katika ngazi ya Halmashauri pia ilibainishwa
kuwa chanzo cha ukosefu wa vitabu vinavyoendana na mtaala. Pia, mahojiano ya
pamoja ya wanafunzi na walimu yameonesha kuwa shule nyingi hazina utaratibu
mzuri wa matumizi ya vitabu hata vile vichache vilivyopo. Kwa ujumla, utafiti
unaonesha upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada katika shule nchini na
matatizo katika upatikanaji, usambazaji na matumizi yake katika shule. Hali hii ina
athari kubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa taaluma shuleni.
4.6.3 Maoni ya Kuboresha Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia
Kati ya wakuu wa shule 132 wa shule za sekondari waliohojiwa, asilimia 61
wameeleza kuwa mazingira mazuri ya kazi ni fursa inayowafanya walimu waendelee
kubaki kwenye vituo vyao. Aidha, asilimia 57 (12) ya Maafisaelimu sekondari wa
Halmashauri waliohojiwa wameeleza kuwa mazingira mazuri yenye huduma za kijamii
kama maji, afya, usafiri, umeme, teknolojia ya habari na mawasiliano ni fursa
inayowafanya walimu kuwepo shuleni. Uwepo wa mazingira mazuri ya kazi kwa
walimu ni motisha itakayowafanya walimu kubaki katika vituo vyao na kutimiza
majukumu yao ya kufundisha kwa ukamilifu.
Wajibuji wamependekeza kuwepo na vitabu vya kutosha shuleni ambavyo
vimeidhinishwa na utaratibu wa kupitia vitabu. Aidha, Kitengo cha Kamati ya
Kutathimini Machapisho ya Kielimu (EMAC) kiimarishwe ili kiwe na watendaji wenye
ujuzi. Serikali irudishe utaratibu wa kuwa na aina moja ya vitabu vya kiada
vitakavyotumika nchi nzima kwa kila somo (visiwe zaidi ya viwili). Wizara inunue na
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
113
kusambaza vitabu hivyo ili kuwezesha kuwepo kwa vitabu vya kutosha shuleni. Hali
kadhalika, matumizi ya TEHAMA shuleni yatiliwe mkazo ili kuwezesha wanafunzi
kupata maarifa kwa njia ya mtandao. Vilevile, imeshauriwa kuwa Serikali ithibiti
matumizi holela ya vitabu vya kugushi vya kufundishia na kujifunzia shuleni. Pia vifaa
vya maabara viongezwe katika kila shule na shule zilizo na maabara ziwezeshwe ili
shule za karibu zisizo na maabara zitumie maabara za shule hizo teule.
Kuhusu posho kwa walimu, ilipendekezwa kuwepo na posho maalum ya kufundishia
ambayo ni asilimia 50 ya mshahara, posho ya mazingira magumu, kupandishwa
madaraja, mafunzo kazini, kuboresha huduma za jamii kama vile umeme, maji,
usafiri na nyumba bora ili kutoa motisha kwa walimu. Vilevile serikali ianzishe mfuko
wa kuwakopesha walimu ili kuwavutia wadumu kufundisha katika mazingira magumu.
Serikali ilishauriwa kuhamasisha wadau mbalimbali wa elimu kuimarisha miundombinu
shuleni kwa kuziwezesha shule kuwa na maktaba, maabara na vifaa vyake ili mitihani
ya “alternative to practical” iondolewe, kuwepo kwa mabweni na vyumba vya kutosha
hasa kwenye shule zilizojengwa kwenye mazingira magumu. Pia, ilipendekezwa kuwa
shule zijengewe uzio ili kuimarisha ulinzi. Sambamba na hilo wadau walipendekeza
kuwe na utaratibu wa kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wa shule za kutwa
ili wanafunzi hao waweze kujifunza kwa ufanisi zaidi.
Aidha, ilipendekezwa kuwe na ziara za mafunzo na kuimarisha vyama vya kimasomo
ili kuwajengea wanafunzi na walimu utamaduni wa kusoma vitabu ili kuwapatia na
uwezo wa kujitafutia maarifa wenyewe kwa mfumo wa kujitegemea.
Kutokana na maoni hayo imeonekana kuna upungufu wa vifaa vya kufundishia na
kujifunzia, miundombinu ya kutosha, ziara za mafunzo na vyama vya masomo. Aidha,
ukosefu wa fedha, ubovu wa miundombinu, uchapaji na usambazaji mbaya wa vitabu
vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa, na uelewa mdogo wa lugha ya Kiingereza
kwa walimu na wanafunzi, ni changamoto ambazo zinaathiri utekelezaji wa mitaala
shuleni.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
114
Pamoja na juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia
kama ilivyobainishwa katika MMES I na II, bado kuna changamoto za uwepo wa vifaa
vya kutosha. Aidha, zinahitajika juhudi za makusudi kuhamasisha wanafunzi
kupenda masomo ya Sayansi na Mathematics kwa kuhakikisha kuwepo kwa vifaa
toshelevu vya kufundishia na kujifunzia kwa sababu Taifa linahitaji wataalam ili
kuhimili ushindani wa kisayansi na kiteknolojia.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
115
SURA YA TANO: HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
Sura hii inaainisha hitimisho la matokeo ya utafiti kwa kuzingatia masuala
yanayoendana na malengo mahsusi na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu
yameonesha sababu mbalimbali za kushuka kwa ufaulu zilizobainishwa na kujadiliwa
katika sura ya nne. Sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu zimegawanyika katika
sehemu mbili ambazo ni chanzo (cause) cha tatizo na athari (effects). Matokeo ya
utafiti yameonesha kuwa usimamizi na uendeshaji wa elimu katika ngazi zote ni
chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4
mwaka 2010. Usimamizi na uendeshaji wenye mapungufu umeathiri utayarishaji na
utekelezaji wa mitaala, mfumo wa utayarishaji na uwepo wa walimu, mfumo na
taratibu za mitihani ya taifa, mazingira na vifaa vya kufundishia na kujifunzia na
mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu.
Aidha, mapendekezo yamewasilishwa kwa kila suala na kubainishwa kwa kuzingatia
muda wa utekelezaji ambao ni mfupi, wa kati na mrefu. Muda mfupi (MF) ni kipindi
chini ya mwaka mmoja, muda wa kati (MK) ni mwaka mmoja hadi mitatu na muda
mrefu (MR) ni zaidi ya miaka mitatu.
5.1. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu
i) Baadhi ya viongozi wa elimu katika ngazi mbalimbali wanateuliwa bila kuzingatia
vigezo vya utaalamu, uzoefu na uadilifu. Hali hii imepelekea kuwa na usimamizi na
uendeshaji usioridhisha na kuwepo na uwajibikaji mdogo katika ngazi mbalimbali
za kielimu;
ii) Maamuzi ya kitaalamu yahusuyo elimu pamoja na uendeshaji wake hufanyika
kisiasa na hivyo kuleta athari katika utekelezaji wa mipango ya utoaji wa elimu
bora nchini;
iii) Kuna ufinyu wa bajeti ya Wizara ya Elimu, TAMISEMI na Halmashauri, hivyo
usimamiaji na uendeshaji wa elimu kutokuwa na ufanisi unaotakiwa kulingana na
malengo ya elimu;
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
116
iv) Utekelezaji wa Sera ya matumizi ya vitabu vingi vya kiada hauendani na
upatikanaji wa vitabu vyenye ithibati na hivyo kusababisha kuwepo kwa vitabu vya
kughushi na kupenyezwa kwa vitabu visivyo na ubora; na
v) Kuna matatizo makubwa katika matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia
na kujifunzia katika elimu ya sekondari, na hivyo kuathiri ufundishaji na ujifunzaji.
vi) Kutokuwepo kwa uadilifu katika usimamizi na matumizi ya fedha zilizotengwa licha
ya ufinyu wa bajeti hali inayokwamisha kufikia malengo ya utoaji wa elimu bora;
na
vii) Kumekuwepo na ongezeko kubwa la wahitimu waliofeli katika mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4, hivyo kuwanyima fursa ya kuendelea na masomo ya juu na fani
mbalimbali.
Mapendekezo
a) Uendeshaji, usimamizi, mawasiliano na mahusiano baina ya asasi za kielimu,
Taasisi, ofisi za elimu mikoa, Halmashauri, na mashirika yasiyo ya kiserikali
uimarishwe katika utoaji wa elimu kwa ngazi zote; (MF)
b) Uadilifu katika usimamizi na matumizi ya fedha zilizotengwa uimarishwe; (MF)
c) Mchakato wa kutoa ithibati ufanyike kwa ukamilifu ili kupata vitabu vyenye ubora
unaotakiwa; (MF)
d) Ufuatialiaji wa usambazaji, upatikaji na utumiaji wa vitabu vya kiada na ziada
pamoja na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia uimarishwe; (MF)
e) Ufundishaji na ujifunzaji wa somo la English kwa shule za Awali, Msingi na
Sekondari uimarishwe; (MF)
f) Uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kielimu uzingatie uzoefu, utaalamu, uwezo,
uadilifu na uwajibikaji. Aidha, nafasi za uongozi zilizoachwa wazi zijazwe na
zisikaimishwe kwa muda mrefu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu;
(MK)
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
117
g) Klabu za masomo kama vile “English, Mathematics, Science na Geography clubs”
vianzishwe na kuimarishwa; (MF)
h) Mfumo wa kuandaa viongozi katika kuachiana madaraka (succession plan)
uanzishwe/kuimarishwa na kutumika; (MK)
i) Maamuzi yanayohusu masuala ya elimu yafanywe kwa kuzingatia utaalam,
tathmini na tafiti za kisayansi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya
utoaji wa elimu; (MF)
j) Bajeti ya elimu iongezwe na izingatie vipaumbele katika sekta ya elimu ili kutatua
changamoto zilizopo; (MK)
k) Chombo cha Kusimamia Taaluma ya Ualimu (Teachers Professional Board)
kianzishwe kwa lengo la kushughulikia viwango vya taaluma, maadili, utendaji na
haki za walimu ili kulinda hadhi ya kazi ya ualimu na kuhakikisha kuwa inakidhi
malengo yaliyokusudiwa; (MK)
l) Utaratibu wa motisha kwa walimu unaoendana na uzito wa kazi, wadhifa na
ugumu wa mazingira anapofanyia kazi uandaliwe na utekelezwe ipasavyo; (MK)
m) Wanafunzi wanaofeli katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 wahimizwe kufanya
mitihani ya marudio kama watahiniwa binafsi ili wapate sifa za kujiendeleza
kitaaluma na kitaalamu; (MK)
n) Programu maalumu ya mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa walimu wa masomo
yote ianzishwe na itekelezwe katika shule zote za sekondari; (MK) na
o) Sheria ya vitabu itungwe ili kudhibiti usambazaji na matumizi ya vitabu visivyo na
ithibati katika shule nchini. (MR) na
p) Vyuo vya ufundi stadi kama vile VETA, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC),
Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (CDTI) vipanuliwe ili kuwawezesha wanafunzi
wanaopenda kujiunga na vyuo hivyo kujiunga na kupata ujuzi na stadi za
kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri. (MR)
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
118
5.2. Utekelezaji wa mitaala
i) Mafunzo kabilishi juu ya mtaala ulioboreshwa mwaka 2005 na 2007 ambao
unazingatia ujuzi yametolewa kwa kiwango kidogo kwa walimu, wakaguzi na
Maafisa Mitihani na hivyo kutotekeleza mtaala ipasavyo;
ii) Dhana ya mtaala unaozingatia ujuzi (competence Based Curriculum) haieleweki
kwa wadau wengi wakiwemo maafisa mitaala, maafisa mitihani, wakaguzi wa
shule na walimu;
iii) Upungufu wa mihtasari ya masomo na vitabu vya kiada na ziada vinavyoendana
na mtaala ulioboreshwa katika shule na vyuo vya ualimu umeathiri mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji;
iv) Mitaala inatayarishwa bila kufanyiwa majaribio (piloting). Kutojaribisha mitaala
wakati wa utayarishaji wake kunasababisha kutekeleza mitaala yenye mapungufu
na isiyokidhi mahitaji ya jamii; na
v) Kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa mihtasari kutoka TET kwenda shuleni,
aidha TET huuza mihtasari na kusababisha upungufu shuleni.
Mapendekezo
a) Mafunzo maalumu kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na
kutekelezwa kwa maafisa mitaala na maafisa mitihani ili kuwajengea uwezo; (MF)
b) Mafunzo kabilishi kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na
kutekelezwa kwa walimu na wakaguzi wote; (MF)
c) Mihtasari ya kutosha isambazwe shuleni na isiuzwe. Aidha nakala laini (soft copy)
ya mihtasari iwekwe kwenye mtandao (website) ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi na TET ili wadau waweze kuipata kiurahisi; (MF)
d) Ithibati ya vitabu vyenye kukidhi mahitaji ya mtaala iharakishwe. Aidha mafunzo
elekezi yatolewe kwa waandishi na wachapishaji ili wachapishe vitabu
vinavyoendana na mtaala ulioboreshwa; (MK) na
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
119
e) Taratibu za utayarishaji wa mitaala zizingatiwe ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti,
tathmini na kujaribisha mitaala kabla ya utekelezaji wake. (MR)
5.3. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa
i) Muundo na aina ya maswali yanayotolewa na walimu katika ngazi ya shule kwa
kiasi kikubwa haufanani na ule wa mitihani ya Taifa. Hivyo upimaji wa wanafunzi
shuleni kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa katika mitihani ya Taifa;
ii) Wanafunzi wana uelewa mdogo wa lugha ya kufundishia (Kiingereza) na hivyo
kushindwa kujibu maswali ya mitihani ipasavyo;
iii) Kuna mianya ya uvujaji wa mitihani unaotokana na kutokuwa na vyumba vya
kuhifadhia mitihani (strong room) katika ngazi ya Halmashauri na shule;
iv) Uteuzi wa wasahihishaji unafanyika kwa upendeleo na hivyo kupoteza umakini
katika usahihishaji;
v) Wasahihishaji wa mitihani ya Taifa hulipwa kwa kiwango kidogo cha pesa na
kufanya kazi kwa muda mrefu kwa siku, na hivyo kushusha ari na kupoteza
umakini katika usahihishaji;
vi) Miongozo ya usahihishaji (marking scheme) ya baadhi ya masomo yenye
mapungufu na makosa katika baadhi ya maswali hutumika wakati wa usahihishaji
wa mitihani ya taifa, hivyo kuwanyima haki watahiniwa;
vii) Muundo wa mitihani (Format) kutowafikia baadhi ya walimu na hivyo kutopata
fursa ya kuutumia katika kuwaandaa wanafunzi;
viii) Mwongozo kuhusu mchango wa CA wa 50% (45% majaribio na mazoezi na 5%
projekti) katika mtihani wa Taifa hautumiki au mchakato wake katika matokeo ya
mwisho haufahamiki kwa wadau wa elimu. Hii inatoa matokeo ambayo siyo
halisia, pia ni kinyume na mwongozo wa mazoezi endelezi (CA) wa NECTA;
ix) Baadhi ya shule huwasilisha NECTA alama za CA zisizo na uhalisia na hivyo
kusababisha NECTA kukosa imani na alama hizo;
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
120
x) Ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 una athari katika ufaulu wa Mtihani
wa Taifa wa Kidato cha 4;
xi) Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 ni sehemu ya mazoezi endelezi (CA) na
hautumiki kuchuja wanafunzi kuendelea na Kidato cha 3. Hali hii imepunguza ari
ya ufundishaji na ujifunzaji;
xii) Utoaji wa adhabu ya kumshusha mtahiniwa daraja kutokana na kufeli kwa baadhi
ya masomo ya msingi na ya mchepuo hakuleti usawa katika ufaulu pia ni kinyume
na alama za madaraja husika; na
xiii) Kuna tofauti ya taratibu zinazotumika kupata gredi katika mitihani ya Taifa na
zile zinazotumika kupata gredi hizo katika mitihani ya shule. Hali hii inasababisha
watahiniwa kutopata gredi stahiki, hivyo kuathiri ufaulu.
Mapendekezo
a) Walimu wawapime wanafunzi kwa kuwapa mazoezi endelezi (CA) yenye uhalisia
(authentic) pia alama za CA zitumike katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4
kama ilivyoelekezwa katika mwongozo wa mazoezi endelezi; (MF)
b) Uteuzi wa wasahihishaji uzingatie sifa na usawa kutoka shule za kitaifa, jamii na
zisizo za serikali; (MF)
c) Utungaji na uhakiki wa mitihani ya taifa uboreshwe na uzingatie mitaala
inayotekelezwa; (MF)
d) Adhabu katika upangaji wa madaraja inayomshusha mtahiniwa hadi daraja la III
baada ya kufeli mojawapo ya masomo ya msingi au mchepuo iondolewe ili kila
mtahiniwa apate daraja linalolingana na kiwango cha ufaulu wake; (MF)
e) Fomati ya mitihani ya Taifa isambazwe katika shule zote na ufuatiliaji ufanyike
kuhakikisha kwamba kila mwalimu anaitumia; (MF)
f) Utaratibu wa kuweka kwenye mtandao (website) taarifa muhimu zinazohusu
taratibu na maelekezo mbalimbali ya uendeshaji wa mitihani ya Taifa na utoaji
matokeo uimarishwe. Kwa mfano ziwekwe fomati za mitihani, ripoti za tathmini za
mitihani, taratibu za mitihani; (MF)
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
121
g) Hadhi ya Mtihani wa taifa wa Kidato cha 2 irudishwe ili utumike kuchuja
wanafunzi. Aidha, wanafunzi wasiokuwa na uwezo wapatiwe masomo ya ziada
(Remedial); (MF)
h) Mfumo rasmi wa kupata gredi katika mitihani ya shule na Taifa unaofahamika
kwa wadau wote wa elimu utayarishwe na kutumika kikamilifu ili kuleta haki kwa
watahiniwa; (MF) na
i) Wasahihishaji wa mitihani ya taifa walipwe posho ya kujikimu (perdiem) kwa
sababu ni haki ya mwajiriwa wa serikali. (MK)
5.4. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu
i) Mfumo wa ukaguzi wa shule za sekondari kuwa katika ya ngazi ya kanda hauleti
ufanisi katika ufuatiliaji na tathmini ya elimu; na
ii) Ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mtaala umefanyika kwa kiwango kidogo
hivyo kutobainika kwa dosari za utekelezaji wake;
Mapendekezo
a) Ukaguzi wa shule, utafiti wa elimu, ufuatiliaji na tathmini uimarishwe kwa kupatiwa
nyenzo na wataalamu wa kutosha ili kutoa maamuzi yenye uhalisia; (MF)
b) Viongozi wa elimu wafanye ziara za mara kwa mara na za kushtukiza shuleni ili
kufuatilia uendeshaji wa elimu; (MF)
c) Jukumu la kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mtaala litekeleze kikamilifu ili
kubaini dosari za kiutekelezaji na hivyo kufanya marekebisho stahiki; (MF) na
d) Ukaguzi wa shule ngazi ya elimu ya sekondari uwe katika ngazi ya Mkoa na
Halmashauri ili kusogeza huduma karibu na walengwa na kuimarisha usimamizi na
uendeshaji; (MK)
5.5. Mfumo wa utayarishaji wa walimu
i) Sifa za udahili wa mwalimu tarajali anayeandaliwa kufundisha elimu ya sekondari
ngazi ya stashahada (1 Principal, and 1 Subsidiary passes) hazitoshelezi kumfanya
mwalimu anayeandaliwa kuwa mahiri;
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
122
ii) Baadhi ya wadahiliwa katika vyuo vya ualimu kutokuwa na wito wa kazi ya ualimu
hivyo kusababisha walimu hao kutokuwa na maadili ya kazi ya ualimu na
kutodumu katika ajira;
iii) Matayarisho hafifu ya walimu tarajali yanatokana na wingi wa wanachuo darasani,
upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kutotumika
kwa mbinu shirikishi. Hali hii inasababisha kutopata walimu mahiri wa kutekeleza
mtaala ulioboreshwa;
iv) Baadhi ya wanachuo wanaomaliza shahada ya elimu huajiriwa kuwa wakufunzi
katika vyuo vya ualimu moja kwa moja, utaratibu ambao unawafanya wanachuo
watayarishwe na wakufunzi wasio na uzoefu wa kufundisha; na
v) Wanachuo wengi wana tatizo la kutumia lugha ya kiingereza katika kuandika na
kujieleza, hivyo wanapohitimu hushindwa kutumia lugha hiyo katika kufundisha
katika shule za sekondari.
i) Kuna upungufu mkubwa wa walimu pamoja na usambazaji wa walimu usiofuata
uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi kati ya shule na shule, mijini na vijijini. Hali hii
inasababisha wanafunzi kutofundishwa ipasavyo;
ii) Kuna walimu wasio na sifa kufundisha sekondari ambao wapo katika shule za
sekondari wakifundisha bila utaalamu wa ualimu;
iii) Kuna upungufu mkubwa wa walimu unaosababishwa na walimu wa shule moja
kwenda masomoni kwa wakati mmoja hususan wa leseni, na hivyo kuathiri
ufundishaji na ujifunzaji shuleni; na
vi) Baadhi ya shule huwatumia wahitimu wa kidato cha 6 na 4 na wasiokuwa na
taaluma na maadili ya ualimu. Hii inasababisha wanafunzi kutopata fursa ya elimu
na malezi bora.
Mapendekezo
a) Walimu wasambazwe kwa usawa kwa kuzingatia mahitaji (ikama) katika shule
zote; (MF)
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
123
b) Programu za mafunzo zisizoathiri ikama ya walimu katika kila shule ziandaliwe;
(MF)
c) Uanzishwe utaratibu wa kuwatumia walimu kufundisha shule zaidi ya moja kwa
masomo yenye ukosefu au upungufu wa walimu; (MF)
d) Sifa za udahili wa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada
zipandishwe kuwa Principal 2 za masomo atakayofundisha, ili kumwezesha
mwalimu kuwa mahiri kitaaluma; (MK)
e) Vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha vipatikane na upanuzi wa
miundombinu ufanyike katika vyuo vya ualimu na vyuo vikuu ili kuendana na
ongezo la udahili na kufikia viwango vilivyowekwa; (MK)
f) Wakufunzi na wahadhiri wapewe mafunzo kazini juu ya mtaala unaozingatia ujuzi
(Competence Based Curriculum) ; (MK)
g) Wakufunzi mahiri na wenye uzoefu wa kufundisha katika shule za sekondari
waajiriwe. Aidha wahitimu wa vyuo vikuu wanaoajiriwa moja kwa moja waanzie
kazi katika shule za sekondari za mazoezi; (MK)
h) Uhamasishaji ufanyike kwa wahitimu wa kidato cha 6 na vyuo vikuu kuelewa fursa
za kazi ya ualimu ili waweze kuijiunga na kuifanya kazi hiyo; (MK)
i) Maabara ya lugha ya kiingereza (language laboratory) zianzishwe na kuimarishwa
katika Vyuo vya ualimu na Vyuo vikuu ambapo walimu tarajali watatumia
kujifunzia lugha ya kiingereza ili kuongeza stadi za kuongea na kuandika; (MR)
j) Udahili wa walimu tarajali uzingatie mahitaji ya walimu kimasomo ili kukabiliana na
upungufu walimu katika baadhi ya masomo; (MK)
k) Udahili wa walimu tarajali ngazi ya stashahada ufanyike kwa wahitimu wa Kidato
cha 4 waliojaza “Sel Form” na mafunzo yawe miaka mitatu yakijumuisha masomo
ya taaluma (Kidato cha 5-6) na ualimu ili kupata walimu mahiri na wenye wito;
(MK)
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
124
l) Utaratibu maalumu uanzishwe kwa kuwapatia mafunzo ya Ualimu (Post Graduate
Diploma in Education) wahitimu wa shahada zisizo za ualimu ili kukabiliana na
tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mfupi; (MK)
m) Utaratibu wa kutumia/kuajiri watu ambao sio walimu kufundishaji katika shule za
sekondari uachwe; (MK)
n) Utaratibu uandaliwe wa kuwaendeleza walimu wanaofundisha katika shule za
sekondari ambao hawana utaalam wa ualimu ili kuwajengea uwezo walimu hao;
(MK)
o) Utaratibu uanzishwe wa kuwatumia Walimu na Maafisa wa Elimu wastaafu ili kutumia
uzoefu wao katika kufanikisha shughuli mbalimbali za elimu; (MK)
p) Wahitimu wa kidato cha 6, 4 na vyuo vikuu wanaofundisha katika shule za
sekondari wajiendeleze kwa kusomea taaluma ya ualimu; (MK) na
q) Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji yaimarishwe. (MK)
5.6. Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia
i) Kuna upungufu mkubwa wa samani na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.
Hali hii inasababisha wanafunzi kutoshiriki kikamilifu katika mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji;
ii) Baadhi ya shule zimepata usajili bila kutimiza vigezo vinavyohitajika kama vile
maabara za Sayansi, maktaba, ofisi na nyumba za walimu na hivyo shule hizo
kuendeshwa kwa mapungufu;
iii) Baadhi ya shule zimejengwa mbali na makazi ya wanafunzi na walimu. Hali hii
inawasababisha walimu na wanafunzi kutumia muda mrefu wa kwenda na kurudi
shuleni na hivyo kupunguza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji; na
iv) Kutokuwepo kwa chakula cha mchana katika shule za kutwa, hivyo kuathiri
mahudhurio na umakini wa wanafunzi katika ujifunzaji.
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
125
Mapendekezo
j) Jamii na wadau wengine wa elimu wahamasishwe kugharamia elimu nchini; (MF)
k) Usajili wa vyuo na shule za Serikali na zisizo za Serikali uzingatie vigezo
vinavyotakiwa; (MF)
l) Fedha za kutosha kwa ajili ya kununua samani na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia shuleni zitengwe na kutumika ipasavyo; (MK)
m) Utaratibu wa usafiri wa wanafunzi na walimu kwenda na kurudi shuleni uandaliwe
kwa shule ambazo ziko mbali na makazi ya walimu na wanafunzi; (MK)
n) Hosteli/mabweni na nyumba za walimu zijengwe kwenye shule zilizo mbali na
makazi ya wanafunzi na ya walimu; (MR) na
o) Wanafunzi katika shule zote za kutwa wapatiwe chakula cha mchana ili kuimarisha
ufundishaji na ujifunzaji. (MR)
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
126
REJEA
1.0 Lissu H. S (2008). Public Perception On The Use Of Continuous Assessment
Marks In Grading O-Level Secondary, M.Ed. (Science Education) Dissertation
(Unpublished), Faculty of Education, University of Dar es Salaam.
2.0 Natinal Examinations Council of Tanzania: Examinations Processing, Dar
es Salaam, July, 1986
3.0 National Examinations Council of Tanzania: NECTA WEBSITE, Dar es
Salaam, May 2001
4.0 National Examinations Council of Tanzania: The Examinations
Regulations, Dar es Salaam, 2006.
5.0 NECTA, 2004. Thirty Years of National Examinations Council of Tanzania
(1973-2003). Dar es Salaam.
6.0 National Examinations Council of Tanzania: Certificate of Secondary
Eeducation Examination, Paper on Literature in English, Dar es Salaam,
Oktober, 2010
7.0 National Examinations Council of Tanzania: Certificate of secondary
Education Examination Format, Dar es Salaam, February, 2008
8.0 National Examinations Counci of Tanzania: Guidelines on the Conduct
and Administration of Continuous assessment in Secondary Schools and
teacher Training Colleges, Dar es Salaam,
9.0 United Republic of Tanzania: Education and Traininng Poplicy, Ministry of
Education, Dar es Salaam, 1995.
10.0 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi: Waraka wa Elimu Na. 1 wa
Mwaka 2006, WEMU, 2006
11.0 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi: Waraka wa Elimu Na. 5 wa
Mwaka 1999, Mtihani wa kidato cha Pili katika Shule za Sekondari, WEMU,
1999.
12.0 Babyegeya E (2006) Teacher Education in Tanzania: developments and
prospects, Journal of Issues and practice in Education (pg.32-46).
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
127
13.0 TIE (1991) A Summary Report on baseline Survey on primary, secondary and
Teacher Education Curriculum Reform in Tanzania Mainland, MOEVT, Dsm.
14.0 Meena W.E. (2009) Curriculum Innovation in Teacher Education. Abo
Academy University Press.
15.0 Osaki K.M. (1996) “Changing Forms of Curriculum in Tanzania” in Papers in
Education and Development No. 17, DSM.
16.0 IBE/UNESCO (Dec 2000) Capacity Building for Curriculum Specialists in East
& South East Asia and The Pacific, Bangkok, Thailand.
17.0 WEU (1995) Sera ya Elimu na Mafunzo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dar es Salaam.
18.0 TIE (2003) National Curriculum Development Framework (NCDF), TIE,
Dar es Salaam.
19.0 TIE, (2008) Secondary Education Curriculum for Tanzania Mainland. Dar es Salaam.
20.0 TET ( Februari 2011) Taarifa ya Utekelezaji wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa
Elimu na Walimu kwa miaka 2005-2010, TET Dar es Salaam.
21.0 WEU (Juni 2005) Marekebisho ya Mtaala wa sekondari na Kuunganishwa kwa
Masomo, Wizara ya Elimu na Utamaduni, Dar es Salaam.
22.0 MOEVT (2007) Teacher Development Management Strategy (TDMS), Ministry
of Education & Vocational Training, Dar es Salaam.
23.0 MoEVT (2001) Practices and Possibilities in Teacher Education in Tanzania,
edited by Mhando et al., Ministry of Education and Vocational Training , Dsm
24.0 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Februari 1982), Mfumo wa Elimu ya
Tanzania 1981-2000:Ripoti na Mapendekezo ya Tume ya Rais ya Elimu, Juzuu
la Kwanza, JMT, Dsm.
25.0 MoEVT (May 2004) A Deliberate Support to Licensed Teachers-Facilitator and
Mentor’s Guide, Ministry of Education and Vocational Training, Dsm
26.0 WEMU (2006), Kiongozi cha Mkaguzi wa shule. Dar es Salaam
27.0 WEMU (2009), Hotuba ya bajeti ya WEMU 2009/2010 p.43). Dar es Salaam
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
128
28.0 Ngodu, A. S . (2007), Licensed Teachers’ Professional Develepment and the
Fate of Teaching Science and Mathematics in Secondary Schools. M.Ed.
(Science Education) Dissertation. (Published), Faculty of Education, University
of Dar es Salaam.
29.0 WEMU (2009), Mihtasari ya Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada
iliyorekebishwa, na Utaratibu wa Kutahini (Barua ya Kamshina), Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dsm
30.0 MoEVT (2010) Basic Education Statistics in Tanzania, 2006 – 2010, Ministry
of Education and Vocational Training, Dsm
31.0 WEMU (2010) Moduli ya Ujuzi wa Kufundisha kwa Umahiri, MWAKEM, Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, DSM
32.0 MoEVT (2005) Facts About Basic Education in Tanzania, Ministry of Education
and Vocational Training, Dsm
33.0 MoEVT (2001), Construction of Secondary Schools, Guidelines for Buildings
and Furniture., Ministry of Education and Vocational Training , Dsm
34.0 WEMU (2007), Utaratibu wa kuzingatia katika kuanzisha Shule za Serikali za
kutwa zinazojengwa kwa nguvu za wananchi (Barua ya Kamshina), wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dsm
35.0 WEMU (2005), Nyaraka za Elimu za mwaka 1998 – 2005, Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Dsm
36.0 MoEVT( 2008), Education Sector Development Program(EDSP) (2008 – 17),
Ministry of Education and Vocational Training, Dsm
37.0 MoEVT (2004), Secondary Education Development Program(SEDP) (2004 –
2009), Ministry of Education and Vocational Training, Dsm
38.0 MoEVT (2010), Education Sector Review Aide Memoire. Ministry of Education
and Vocational Training, Dsm
39.0 MoEVT, The Teacher Management Development Strategy 2008 – 2013
40.0 Wizara ya elimu na Utamaduni (1997 ) Kiongozi cha Mkuu wa shule ya
Sekondari . Dar es Salaam
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
129
41.0 MOEVT (2010), Secondary Education Development Program II (SEDP II) 2010
– 2014, MOEVT, Dsm
42.0 Nyerere (1967), Education for Self Reliance ……………………………………………
43.0 MOEVT (2002), Primary Education Development Program I (PEDP I) 2002 -
2006, MOEVT, Dsm
44.0 MOEVT (2017), Updated Secondary Education Development Program I (SEDP
I) 2007, MOEVT, Dsm
45.0 MOEVT (2007), Primary Education Development Program I (PEDP I) 2002 -
2006, MOEVT, Dsm
46.0 WEMU (2009), Waraka wa Elimu Na.13 wa mwaka 2009, WEMU, Dsm
47.0 MOEVT (2010), Public Expenditure Tracking Survey, MOEVT, Dsm
48.0 OWM-TAMISEMI (2011), Taarifa ya OWM-TAMISEMI……………………………
49.0 MOEVT (2008), Education Sector Performance report, MOEVT, Dsm
50.0 WEMU (1998), Waraka wa Elimu Na.1 wa mwaka 1998, WEMU, Dsm
51.0 WEMU (2009), Taarifa ya Utafiti Kuhusu kushuka kwa Kiwango cha Ufaulu wa
Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2008, WEMU, Dsm
52.0 TIE (2008), Secondary Education Curriculum for Tanzania Mainland,
53.0 Maelezo ya Waziri (Juni, 2005),………………………………………..
54.0 UWEZO (2010), Uwezo Assessment Project www.JamiiForums.com
Rasimu 2
130
VIAMBATISHO
Kiambatisho Na. 3.1: Maeneo Yaliyohusika katika Utafiti
(a) Kanda za Elimu, Mikoa, Halmashauri na Shule zilizohusika:
Na Kanda ya
Elimu
Mkoa Halmashauri Shule
1 Dar es Salaam Dar es Salaam  Kinondoni  Kambangwa, Salma Kikwete,
Manzese, Goba Mpakani, Canosa,
Sierra
 Ilala  Azania, Jangwani, Mkera, Nyeburu,
Tusiime, Sandy Valley
2 Mashariki Pwani  Bagamoyo  Bagamoyo, Chalinze, Zinga, Ubena,
Marian girls, Kaole
 Mkuranga  Mwinyi, Lukanga, Kisiju, Mkungilo,
Mwandege Boys, Mseru
3 Nyanda za
Juu Kusini
Ruvuma  Mbinga  Kigonsela, Kitura, Monica Mbega,
Mkoha, St Luise Mbinga Girls, Kikodi
 Songea (V)  Matimira, Daraja mbili, Ndongosi,
Sili, Peramiho, Wilima
4 Nyanda za
Juu
Rukwa  Sumbawanga  Mzindakaya, Msanzi, Mbizi, Kaoze,
Kaengesa, Laela
 Mpanda  Katumba, Kanoge, Kabungu, Ikola,
FPC-Tumaini, Milala
5 Kusini Lindi  Lindi (V)  Mchinga, Mnara, Chikonji, Mipingo,
Namupa Sem, Nyangao
 Kilwa  Kilwa, Mitole, Pande, Mtanga
6 Magharibi Shinyanga  Bukombe  Iyogelo, Ushirombo, Nyakasaluma,
Uyovu, Queen
 Maswa  Senani, Majebele, Mwakaleka,
Mwamanenge, Ng’wanza, Lalago
7 Ziwa
Magharibi
Kagera  Muleba  Kimwani, Izigo, Kibanga, Biirabo,
Rubya Sem., Humura
 Karagwe  Rwambaizi, Mukiri, Morongo, Nono,
Karagwe, Rumanyika
8 Ziwa Mara  Musoma  Mara, Musoma, Nyasho, Nyabisare,
Makoko Sem, Victoria
 Bunda  Chitengule, Bunda, Sizaki, Nyeruma,
Ikizu, Wariku
9 Kati Singida  Singida (V)  Ughandi, Mungaa, Siuyu, Minyughe,
Dungunyi Sem, Ihanja
 Manyoni  Ipamuda, Idodyandole, Makuru,
Kinangali, Amani Girls, Mkwese
10 Kaskazini
Mashariki
Tanga  Tanga Jiji  Galanos, Tanga Tech, Mabokweni,
Chongoleani, Rosmini, Sahare
 Lushoto  Mgwashi, Soni, Mdando, Kireti,
Kifungiro Girls, Upendo
11 Kaskazini
Magharibi
Manyara  Mbulu  Maghang, Tlawi, Siday, Haydom,
Sanu Sem, Dongobeshi
Babati  Dareda, Duru, Gorowa, Ndeki,
Madunga, Joshua
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
131
(b) Maeneo Mengine Yaliyohusika katika Utafiti
Na. Eneo la Utafiti Ngazi
1 Taasisi ya Elimu Tanzania Taifa
2 Baraza la Mitihani la taifa Taifa
3 Vyuo Vikuu Mkoa/Taifa
4 Vyuo vya Ualimu Mkoa
5 Uk aguzi wa Shule Kanda Kanda
6 Ukaguzi wa Shule Wilaya Wilaya
7 Elimu Mkoa Mkoa
8 Elimu – Halmashauri(M) na (S) Wilaya
9 Tume ya Utumishi wa Umma (TSD) Wilaya
10 Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Wilaya
11 Madhehebu ya Dini Wilaya
12 Mashirika yasiyo ya Kiserikali Wilaya
13 TAMONGSCO Taifa
14 TEN/MET Taifa
15 Ofisi ya Mh. Mbunge Wilaya
16 Ofisi ya Mh. Diwani Kata www.JamiiForums.com
Rasimu 2
132
Kiambatisho 3.5: Zana na Idadi ya Wajibuji Kitaifa na Kimkoa
Na AINA YA ZANA WAJIBUJI
MALENGO IDADI YA WAJIBUJI WALIOPATIKANA KITAIFA NA KIMKOA
JUMLA
KIMKOA
KITAIFA
KITAIFA
RUVUMA
RUKWA
SHINYAN
GA
SINGIDA
DSM
PWANI
KAGERA
MARA
LINDI
MANYARA
TANGA
1 Dodoso A Wakaguzi wa Shule Kanda 4 44 4 4 4 4 4 4 1 4 4 4 4 41
2 Dodoso B Mkuu wa Shule 12 132 12 12 12 12 12 12 12 12 13 12 12 132
3 Dodoso C Wakurugenzi TET 4 4 4
4 Dodoso D Wakuu wa Idara za Mitihani NECTA 5 4 4
5 Hojaji A Wahadhiri - Vyuo Vikuu 2 4 4
6 Hojaji A Wanachuo- vyuo Vikuu vya Elimu 2 4 4
7 Hojaji A Wakufunzi wa Vyuo vya Ualimu 2 22 2 2 2 4 2 2 8 2 2 2 28
8 Hojaji A Wanachuo- vyuo vya Ualimu 4 44 4 4 4 8 4 4 6 4 4 2 44
9 Hojaji B Afisa Elimu Mkoa 1 11 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 11
10 Hojaji B Wakurugenzi Halmashauri 2 22 2 1 2 2 2 1 2 1 2 15
11 Hojaji B Afisa Elimu Halmashauri (S) 2 22 2 2 2 2 2 2 2 1 2 2 2 21
12 Hojaji C Afisa Elimu Halmashauri (M) 2 22 2 2 2 2 2 2 2 1 2 2 2 21
13 Hojaji C Mkaguzi Mkuu wa Shule(W) 2 22 2 2 2 2 2 2 2 2 2 2 2 22
14 Hojaji D Maafisa Tume ya Utumishi wa
Umma TSD (W)
2 22 2
2 2 2 2 2 2 2 2 2 2
22
15 Hojaji E Afisa CWT (W) 2 22 2 2 3 2 2 2 2 2 2 2 2 23
16 Hojaji E Viongozi wa Dini 4 22 4 4 2 4 4 4 4 2 4 4 4 40
17 Hojaji E Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2 22 2 1 2 2 2 1 1 2 2 2 17
18 Hojaji F Wabunge 2 22 1 2 2 2 2 1 3 1 2 1 17
19 Hojaji F Madiwani 2 22 2 2 5 11 2 2 2 11 2 2 2 43
20 Hojaji F Wazazi/Walezi 4 44 4 4 35 21 4 4 4 5 4 6 4 95
21 Hojaji G Wajumbe wa Bodi ya Shule 4 44 4 4 18 17 4 4 4 16 4 3 4 82
22 Hojaji H Wahitimu wa Kidato cha 4 - 2010 60 660 39 48 23 30 24 60 15 73 17 12 60 401
23 Mahojiano ya Pamoja A Wakuza Mitaala 5 10 10
24 Mahojiano ya Pamoja B Maafisa Mitihani (NECTA) 5 8 8
25 Mahojiano ya Pamoja C TAMONGSCO 5 6 6
26 Mahojiano ya Pamoja C TENMET 5 6 6
27 Mahojiano ya Pamoja D Walimu 60 660 43 67 67 43 72 60 50 48 51 52 60 613
28 Mahojiano ya Pamoja E Walimu Wasahihishaji Mitihani
Kidato cha 4
60 660 8
4 9 7 30 24 5 4 3 8 60 162
29 Mahojiano ya Pamoja F Wanafunzi Kidato cha 3-4 120 1320 108 109 106 115 120 116 100 112 130 4 120 1140
JUMLA 353 3894 46 246 275 301 287 305 313 217 316 252 129 350 3037
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
133
Kiambatisho 4.1 – Takwimu za ukaguzi wa shule ( 2007–2010) katika
Halmashauri zilizofanyiwa utafiti.
MKOA HALMASHAURI SHULE
UKAGUZI UMEFANYIKA
MARA NGAPI
DAR ES SALAAM
ILALA MKERA 2
NYEBURU 3
Jangwani 4
Azania 3
KINONDONI Kambangwa 2
Goba Mapakani 1
Manzese 1
Salma Kikwete 1
Zisizo za serikali
ILALA Siera 1
Canossa 3
MAGNUS 4
Tusiime 0
KAGERA
KARAGWE RWAMBAIZI 0
NONO 0
MUKIRE 1
MURONGO 0
MULEBA BIIRABO 2
KIBANGA 0
KIMWANI 1
IZIGO 0
Zisizo za serikali
KARAGWE KARAGWE 0
RUMANYIKA 0
MULEBA RUBYA SEMINARI 1
HUMURA 0
LINDI
KILWA MITOLE
KIVINJE 1
KIRANJERANJE 1
MTANGA
MPUNYURE
KILWA 1
LINDI (V) Chikonji
Mnara sekondari 1
Mchinga sekondari 1
Mipingo Sekondari
Zisizo za serikali
LINDI (V) Nyangao sekondari
Khairaat Islamic ss 1
Rondo seminari
MANYARA
MBULU HAYDOM 2
MAGHANG 1
SIDAY 1
TLAWI 2
Babati(HW) GOROWA 1
DURU 2
NDEKI
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
134
MKOA HALMASHAURI SHULE
UKAGUZI UMEFANYIKA
MARA NGAPI
DAREDA 4
Zisizo za serikali
MBULU Dongobesh 2
Sanu sem 3
Babati(HW) Madunga 1
Joshua 1
MARA
BUNDA CHITENGULE 1
BUNDA 1
WARIKU
NYERUMA 2
SIZAKI 1
MUSOMA (M) MUSOMA 1
NYABISARE 3
MARA 2
NYASNHIO 1
Zisizo za serikali
BUNDA IKIZU 2
MUSOMA (M) Victoria 2
Makoko sem
PWANI
BAGAMOYO Bagamoyo 2
Chalinze
Zinga 2
Ubena 2
MKURANGA Kisiju 2
Mwinyi 2
Mkugilo 1
Vikindu 2
Zisizo za serikali
BAGAMOYO Kaole 1
Marian Girls 2
MKURANGA Mseru Seminary
Mwandege Boys 1
RUKWA
SUMBAWANGA –
V Mzindakaya 3
Msanzi 2
SUMBAWANGA –
M Mbizi 1
Kaoze 3
MPANDA IKOLA
KABUNGU
KANOGE
KATUMBA
Zisizo za serikali
SUMBAWANGA –
V Laela
Kaegesa Seminary 1
MPANDA MILALA
FPCT TUMAINI
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
135
MKOA HALMASHAURI SHULE
UKAGUZI UMEFANYIKA
MARA NGAPI
RUVUMA
MBINGA KIGONSERA 2
KITURA
M.MBEGA
MKOHA 4
MBINGA Daraja Mbili
Matimira
Ndongosi
Sili 2
Zisizo za serikali
MBINGA St. Luise 1
Kikodi 2
MBINGA Peramiho 2
Wilima
SHINYANGA
BUKOMBE IYOGELO 3
USHIROMBO 3
NYAKASALUMA
UYOVU
MASWA SENANI
MAJEBELE
MWAKALEKA 1
MWAMANENGE 1
Zisizo za serikali
BUKOMBE Queen 2
Goldenland 3
MASWA Ng'wanza 2
Lalago
SINGIDA
SINGIDA -V MUNGAA 3
SIUYU 1
UGHANDI 1
MINYUGHE 1
MANYONI IPAMUDA
IDODYANDOLE 1
MAKURU 1
KINANGALI
Zisizo za serikali
SINGIDA -V Ihanja
Dung'unyi
Seminary 2
MANYONI Amani girls 3
Mkwese 1
TANGA
MABOKWENI 1
GALANOSI 1
CHONGOLEANI
TANGA UFUNDI
KIRETI
MDANDO
MGWASHI 2
SONI
3
www.JamiiForums.com
Rasimu 2
136
MKOA HALMASHAURI SHULE
UKAGUZI UMEFANYIKA
MARA NGAPI
Zisizo za serikali
Sahare 4
Rosmin 1
Kifungilo 1
Upendo 3
TANBIHI
Jumla ya shule 132
Jumla ya shule ambazo hazikukaguliwa 46
Jumla ya shule zilizokazguliwa mara 1 mau 269
Jumla ya shule zilizokaguliwa mara 2 au zaidi 18
Ukaguzi uliofanyika ulikuwa wa jumla, kufuatilia au maalum
www.JamiiForums.com

0 comments:

Post a Comment