Wednesday, September 25, 2013

HAYA NDIO MAJINA YA WAFANYAKAZI WA BENKI YA EXIM WANAODAIWA KUIBA PESA BENKI ZAIDI YA BILLIONI SABA.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imewazuia wafanyakazi  14 wa Benki ya Exim tawi la Arusha, akiwamo meneja wa benki
hiyo, Bimal Gondalia, kutosafiri nje ya mkoa wa Arusha, bila idhini ya Mahakama hiyo,Maamuzi hayo yanawafanya washtakiwa kushindwa kusafiri au kutoka katika Mji wa Arusha bila ruhusa ya Mahakama.

Washitakiwa hao walipandishwa kizimbani Septemba 20, mwaka huu na kusomewa shitaka la kula njama na kuiba zaidi ya Sh. bilioni saba.

Washitakiwa wenyewe ni Joyce Kimaro, Lilian Kageye, Doroth Chijana, Tuntufe Agrey, Michael Majebele, Ginese Massawe na Joseph Meck.

Wengine ni Robert Rubeni, Livingstone Mwakijabe, Clara Lawena, Evance Kashebo, Neema Kinabo na Christopher Lyimo.

Pia wanadaiwa  kuiibia benki hiyo Dola za za marekani 400,000 katika kipindi cha  miaka mitatu.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Diaz Makule, alidai kuwa wizi huo ulifanywa na wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti  kati ya mwaka 2011 na 2013.

0 comments:

Post a Comment