1. R.O.M.A ni muumini wa dini ya kikristo(R.C)
aliyezisoma sakramenti zote 7 na kupokea ya ubatizo/ekaristi takatifu
na hata kipaimara...nangoja NDOA!!
2. Ile sauti mnayosikiaga
ikisema TONGWE RECORDS BEIB siyo ya ROMA ni JOSLIN!!ambae naye ni
miongoni mwa wasanii walio chini ya tongwe!! plus KAMIKAZE/JOS
MTAMBO/DOMO KAYA/SAIGON/NORMAN WA BSS/
3. Kuna J. MURDER ambae
ndiye CEO wa tongwe records, na kuna J.RYDER ambaye ndiye anagonga
midundo ya TONGWE RECORDS. watu wawili tofauti!!
4. Tongwe
records ni studio zilizopo daresalaam mitaa ya masaki/ dakika kama 3
tu kutokea coco beach!! na haipo kigamboni kama wengi wanavyodhani!!
lakini tanga kuna kijiji kinaitwa TONGWE na ndicho kijiji ama himaya
ya J. MURDER!! ambaye ndiye huyo mmiliki!!
5. Sijawahi
kufungwa wala kwenda jela/ sijawahi kuitwa ikulu/ nyimbo zangu za
awali tanzania/ mr president ndiyo zilipigwa stop kupigwa ktk baadhi
ya vituo vya radio, kwa sababu zao binafsi!!
6. Mimi kwetu ni
TANGA nimezaliwa na kukulia na kusoma na kuanza muziki TANGA/ kiasili
ni mpare(SAME KILIMANJARO) na mama ni mchaga!! kikabila utani
unaruhusiwa, mpare mtani wake mchaga, ndiyo maana mchaga siku zote
namuona ni mtani wangu(MSIPANIKI)!! nadumisha mila ya utani!!
7.
Katika face book account yangu niitumiayo ni hii ya Roma
Tongwe na pia kuna page yangu inaitwa R.O.M.A
na kuna group inaitwa ONGEA
NA ROMA baaaasiii!! lakini kuna wana tu kwa mapenzi yao ama kwa
uduanzi wao huamua na wamefungua akaunti kibao wakijiita Roma
mkatoliki/Roma mtanzania/Roma Tanga/ na zingine, tena ukizipitia
jamaa wana marafiki wengi kuliko hata mimi, na wanazi-run kama mimi
yaani nao wanapost kabisa ETI OYAA MOROGORO HERE I COME...hahahahahha
bongo bana!!
8. Aliyeimba chorus ya 2030 ni mtoto wa rafiki
yangu anaitwa STORY, ni mtoto wa miaka 7hiviii!! lakini chorus ile
iliimbwa miaka ya 90 naa zamani sana na binti mmoja ambaye kwa sasa
amekuwa sana!!!
9. Nilianzisha mtindo wakuuza nyimbo zangu
on-line(BUT LOKO) na kama trial nilianza na 2030(tsh 3000/=), ilikuwa
ni nyimbo inayohitajika sana na wenye mapenzi na kuujua umuhimu wa
kazi ya sanaa walinunua(sio woote) ila kati ya marafiki 5000 wa fb
walinunua takribani watu 500 tu!! hadi sasa siwezi na sijawahi mtumia
mtu nyimbo yangu akiniomba for free!! it z for sale!! 3000 per
track!! otherws tumia indirect ways!!
10. Natoa ngoma 1 kwa
mwaka!! tokea naanza game hii, ndiyo utaratibu niliojiwekea, najaribu
kufanya LIVING SONGS!!(nyimbo zinazodumu/zinazoishi, kana kwamba
ukisikia jogoo la tanzania linawika sasa uamke kwenye kiti chako
turuke ruke!!) wapo artist ambao ndani ya miezi 6 wanatoa ngoma hata
4, na zinaweza feli zote, ama zikafaulu zote!! ni sawa kwa upande
wao!!ndio njia waliyoichagua!! So toka tanzania 2008 hadi 2030
iliyotoka december 29 2012 siku moja kabla ya 2013!! ipo
hivo!!
kwahiyo nadaiwa ngoma mpya mwaka huu!! na SOON ZITATOKA
VIDEO 2 ZA ROMA!!
0 comments:
Post a Comment