MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Mchana huu ukimuona mtu kitambaa cheupe na kasimama nje ya
nyumba, hiyo ni dalili kwamba mambo>>>>>>
yako mengi yatakuwa hadharani,
unashauriwa nenda safari yako na kila unalotaka kulifanya ulifanye
haraka sana.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Mchana huu
unafikiri juu ya nafsi yako,unataka kujua maisha na hali yako
itakuwaje. Pana kazi au jambo ambalo unashaka nalo kama litatimia au
vipi? mambo yako unayotaka yatakuwa kwa kupata ushauri wa rafiki
yako. Usipopata msaada yataharibika..
NGE - SCORPIO (OCT 24-
NOV 22)
Mchana huu pana mgeni unayemtegemea au kitu kilichopotea
ambacho unataka sana kujua habari zake, Nyota zinasema kuwa Mgeni
atakuja kati ya leo na siku tatu zijazo na na kitu kipo muulize mdogo
wako atakwambia hiyo. Kimehifadhiwa kwenye kona au chini ya kitanda.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Mchana huu una
hamu ya kukutana na mpenzi wako na kujua juu ya safari au biashara na
kazi. shughuli zako za kawaida zina uzito na kuna mtu anataka
kukukwamisha dawa, Fanya ibada na sala kwa mola wako Mambo yako mengi
yatanyooka baada ya kujirudi.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 –
JAN 20)
Leo ujue kuwa yote unayoyataka yakiwa ya kimapenzi,
kibiashara na kimaisha yatatimia kati ya leo Jumatatu au Ijumaa usiku
Hakikisha kila neno unaloambiwa unalifanyia kazi
NDOO
–AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Wiki hii ukipita mahala ukakuta
sherehe, hiyo ni dalili kuwa Mpenzi wako atarejea salama, na
utashinda mitihani na adui yako atajuta.mambo yako yatafunguka na
mikwamo ya hapa na pale itapotea.
SAMAKI – PISCES (FEB 20-
MACH 20)
Leo ukiona watu wamekaa pamoja wakicheka na kuongea kwa
fujo, Lazima utapata kitu unachokitaka au pesa unazohitaji au mtu
unayemtarajia. Mtoto au kitu kilichopotea kitarejea. Jihadhari na
marafiki zako inaonekana wiki hii watakujia na mpango ambao ya
kukupotezea pesa.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo Safari
unayofikiria ni nzuri, na biashara yako itafanikiwa mambo yako
hayatakuendea kombo Unashauriwa kuwa kufanikiwa kwa mambo yako
kunahitaji wewe uanze kujishughulisha na mambo hayo mara moja wala
usisite site.
.
NG’OMBE – TAURUS (APR 21 – MAY
20)
Mchana huu kuna dalili huko uendako utakumbana mambo ya
vitisho au kutatokea hali ya kutoelewana na mtu unayemdai.
unashauriwa kuwa pesa hizo au kazi unayoitaka itapatikana tu baada ya
mtu fulani kurejea, au baada ya kupata barua.
MAPACHA -
GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Wiki hii utapata raha katika matembezi
yako utakayoyafanya jioni , pia yule mpenzi wako atakutembelea na
kukuburudisha. Ukikosa vitu hivyo basi cheo lazima utapata, lakini
unashauriwa uwe na tabia ya kuacha wasiwasi na uwe na moyo wa
kujitegemea
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Siku tatu zijazo
kuwa waangalifu sana hasa katika mambo madogo madogo, kila kitu chako
kiwe kinakwenda katika mpangilio maalum, kuwa makini sana katika
masuala ya uvaaji, huko uendako kuna kudanganyana tu hakuna maelewano
yeyote mtakayoyafikia, kwa kuwa unayemfuata huko amepanga
kukudanganya.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Kipindi hiki
kuna dalili kwamba matatizo yako yatakwisha au kupungua kwa kiasi
kikubwa. Ile mikosi iliyokuwa inakuandama wewe mwenyewe au familia
yako itakwisha kwa msaada wa mtu kutoka mbali atakayekuja kati ya leo
na Jumatano.
0 comments:
Post a Comment