![]() |
RUGE MUTAHABA |
Moja ya matatizo yanayoikumba nchi yetu ni wananchi kutokujua haki na sheria za msingi, Nimefuatilia sana suala na mgogoro wa kurushiana maneno kati ya CLOUDS MEDIA na LADY JAY DEE. Nachukua nafasi hii kama mdau wa vyombo vya habari kwakua ndipo ueledi wangu ulipo.
Lady Jay Dee ametoa duku duku lake rohoni kwenye mitandao yakijamii ingawa yeye sio mtu wakwanza kulalamika kuhusu Clouds Media, Na kila malalamiko yanapotokea huwa yanapata msukumo mkubwa sana kutoka kwa wananchi na hii inaashiria fika kua watu wengi wanaona mapungufu ya Clouds Media.
Kwa upande wa muziki wa kizazi kipya haina ubishi kua Clouds Media imesaidia sana na ndio imekua chachu yakukuza mziki huu na kutambulisha wasanii wengi sana na kuvumbua vipaji vyao, Binafsi nawapa hongera sana na muendelee na moyo huo.

Nimekua karibu na kuzungumza na zaidi ya 80% ya wasanii wa hapa Tanzania, tatizo lao kubwa na Clouds Media ni ile hali yakutaka kudominate na kuwanyonya wasanii kisa wao ndio wamewatoa. Dunia ya sasa ni ya utandawazi na wasanii wengi wamefunguka kiakili na mtazamo na pia wameaanza kujua haki zao kutokana na jasho lao.
Leo Ruge kapoteza muda mwingi sana kuzungumzia suala la Ugomvi wao na Lady Jay Dee. kwa mtazamo wangu ni kwamba RUGE KATUMIA NGUVU NYINGI SILAHA NYINGI NA KAMPUNI YAKE KUMPIGA LADY JAY DEE kitendo ambacho kimempotezea hadhi na ueledi wa kazi na hata Cheo chake. Kusema kua bongo flava isipigwe leo kisa anaonyesha kua anauwezo wakufanya lolote ni sawa na kumfukuza mwendawazimu aliechukua taulo lako ukiwa bafuni ukaanza kumkimbiza ukiwa mtupu barabarani. Lady Jay Dee has nothing to loose kwa maamuzi yake ya leo.
Na aliposema wamekua wakipiga na kuwasuport wasanii bure ni kosa kubwa sana kwakua clouds wanatumia nyimbo hizo za wasanii bure bila kuwalipa chochote, unapotengeneza tangazo unatumia wimbo wa msanii unatakiwa kumlipa, unapopiga nyimbo zake unatakiwa kumlipa maana yeye kakufanya upate wasikilizaji na watazamaji.
JE? leo wasanii wote wakiungana na kusema kua kuanzia sasa Clouds wasitumie nyimbo zao kwa lolote itakuaje? si ndio mtapotea kabisa kwenye ramani hii ya media? RUGE HAJATUMIA BUSARA NA CLOUDS MEDIA IMEPOTEZA HADHI YAKE LEO. Alipotumia muda mwingi kuhusu SUGU nilifikiri management nzima ilijifunza kutokana na kosa lile kumbe laah.
JE? kama kweli ni radio ya watu, maamuzi haya yameangalia watu au mtu?
Kikubwa zaidi ni kwamba kuna kauli mbia ya Made in Tz, hii ndio maana yake?ulilifikiria hili?
Hii inadhihirisha wazi kua CLOUDS MEDIA inawadharau na kutokuwaheshimu wasanii wote wa Tanzania. Ingekua wasanii wana umoja wangegoma kazi zao zisisikike wala kuonekana kwenye chombo chochote cha CLOUDS MEDIA ili na wao wafeel pinch wanayoipata wasanii leo.
Je ni kwanini kila kukicha clouds mpate lawama? lazima kuna tatizo sehemu hivyo ni vyema kurekebisha mapungufu tujenge Taifa na muziki wetu.
Rafiki yangu Dada yangu Lady Jay Dee maneno uliyotumia kufikisha ujumbe yalikua makali sana na hayakua na amani ndani yake.Clouds kutohudhuria mazishi yako au kugusa jeneza lako haitobadiliki yale yanayotokea leo zaidi yakuongeza chuki na mpasuko.
BUSARA NI MUHIMU SANA KUTUMIKA PANDE ZOTE!
Mwandishi
Bazo Komu
0 comments:
Post a Comment