Monday, May 6, 2013

NYOTA YAKO LEO JUMANNE TAREHE : 7/5/2013



NG’OMBE – TAURUS (APR 21 – MAY 20)
Siku ya leo ukimuona mtu anamhudumia mgonjwa wa homa, hiyo ni dalili kwamba mpenzi wako atakughasi kwa maneno maneno kila wakati hata kama wewe utakanusha lakini yeye bado atashikilia kukuhasi. 

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Ikitokea leo wakati wowote ukaona watoto wanapigana, au watu wazima wanazozana, hiyo ni dalili ya kwamba mambo yako yatasimama au kuwekewa vikwazo vya hapa na pale. Pendelea kufanya ibada na kutoa sadaka

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22) 
Siku ya leo akikutana na Wanawake wanapigana, hiyo ni dalili kuwa kuna marafiki zako walio mbali a wewe wanakufikiria sana na wapo njiani kuja kukutembelea na kukuletea msaada. 

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Siku ya leo ukikutana na mtu wakati wowote anakata kucha, hiyo ni dalili kuwa mambo yako mengi yatakwama kutokana na vizingiti utakavyokuwa unawekewa na wabaya wako. Kuondoa hali hiyo pata msaada kutoka kwa watalaam.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23) 
Leo katika matembezi yako ukikutana na Mtu mwenye vidole vya mkononi pungufu, hiyo ni dalili ya kupoteza mpenzi wako wa muda mrefu, pia ni dalili ya kupoteza kitu chako cha thamani sana, chunga sana hali ya kusahausahau.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23) 
Kama ikitokea leo ukakutana na Moto unawaka au mtu aliyeungua, hiyo ni dalili kuwa mambo yako yataharibika na chanzocha yote hayo ni mpinzani wako wa karibu asiyependa maendeleo yako. Unashauriwa ili kuepukana na hayo ni vyema ukahama sehemu uliyopo hivi sasa. 

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22) 
Siku ya leo katika matembezi yako ukikutana na mtu amebeba Samaki, hiyo ni dalili kuwa mambo yako yatakwama, unatakiwa kuwa makini sana na watu watakaokujia na kutaka msaada kwako, utapata bahati mbaya, kila samaki mmoja utakayemuona ni tatizo moja zito. 

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21) 
Siku ya leo ukion kitu chochote kinaelea kwenye maji, hiyo ni dalili kuwa mambo yako yaliyokuwa yamekwama sasa yatakwamuka na kuanza kukuletea faida kidogo kidogo.. Jitahidi kujibidiisha..

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20) 
Ikitokea leo kama ukiwa katika matembezi yako ukakuta watoto wanacheza mpira,hiyo ni dalili kuwa wewe ni muoga kutoa msadaa kwa matatizo yanayowapata wenzio hasa kama mkiwa mmeongozana pamoja. Jaribu kulekebisha hiyo tabia mara moja vingenevyo itakuleta balaa. 

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19) Siku hii ya leo ukimuona mtu anaimba asubuhi, hiyo ni dalili kwamba utapata mkosi kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20) 
Siku hii ya leo ukikutana na Mbwa na akawa anakufuata bila kufanya fujo, hiyo ni dalili kwamba utapata fedha leo au utapata faida ambayo hukuitegemea au utasamehewa madhambi uliyomfanyia rafiki yako.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Siku ya leo Jumanne, ukikujia mtu akakwambia anaumwa homa, hiyo ni dalili ya kwamba mikwamo yako itafunguka hivi karibuni na kama ulikuwa unaugua basi utapona haraka. Vile vile ni dalili ya kuletewa zawadi kutoka kwa rafiki yako

imeandaliwa na Mtabiri Maalim Hassan

0 comments:

Post a Comment