Monday, May 6, 2013

CHIDDI BEENZ MADAWA YA KULEVYA YANAKUPOTEZA-KALA PINA



Moja kati ya waasisis wa muziki wa Hip Hop Tanzania kutoka katika kundi la Kikosi cha Mizinga Kala Pina amemtuhumu Msanii mwenzake wa Hip Hop kutoka Ilala Dar es salaam Chiddi Benzi Chuma kuwa anatumia madawa ya kulevya.

Kala pina alizungumza hayo katika kipindi cha Redio Moja Hapa Mjini alipokuwa akaisema sababu za yeyer kuamuwa kumshushia kipigo Msanii huyo jukwaani Maisha Club

" ukweli ni mambo fedheha, mdogo wetu chidi benzi cocaine au heroin / unga anaovuta unampeleka pabaya, tena mimi kama kaka yake namshauri aachane na matumizi ya madawa kulevya, kwa sababu mwisho wake utakua m'baya,

mimi nilikua back stage na ikafika zamu yangu kupanda jukwaani nikawa naskia sauti mtu anatamba jukwaani kwa dakika saba ama nane, alikua ananichelewesha kupanda, na ananiharibia show yangu, huyu mtu si adui, nikatoa amri mara tatu kama F.F.U aka kaidi ndipo nikamfata na kumpa dozi, si akaanguka chini na mimi nikaendelea na show yangu, hakuna hata mtu mmoja atakaye kubali kuharibiwa kazi, hata rais Kikwete ukimharibia utaishia jela."

madai ya kuwa msanii Chiddi Benzi anatumia madawa ya kulevya yamezidi kukua na kuongezeka kwani hata siku ya jana msanii huyo aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Ney wa Mitego anamtumia messeji na kumwambia kuwa yeye ni Teja.anavuta unga na kuwa hana cha maana anachofanya katika maisha ya kila siku.

KALA PINA
Lisemwalo daima huwa lipo na kama halipo basi laja hivyo Chuma kama kweli ni mtumiaji wa madawa ya kulevya bora uachane nazo kwani unatambua kuwa kuna wasanii kadhaa wameshapitia hali hizo na kupata madhara makubwa na kujikuta wakishindwa kufanya mambo ya maendeleo.

0 comments:

Post a Comment