Tuesday, May 7, 2013

PROFESA JAY KWA NGUVUZANGU,AKILI ZANGU NA UWEZO WANGU NA MSUPPORT LADY JAYDEE.


Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Profesa Jay anaetamba na ngoma kali kibao katika tasnia ya Bongo Flava ameonesha wazi kutoa support kwa msanii Lady Jaydee katika show ya kutimiza miaka kumi na tatu ya Kimuziki kwa mwanadada Lady Jaydee.

Profesa Jay ameweka wazi msimamo wake huo leo hii mchana na kusema kuwa kwa nguvu yake yote,akili zake zote na uwezo wake wote atajitoa kuhakikisha anafanikisha Show HIYO kwa kufanya PERFORMANCE KALI.

Nitakuwa na @JideJaydee kwenye show yake ya miaka 13 ya LADY JD, Kwa NGUVU zangu zote, AKILI zangu zote na UWEZO wangu wote, KARIBUNI SANA”

Hapo awali mwadada Lady Jaydee alisema kuwa kina Linah.Barnabas na Ben Paul wangekuwepo katika show hiyo lakini baada ya siku kadhaa mbeleni Linah Sanga na Barnaba walijitoa katika Kufanya Tamasha Hilo la Miaka 13 ya Lady Jaydee.

Lady jaydee akizunguzia show hiyo amesema kuwa teyari mpaka sasa Tickets zishaanza kupatikana katika maeneo aliyoainisha

Tickets za VIP Tsh.50,000/= zinapatikana SHEAR ILLUSIONS Mlimani City, BM Salon Kinondoni, CITY SPORTS LOUNGE mjini, NYUMBANI LOUNGE, SAMAKI SAMAKI Mlimani City na kwenye gari yangu popote utakapopishana na mimi.

Alimaliza kwa kusema kuwa MIAKA 13 YA LADY JAYDEE njooni tuimbe na tusherehekee kwa pamoja ta 31 May 2013.
Sehemu ya Parking ya ndani ya Nyumbani Lounge, Tranic Plaza 

0 comments:

Post a Comment