Chuo
kikuu cha kampala University KIU kilichopo jijini Dar es salaam
maeneo ya Gongolamboto kimesimamishwa kutoa mafunzo ya Shahada za
Uzamili na Uzamivu kufuatia kukuendesha mafunzo kinyume na Utaratibu
na kutokuwa na wahadhiri wakutosha na wenye sifa.
Tume
ya Vyuo vikuu TCU katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru
Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam yafuatayo;
- KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikuwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam
- KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu zilizotajwa hapo juu waweze kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.
Tume
haitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na
chuo hicho kwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam.
Angalizo:
Chuo
cha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa
mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti
zilizopitishwa
na TCU kwa mujibu wa Ithibati ya Chuo Husika.
Imetolewa
na:
Katibu
Mtendaji
TUME
YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
0 comments:
Post a Comment