Tuesday, May 7, 2013

NILIOTA NDOTO KWA HAYA YANATOKEA SASA -MASANJA MKANDAMIZAJI


Msanii wa nyimbo za injiri na mchekeshaji wa kundi la komedi Masanja Mkandamizaji ameandika amesema kuwa aliota ndoto kuwa kuna watu wanapenda wengine wagombane ili wao waweze kufanya biashara zao vzuri.

Niliota ndoto. Kuna watu wanapenda watu wengine wagombane ili wafanye biashara zao vizuri. Mungu anawaona”

msanii na Mchekeshaji huyo amefunguka hayo kufuatia ugomvi uliopo katika tasnia ya muziki kati ya baadhi ya viongozi wa Redio Clouds pamoja na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Mwanadada Lady Jaydee unaoendelea na kushika kasi kubwa katika masikio ya watu na katika vyombo vya habari mbalimbali nchini.


Kwani kwa ugomvi huo kuna kundi kubwa la watu linafaidika na mvutano wa watu hao wawili ingawa kwa namna moja unajenga na kuhalibu pia,hivyo kuna kundi kubwa la watu wanaendelea kufaidika na kutengeneza maisha yao.

0 comments:

Post a Comment