Mahakama
kuu ya kanda ya Dar es salaam leo imemfutia mashtaka ya Ugaidi aliyokuwa
nayo Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa
Chama cha Demokrasia na maendeleo Bw Wilfred Lwakatare.
Taarifa
kutoka Mahakamani zinasema kuwa Lwakatare amebakiza shitaka moja la Utekaji
ambalo pia linanafasi ya Dhamani
Lwakatare
alikamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani na kushatakiwa kwa kesi
ya Ugaidi na Utekaji baada ya kuvuja kwa Video iliyokuwa akionesha kuwa
Mkurugenzi huyo alishiriki katika kupanga njama za kigaidi na kuwashambulia
baadhi ya watu wakiwamo waandishi wa habari nchini.
Kutokana
na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili
Lwakatare hakuweza kupata mdhamana .
0 comments:
Post a Comment