Shindano
la kunengua la Manywele Kigori wa Extra Bongo sasa limefika patamu mazoezi
yanatarajiwa kuanza mwisho wa mwezi huu.
Maimatha
Jesse ambae ni mwaandaaji wa tamasha hilo amesema kuwa atakutana na waandishi
wa habari wiki ijayo kutoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na shindano hilo ambalo
miaka ya nyuma lilikuwa likijulikana kama 'Manywele Kimwana wa Twanga Pepeta'
"Nitakutana
na waandishi wa habari ili kuwaelezea kwa undani zaidi, lakini mwishoni mwa
mwezi huu tutafanya uzinduzi wa shindano letu na kisha vigori wataanza rasmi
mazoezi,"
Alifafanua
kuwa uzinduzi wa mazoezi ya vigori utashirikisha wasanii mbalimbali wa muziki
wa kizazi kipya na kwamba wakati wa mazoezi washiriki watakuwa wanajifunza
kucheza mitindo mbalimbali ya bendi ya Extra Bongo.
"Ndiyo
maana shindano likaitwa Manywele Kigori wa Extra Bongo, hivyo wakati wa fainali
vigori watachuana kwa kucheza mitindo mbalimbali ya bendi hiyo ambayo kwa sasa
inaonekana kuwa juu kuliko nyingine.
0 comments:
Post a Comment