Wednesday, May 8, 2013

SIR ALEX FERGUSON AMEIACHA MANCHESTER UNITED



Meneja wa Kikosi cha Man United Sir Alex Ferguson ameiacha Club ya Man U  rasmi baada ya kustaafu kazi yakuongoza Club ya Manchester United .

Club ya manchester imethibitisha kustaafu kwa Meneja huyo na kusema kuwa akimaliza msimu huu hatakuwepo  tena na club hiyo kwa sababu muda wake utakuwa teyari umekwisha kuwepo katika club hiyo na pia utakuwa umefika wakati wa Meneja huyo kupumzika kufanya kazi ya kufundisha na kuongoza Club ya Manchester United.

Maamuzi hayo ya Meneja huyo yamekuja kutokana na kuweza kufanya mambo mengi katika Clubs mbalimbali alizopita na kutimiza malengo yake katika soka hivyo anapaswa kukaa pembeni na kuwa kama mshauri na si Meneja tena wa Club hiyo ya Mancheter United
Baada ya maamuzi hayo Club ya Manchester United imetoa shukrani kwa Meneja huyo kwa mambo mengi aliyoyafanya katika Club hiyo.

0 comments:

Post a Comment