9:36 PM
PUNDA- ARIES (MACH 23- APR
20)
Leo kuna dalili ya mambo yako kukuendea vizuri lakini
utajikuta unakabiliwa na kesi ijapokuwa kesi hiyo utakuja kushinda
hapo baadae. Yule rafiki yako au ndugu yako aliyekuwa jela atatoka
hivi karibuni, lakini atakuletea matatizo makubwa.
NG’OMBE
– TAURUS (APR 23 – MAY 20)
Leo huko uendako utakumbana mambo
ya kufurahisha au kutatokea hali ya makubaliano na mtu
uliyemkopa.Unashsuriwa baada ya matatizo haya usijaribu kukopa tena
wuiki hii unaweza kushiondwa kulipa.
MAPACHA - GEMINI (MAY 23-
JUN 23)
Leo yule adui yako atakutembelea na kukuudhi.naikitokea
ukikutana na mtu mzigo wa aina yeyote, basi elewa kuwa utaona mambo
ya ajabu katika matembezi yako utakayoyafanya jioni ya kesho,
KAA
- CANCER (JUN 22- JUL 22)
Elewa kwamba huyo unayemfuata huko
unakokwenda amepanga kukudanganya, ni vyema usiende. Leo ukimwona
mtoto amelala kwenye godoro nje ya nyumba, basi ujue hiyo ni dalili
kwamba kuna ugomvi unakuja na kutakuwa hakuna maelewano yeyote
mtakayoyafikia,
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Matatizo
yako ya kifedha yaliyokuwa yanakuandama wewe mwenyewe au familia yako
yatakwisha.Kuna mpango utaletewa ambao utakukwamua katika ukwasi. Na
ikiwa leo utakutana na mwanamme kabeba Ndoo, hiyo ni dalili kwamba
matatizo yako yatakwisha kabisa.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT
23)
Leo mambo yako mengi yatakuwa hadharani, yatakufedhehesha na
kukuaibisha sana, unashauriwa kuwa makini na kila unalotaka
kulifanya. Na ikitokea ukimuona mtu ameshika Panga, hiyo ni dalili
kwamba utaaibika
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Leo
ukikutana na mtu ambaye Sharubu mchanganyiko nyingi basi ujue kuwa
mambo yako utakayo yafanya kwa ushauri wa rafiki yako yatakuwa
mabaya, Elewa rafiki huyo ni adui na hatakusaidia .Jiepushe naye.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Mambo yako yanahitaji
ujasiri wa hali ya juu kuweza kuyaendeleza, ulegevu kidogo tu
utakusababishia hasara kubwa usiyoitegemea. Jaribu kuwa mkali na
ufatilie kwa karibu mipango yako yote.
MSHALE - SAGITARIUS (
NOV 23 - DES 23)
Leo hii katika shughuli zako za kawaida
ukikutana na Mlevi, hiyo ni dalili kwamba kuna safari ya mbali na
yenye faida itakujia. Ukipata nafasi hiyo usiiachie.
MBUZI -
CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Mambo utakayoambiwa Leo hii
yatakuwa ya kweli Hakikisha kila neno unaloambiwa unalifanyia kazi
hasa masuala yanayohusiana na mapenzi na biashara. Usiyapuuzie hata
kidogo
NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 19)
Leo kula
kila dalili kuwa mambo yako yatafunguka na mikwamo ya hapa na pale
itapotea, baada ya muda hali itaendelea kuwa nzuri na matatizo
yaliyokujia kwa kasi yatapotea na kukuacha ukiwa na furaha
SAMAKI
– PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo mipango yako itakuwa
mizuri. Epuka kupingana pingana na watu unaofanya nao Biashara,
Jihadhari na marafiki zako inaonekana leo watakujia na mpango
ambayousipokuwa makini itakupotezea pesa.
Imeandaliwa na Mtabiri Maalim Hassan
0 comments:
Post a Comment