Thursday, April 18, 2013

BIBI KIDUDE AZIKWA KWA MILLIONI ISHIRINI ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar imetoa pesa jumla ya Millioni ishirini za kitanzania kwa ajiri ya kukamilisha suala la mazishi ya Legendary huyo aliefariki jana baada ya kusumbuliwa na matatizo ya vidonda vya tumbo na miguu.
 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa fungu la pesa hizo kukamilisha mazishi na heshima ya Mwisho kwa Bikidude kutokana na nafasi yake katika jamii na mchango alioufanya kwa nchi kwani alikuwa Balozi mzuri kupitia fani yake ya muziki wa Taarabu aliyoitumia kupeperusha bendera ya Tanzania na Zanzibar sehemu mbali mbali ulimwenguni.



Hii ndio safari ya Mwisho ya Bibi Kidude iliyosindikizwa na viongozi mbalimbali na watu maarufu wengi waliojitokeza kumsindikiza katika nyumba yake ya Milele.

UPUMZIKE KWA AMANI BIBI YETU:AMINA

0 comments:

Post a Comment