Tuesday, March 12, 2013

WALINZI WAWILI WAUWAWA SERENGETI



Mwandishi Yassin Sanga-Serengeti
Walinzi wawili wanaolinda Bwawa la Serengeti Manchila linalosamabaza maji katika mji wa Magumu,walinzi hao walipigwa risasi usiku wa kuamkia leo na kufa hapo hapo.
 Watu waliotenda tukio la mauwaji hayo hawakuweza kuchukua mali aina yoyote ile katika eneo la tukio licha ya kuwepo kwa PikiPiki simu na vitu vingine katika eneo la tukio lakini kwa mujibu wa Raia wema katika eneo hilo walilifananisha tukio hilo na ulipwaji kisasi kwa walinzi hao jambo ambalo halina ukweli ndani yake kwani hatujapata chanzio kamili cha tukio hilo.
Mungu azilaze pema peponi Roho za Marehemu hao.


0 comments:

Post a Comment