Mwandishi kitalima gerald/kwa msaada wa mtandao
Zaidi ya makadinali mia moja wamekutana Roma ITALIA leo kwa ajiri ya
kumchangua PAPA atakae liongoza kanisa katoliki Duniani kama kiongozi wa kiroho
kwa wakristu Duniani kote.
Makadinali 115 walihudhuria misa
maalumu iliyofanyika katika kanisa la St Peter’s Basilica mjini Roma Italia.
Mchana huu makadinali hao wataendelea na mchakato wa kumchagua Kiongozi
mpya wa wakristu Duniani kote kitendo ambacho kitafanyika kwa siri kubwa.
Makadinali hao watachagua kwa mara nne kila siku mpaka Robo tatu ya
makadinali watapokubaliana na jina husika la kiongozi alioteuliwa au
kuchaguliwa.
Uchaguzi huu umefuatiwa kujiudhuru kwa Benedict xvi mwezi uliopita baada ya
kujiona anahitaji kupumzika kufuatia umri wake kuwa mkubwa,Hivyo kushindwa
kuongoza,mpaka anajiudhulu Benedict xvi alikuwa na umri wa miaka 85.
0 comments:
Post a Comment