Monday, March 11, 2013

NYOTA YAKO LEO JUMATATU : 11/3/2013:



SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20) 

Leo, ikitokea ukajikwaa mguu wa kulia mara mbili, hiyo ni dalili ya kuletewa zawadi kutoka kwa rafiki yako aliye mbali. Kuna habari ya matatizo utaletewa kati ya leo na juapili ijayo. Kuwa tayari kukabiliana na habari hizo

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)

Leo mambo yako mengi yatakwama unatakiwa uwatumie watu wengine kukusaidia . Mwendee mtu mkubwa Serikalini au katika dini ambaye atakusaidia kuondokana na shida hizo.

NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Wiki hii maisha yako yatakuwa mazuri matatizo madogomadogo kama maradhi au kukosa pesa au kugombana na watu yatapungua. Vilevile Mkeo au mumeo atakufurahisha kwa zawadi atakayokupa. .

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23) 

Leo una wasiwasi na jambo lako unalotaka kufanya, Elewa kuwa kuna dalili kuwa mambo yote uliyokuwa unayafuatilia hayatafanikiwa, unashauriwa usafanye jambo hilo au lingine lolote kwa wakati huu.

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22) 
Mwezi huu utakuwa mwezi mbaya kwako, mambo yako yatafuatiliwa na watu bila ya wewe mwenyewe kujua, wengine wakitaka kukuhujumu na kukusaliti kutokana na mafanikio ambayo ungepata, jaribu kuwa mwangalifu kwa kila hatua utakayoichukua.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Wiki hii mipango ya ndoa au mapenzi itaendelea kama kawaida na mwanamme au mwanamke utakaekutana nae atakupa mawazo mazuri kuhusiana na mipango yako na hiyo itakuwa ni dalili ya kufanikiwa kwa kila jambo.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23) 

Hivi sasa unafikiri sana juu ya safari na unataka safari hiyo ifanikiwe. Unakabiliwa ugomvi, upinzani, uadui, ugonjwa au unauguliwa . Kipindi hiki moyo wako umeshughulika sana na Mwanamke au mshirika wako au ndugu zako au rafiki yako.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23) 

Leo Inaonekana kutatokea mgogoro mkubwa kati yako wewe na mmoja wa hao unaowategemea. Wewe unataka kuwaongoza na wao wanakufanya wewe adui yao, Migongano hiyo imewahi kuzua mzozo wa kutupiana maneno machafu hadharani ambapo palijaa watu wengi wakawa wanakusikilizeni.jaribu kuwa mvumilivu

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22) 
Vile vile una wasiwasi sana juu ya kupungua kwa pesa zako au kufukuzwa kazi, inaonekana pia una wasiwasi mwingi juu ya mtoto kuwa katika taabu huko aliko, au ugonjwa ulionao kama utapona au kama watu uliowaomba msaada watakupigania.toa sadaka mambo yatafunguka

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 23) 
Hivi sasa katika moyo wako una wasiwasi sana kuhusu kuongoka kwa mambo yako, una dhamira ya kusafiri lakini unaona uzito na unataka safari hiyo ifutwe au isiwepo. Kuna ushindani mzito na unataka upate ushindi. Njia nyepesi ni kuwaona wakubwa wataklusaidia.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20) 

Leo una matarajio unayo yangojea unataka yafanikiwe na pana mkutano unaokutia wasiwasi. Kuna marafiki au washirika wako unaotaka sana kukutana nao. Vile vile unafikiria sana juu ya ndugu zako ambao wako katika mgogoro na wanawake au wanaume zao. Jaribu usijiingize katika ugomvi au mgogoro utaadhirika.

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 19) 

Leo katika roho yako unapenda sana kununua kitu cha makelele kama Redio, kuna matatizo au ugonjwa unataka ukuondokee. Na safari ya mbali ije. Hicho unachotaka kununua nunua kipya kilichotumika kitakuletea matatizo, ugonjwa unaokusumbua utapata tiba yake.


IMEANDALIWA NA Mtabiri Maalim Hassan

0 comments:

Post a Comment