Mwandishi Gerald Kitalima
Kocha Mkuu wa timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen kesho Machi 13 atataja kikosi
kitakacho shikana shati na timu ya Morroco katika mchezo utakao chezwa katika
viwanja Kiwanja cha Taifa March 24 mwaka huu Dar es salaam.
Kim poulsen atakutana na waandishi wa Habari katika mkutano utakaofanyika
katika ofisi za shirikisho la mpira wa miguu Tanzania maeneo ya Karume kesho
mida ya saa tano asubuhi.
Kutokana na kuendelea kwa ligi ya vodacom bara na wachezaji wengi kuonekana
kufanya vizuri kesho ndipo tutajua mchezaji yupi alifanya vizuri zaidi mpaka
kuonekana na kupendekezwa kuingia katika kikosi cha taifa kinachoongozwa na
kocha paulsen.
0 comments:
Post a Comment