Wednesday, March 13, 2013

TANZANIA HAITORUDI KWENYE ANALOGIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) IMESEMA KUWA TANZANIA HAITALUDI KURUSHA MATANGAZO KWA NJIA  YA ANALOGIA ILI KUWAFIKIA WATANZANIA WENGI WA KIPATO CHA CHINI WASIO NA UWEZO WA KUNUNUA VINGA’MUZI NA WAKOSAO HAKI YAO YA KUPATA HABARI.

HAYO YAMESEMWA JANA NA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA KUFUATIA MALALAMIKO YALIYOTOLEWA NA UMOJA WA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA (MOAT).


Prof John Nkoma akizungumza na waandishi wa habari
MBALI NA KUPINGA OMBI LA (MOAT) MAMLAKA IMESEMA ITATOA KAULI JUU YA NINI KIFANYIKE KUZINGATIA UWEZO MDOGO WA KIUCHUMI WALIONAO WATANZANIA WENGI AMBAO WANASHINDWA HAWAPATI HAKI YA KUPATA HABARI KUTOKANA NA KUKOSA VINGA’MUZI.

KATIKA KIKAO WALICHOKAA JUZI WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI WALIOMBA MAMLAKA YA MAWASILIANO IRUHUSU MATUMIZI YA ANALOGIA KWA MUDA ILI KUWAPA NAFASI WATANZANIA WALIO NA KIPATO CHA CHINI KUWEZA KUPATA HABARI NA TAARIFA KUPITIA TELEVISHENI BILA VINGA’MUZI.


VILEVILE WAMILIKI HAO WANAHOFU YA KUSHINDWA KUENDESHA VITUO VYA LUNINGA KAMA WAFUATILIAJI WATAKUWA NI WACHACHE.


0 comments:

Post a Comment