Sunday, February 16, 2014

KOCHA WA SIMBA AZIOMBEA MABAYA YANGA,MBEYA CITY NA AZAM

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema ili timu yake iweze kumaliza katika nafasi mbili za juu ni lazima Yanga na Azam zifanye vibaya.
Hata hivyo, Logarusic amesema hajakata tamaa hadi mechi ya mwisho ya msimu kwa sababu atakutana na mabingwa watetezi, Yanga Aprili 27, mwaka huu.

Logarusic alisema sare aliyoipata juzi, Jumamosi dhidi ya Mbeya City imezidi kupoteza matumaini yao ya kuivua Yanga ubingwa msimu huu.

Alisema matokeo hayo mabaya kwa Simba yanatokana na kikosi chake kuwa na baadhi ya wachezaji wasiostahili kuichezea timu hiyo iliyowahi kucheza fainali za Kombe la Shirikisho barani Afrika 1993.

"Niko katika wakati mgumu, ila kuna wachezaji wanaipa timu matokeo mabaya kutokana na kuwa na viwango vya kati vya kuzichezea timu nyingine na si Simba," alisema Logarusic.

Kocha huyo alisema endapo Yanga, Azam na Mbeya City zitafanya vibaya ndiyo Simba itarudi katika harakati za kusaka tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani.

0 comments:

Post a Comment