Vijana Wanne wamehukumiwa katika Mahakama ya Wilaya Singida kutumikia vifungo vya miaka 120 jela kwa
kuteka gari
lililokuwa likisafirisha maiti kutoka mkoani Morogoro
kwenda Musoma mkoani Mara na kupora waombolezaji kompyuta na
fedha.
Waliohukumiwa vifungo hivyo kila mmoja miaka 30 jela ni
Hamis Ali (23), Hamisi Issa (33); Khaldi Hamis (21) na
Abubakari Jumanne (26), wakazi wa Kisaki Manispaa ya Singida.
Mshtakiwa wa kwanza Iddi Omari (38), aliachiwa huru baada ya
mahakama hiyo kukosa ushahidi wa kumtia hatiani. Akisoma hukumu
hiyo, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Flora Ndale, alisema ushahidi
uliotolewa na upande wa mashtaka bila kuacha shaka umethibitisha
washtakiwa hao walitenda kosa hilo.







0 comments:
Post a Comment