Waliokuwa Wachezaji wa
Simba nahodha Juma Kaseja, na Amir Maftah wameanza kujinoa tena na
kikosi cha vijana (Simba B) ili
kujiweka tayari kwa ajili ya
mashindano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati
yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu
jijini Nairobi, Kenya.Baadhi ya wanachama na wadau wa Simba wanapendekeza Kaseja arejeshwe katika timu wakati wa dirisha dogo lakini kipa huyo hakuwa tayari kuelezea chochote.
Mbali na Kaseja ambaye kwa sasa hana timu, jana asubuhi beki wa zamani wa Simba, Amir Maftah,ALIFUMWA akijifua na kikosi hicho kinachofanya mazoezi yake kwenye uwanja wa Mwenge Shooting ulioko Mwenge jijini.
Mara baada ya kufika uwanjani hapo na kuvaa nguo za mazoezi, kipa huyo aliyemaliza mkataba wa kuichezea Simba tangu Juni 30 mwaka huu, aliungana na makipa wanne yosso wa timu hiyo na kuongoza mazoezi.
Akizungumza na gazeti hili, kocha wa Simba B, Selemani Matola, alisema kuwa hawezi kumkataza Kaseja na mchezaji mwingine kufanya mazoezi kwa sababu hana sababu za msingi za kufanya hivyo.







0 comments:
Post a Comment