Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA) limemuidhinisha mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold
Okwi kuchezea klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
Katibu wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa ametoa taarifa muda huu
kwamba, FIFA imewaandikia barua ikiwaambia Okwi ni halali kuchezea
Yanga SC.
“Suala la Okwi
limekwisha, ila siwezi kuzungumza zaidi kwa sasa naingia kwenye
kikao, tutatuma taarifa kwa vyombo vya habari baadaye,”alisema
Mwesigwa.
0 comments:
Post a Comment