Waandaaji
wa Tuzo za Kilimanjaro Music Awards kampuni ya bia ya Kilimanjaro leo
inazindua rasmi mchakato wa kuwapata wakali waliofanya vyema katika
tasnia
ya muziki kwa mwaka 2013.
Kampuni
ya bia ya Kilimnajaro kupitia ukurasa wake wa Face-book na Twitter
wameweka wazi kuwa tuzo hizo zinazinduliwa leo na kutoa nafasi kwa
mara ya wapenzi wa muziki kupendekeza wasanii watakaoingia kwenye
kinyang'anyiro hicho kwa mwaka huu.
“Tuzo
za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014 zinazinduliwa rasmi siku ya
leo. Kwa mara ya kwanza katika tuzo za #KTMA2014
wapenzi wa muziki watapewa nafasi ya kupendekeza wasanii watakaoingia
kwenye kinyang'anyiro.”
Kwa
kusisitiza hilo washabiki wataweza kuchangia mapendekezo yao juu ya
aina gani ya wasanii wanapaswa kushiriki zoezi hilo kupitia tovuti na
njia ya SMS.
0 comments:
Post a Comment