Wednesday, October 15, 2014

KIINGILIO KUONA MECHI YA SIMBA NA YANGA CHAPANDA JUU.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana limetangaza kiingilio cha chini katika mechi ya Ligi Kuu ya Bara kati ya watani wa jadi,
Simba na Yanga inayotarajiwa kufanyika Jumamosi Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwa ni Sh. 7,000.

Kiingilio hicho ni ziada ya Sh. 2,000 kutokana na mechi ya watani hao wa jadi mwaka jana kuwa Sh. 5,000.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura, kiingilio cha juu katika eneo la VIP A ni Sh. 30,000 sawa na cha mwaka jana.

Wambura alisema katika taarifa hiyo kuwa kiingilio katika viti vya rangi ya chungwa ni Sh. 10,000 na Sh. 20,000 kwa eneo la VIP B na C.

Alisema kuwa tiketi za mchezo huo zilianza kuuzwa juzi Jumatatu na ni za elektroniki licha ya maombi yaliyotolewa na klabu hizo kongwe kukataa mfumo huo mpya wa kuuza tiketi msimu huu.

Alisema kuwa mechi hiyo namba 27 itachezeshwa na mwamuzi, Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam ambaye atasaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya na Ferdinand Chacha wa Mwanza na itaanza saa 10:00 alasiri.

0 comments:

Post a Comment