Wednesday, October 15, 2014

AZAM KUIFUATA MBEYA CITY LEO

Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Azam kinatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam leo kuelekea
Mbeya kwa ajili ya kuikabili Mbeya City katika mchezo wao wa ligi utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Habari wa Azam, Jaffer Idd, alisema kuwa wachezaji 20 ndiyo wataondoka kuelekea Mbeya kwa basi lao jipya na safari hiyo itaanza asubuhi.

Idd aliwataja wachezaji ambao hawataondoka kwa vile bado hawajawa 'fiti' ni pamoja na nahodha, John Bocco, Kelvin Friday, David Mwantika, Leonel Preux, Joseph Kimwaga na Frank Domayo.

"Wachezaji ambao hawataenda ni Bocco, Friday na Mwantika ambao sasa wameanza mazoezi mepesi, Domayo naye pia ameanza kujifua na goti limeanza kukunja lakini Kimwaga yeye bado kabisa," alisema Idd.

0 comments:

Post a Comment