Msanii
wa Hip Hop Bongo anewakilisha kipande cha Ilala ChiD Benz amefunguka
leo na kusema kuwa hakuwahi kumpiga Marehemu Ngwear kama ambavyo
amekuwa akikariliwa na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa amewai
kumpiga mwanamuziki huyo enzi za Uhai wake.
Chid
amesema kuwa hizo stori watu wanapozizungumzia zinamuumiza moyo wake
na kumtesa pia na madai yake amesema kuwa kwa mara ya mwisho
alizungumza na Ngwear kwa njia ya Sms japo hakuona ulazima wa
kuliweka wazi.
'Story
za kumpiga marehem zinaniumiza kwa kweli,mara ya mwisho alinitumia
msgs na tukaongea sio lzm tuseme.SIJAWAI KUMPIGA NGWEA alipo anajua”
Chid
Benz ameonesha kuumizwa na maneno ya kuwa aliwahi kumpiga Marehemu na
ndio maana anajaribu kuwaambia watu kuwa hakufanya kitendo hicho na
kusema ya kuwa alipo Marehemu anatambua ya kuwa hajawai kufanya
kitendo hicho.
0 comments:
Post a Comment