Mkazi
Wa Mburahati Jogoo jijini Dar es salaam, Nassor Issa Mohamed(25)
amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya shilingi
milioni tatu kwa kosa la kuwatumia ujumbe wenye nia mbayawa simu ya
mkononi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi na
Inspekta General wa Polisi Said Mwema.
Akitoa
hukumu hiyo hakimu Helen Riwa wa mahakama Kisutu aliiambia mahakama
kuwa Mohamed alisajili kadi zake za simu kwa majina tofauti na kwa
mitandao tofauti kwa nia ya kutumia kadi hizo kutuma ujumbe wa simu
wenye nia mbaya kwa viongozi hao.
Alisema
mshtakiwa alikutwa akiwa na kadi ya simu yenye namba 0759 799956 ya
Vodacom iliyosajiliwa kwa jina la Fadhil Issah, nyingine ya Airtel
0687 521948 iliyosajiliwa kwa jina la Godfrey Joseph na kadi yenye
namba 0687521947 ya Airtel iliyosajiliwa kwa jina la Fadhil Issa.
Hakimu
Riwa aliitaka jamii kutumia kwa uangalifu mitandao kwa kuwani
teknolojia mpya ambapo makosa yake yanakuwa ni mapya na sheria ni
mpya.
Alisema
ametoa adhabu hiyo kwa kutumia Sheria ya Mawasiliano ya kielektroniki
na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 kifungu cha 132 ili iwe fundisho kwa
wote wenye nia ya kufanya makosa kama hayo.
Awali
Mwendesha Mashitaka Ladislaus Komanya aliiambia mahakama kuwa mnamo
Mei 20 mwaka huu taarifa za kiinteligensia zilifikishwa kwa Maafisa
wa juu wa jeshi la Polisi kuwa kuna mtu aliyesajili simuzake kwa
mitandao tofauti anatumia simu hizo kuwatumia ujumbembaya wa simu ya
mkononi Waziri Nchimbi na IGP na baada ya upelelezi ilipobainika kuwa
namba hizo zilikuwa zimesajiliwa kwa majina tofauti.
Alisema
iligundulika kuwa namba hizo zilikuwa zinamilikiwa na mtuhuyo ambaye
jina lake halisi ni Nassor Issah Mohamed
Alisema
Mohamed alikamatwa Mei 25mwaka huu na baada ya mahojiano alikiri
kumiliki kadi ya simu na kwamba ndiyo yeye aliyesajili namba hizo kwa
mitandao tofauti akitumia majina tofauti ili kuficha utambulisho wake
akiwa na lengo lakufanya uhalifu. Mshtakiwa alifikishwa mahakamani
kwa mara ya kwanza Mei 27 mwaka huu na kukiri mashitaka.
0 comments:
Post a Comment