Alianza
kupata umaarufu baada ya kuonesha Mapenzi makubwa aliyonayo katika
Timu yake ya Soka ya Yanga kwa kulia huku akionesha machungu makubwa
aliyokuwa nayo baada ya Timu yake hiyo kukubali kichapo Mabao Matano
kutoka kwa Watani wao wa Jadi Simba.
Kutokana
na watu wengi kupenda aina ya Mapenzi aliyonayo katika Timu yake hiyo
ndipo jamii ilianza kumtambua Steve wa Yanga kupitia Interview ambayo
alifanya na Mtangazaji Millard Ayo kupitia Mtandao wake wa Jamii.
Interview
hiyo ilizidi kuongeza Umaarufu na kulipaisha zaidi jina la Steve wa
Yanga mpaka huko Nchini Kenya ambapo kuna Kituo cha Tv kilifunga
Safari kuja Tanzania na kutengeneza naye Documentary ambayo nayo
ilizidi kumvusha boda na kumuongezea idadi kubwa ya Mashabiki ambao
wengi wao huangua kicheko kutokana na namna alivyona mapenzi ya Kweli
ya Club yake ya Yanga.
Salama
Jabir kupitia Mkasi Show ambayo inaruka katika Ting'a Namba moja kwa
vijana alimuona Steve na kumpa Shavu tena na hii ilitokana na
kukutana na kijna Steve wa Yanga alipokwenda katika Usaili wa Epiq
Bongo Star Search 2013 alipokwenda kuonesha kipaji chake kingine cha
Kuimba mbali na kutoa mchozi.
Kutokana
na kuonekana katika Misukosuko na mihangaiko hiyo Dr Chein Muingizaji
akaona kipaji cha Steve wa Yanga na kuamua kuigiza naye katika Filamu
yake inayokwenda kwa Jina la NIMEKUBALI KUOLEWA ambapo katika Filamu
hiyo mkali Steve wa Kulia amepewa scene ya Kumwaga mchozi pia.
Je
unatka kujionea kipande hicho BOFYA HAPO NA MTIZAME MWENYEWE.







0 comments:
Post a Comment