Mwanamuziki
Lady Jaydee anaetamba na kibao chake cha Joto Hasira katika vituo
mbalimbali vya Radio na Luninga hapa nchini ameomba radhi kwa
mashabiki wake kufuatia kuairisha show yake ya Miaka kumi na tatu
kutokana na msiba uliotokea wa msanii Albert Magwear.
Show
ya mwanadada Jide ilipaswa kufanyika siku ya Ijumaa ya kesho katika
Ukumbi wa Nyumbani Lounge lakini jana kupitia kipindi cha Super Mix
cha East Africa Radio alitangaza kusitisha show yake kupisha taratibu
za msiba kwanza na kusema atatangaza siku baada ya msiba kuisha.
“Tunaomba
radhi kwa watu wote ambao mlikuwa mmeshanunua tickets za miaka 13 ya
Lady JayDee ambapo onyesho ilikuwa lifanyike Ijumaa ya tar 31 May
2013.
Tunapenda kuwataarifu kuwa onyesho hilo limesitishwa kutokana na
msiba mzito wa msanii mwenzetu Ngwair mpaka hapo tutakapo wataarifu
tena”
Akizungumzia kwa wale waliokwisha nunua ticket teyari amesema kuwa wazitunze Tickets hizo kwani ndizo hizo zitakazo tumika siku ya show pindi itapotangazwa siku rasmi.
“Wale mliokwisha nunua tickets naomba mzitunze tickets zenu, kwani ndio hizo hizo mtakazozitumia siku ya show hata kama tarehe imebadilishwa.Natanguliza shukrani na naomba radhi kwa usumbufu wowote nitakaokuwa nimewasababishia,Kila kitu kitaendelea kama kilivyokuwa kimepangwa, hapo baadae”
0 comments:
Post a Comment