Msanii
wa Hip Hop Roma Mkatoliki anaetamba na ngoma yake ya 2030 alieifanya
maalumu kwa ajiri ya mwanae na watanzania kiujumla amefunguka kuwa
watanzania sasa wanahitaji mabadiliko na kama hawawezi kuyapata
mabadiliko ndani ya chama tawala basi watayafuata mabadiliko nje ya
Chama hicho.
“Watanzania
wanataka mabadiliko/ wasipoyaona na wasipoyapata ndani ya ccm
watayatafuta nje ya ccm!Kiongozi bora hawezi toka nje ya ccm”
Mkali
huyo wa miondoko ya Hip Hop mwaka jana katika tuzo za KTM ametiririka
hayo siku moja baada ya wananchi wa Mtwara kufanya fujo na vurugu
zilizosababisha watu kadhaa kupoteza maisha yao huku wengine wengi
wakijeruhiwa kutokana na vurugu hizo na kusababisha uhalibifu wa mali
za watu ikiwa ni pamoja na kuchomwa kwa nyumba za viongozi,kuvunjwa
kwa daraja yote ni katika kupingana na kauli ya serikali juu ya
kutaka kusafirisha Gas kutoka Mtwara na kuipeleka Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment