Rais Jakaya Kikwete amekemea vikali vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza
katika eneo la Kizota, Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema wote
waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali.
Rais
Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini
inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote... “Hivi watu wa Nyarugusu
wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na
watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali
Rais Kikwete.
Rais
Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote wanaoongoza
vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo... “Tutawasaka hawa
watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.”
Alichosema
Waziri Muhongo
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema mradi wa
kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, umeanza
kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda huko wiki ijayo
kuweka jiwe la msingi.
Akiwasilisha
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini jana,
Waziri Muhongo alisema:
“Mradi
wa kujenga bomba la gesi uko palepale na unaendelea kwa kasi na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ataenda kuweka jiwe la msingi wiki
lijalo.”
“Tumezungumza
mengi kuhusu suala hilo na hata viongozi wa watu wa Mtwara
walipelekwa nje kujifunza faida zake, lakini hata kama hawajaelewa,
nimetoa kijitabu kinachozungumzia faida mbalimbali watakazopata wana
Mtwara katika mradi huo.”
Profesa
aliyeanza hotuba yake kwa kueleza machapisho mbalimbali yaliyotolewa
na wizara yake kufafanua faida za gesi ya Mtwara kwa taifa, alisema
mradi huo uliozinduliwa Novemba mwaka jana na Rais Kikwete,
unahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 532 na kipenyo cha
nchi 36.
“Bomba
hilo lina uwezo wa kusafirisha futi za ujazo za gesi milioni 784 kwa
siku. Mradi utahusisha mitambo miwili ya kusafirisha gesi asilia
katika maeneo ya Mnazi Bay- Madimba (Mtwara) na Kisiwa cha Songosongo
(Lindi). Utagharimu Dola za Marekani 1,225.3 milioni,” alisema.
Alisema
kazi za usanifu wa mradi na ulipaji fidia kwa wananchi wapatao 3,092
waliopisha maeneo ya mradi, zimekamilika na hatua za awali za ujenzi
wa mitambo ya kusafirisha gesi asilia zimeanza.
Source
Mwanchi
0 comments:
Post a Comment