Thursday, May 23, 2013

JOKATE KUWASAIDIA WANAFUNZI KUGUNDUA VIPAJI VYAO.


Mwanamitindi Jokate Mwegelo alimaarufu kwa jina la Kidoti ameanzisha program inayolenga kuwasaidia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri darasani na kuwasaidia kugundua vipaji vyao na namna ya kuviendeleza vipajio hivyo wawapo shuleni.

Program hiyo inayokwenda kwa jina la KidotiTime itaingizwa katika ratiba za shule kwa kuanZia itakuwa ni kwa siku 27 kwa mujibu wa Jokate amesema kuwa ameanzia nyumbani kufanikisha mpango huo ambako ni songea.

Jumamosi iliyopita nilikuwa kwetu songea vijijini kama mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michezo ya Umisseta ngazi ya wilaya. Lakini vile vile nilipata nafasi kutambulisha program ya Kidoti Time itakatoingizwa kwenye ratiba za shule takribani 27 kwa kuanzia. Program hii ni kusaidia wanafunzi kujitahidi darasani huku wakigundua na kuendeleza vipaji vyao vingine.

0 comments:

Post a Comment