Msanii
wa muziki wa Rnb pande za Bongo anaetamba na Hits Song kibao japo kwa
sasa kwa ngoma yake ya Jikubali amezidi kujiongezea mashabiki rukuki
kutoka kila pande ya Nchi amekataa kuwa alishawahi jishughulisha na
biashara ya kuuza matunda.
Ben
Paul alikuwa ndani ya Tinga namba moja kwa vijana kupitia ukurasa wa
Facebook akibadilishana mawazo kwa kuchat na Fans zake kupitia
KIKAANGONI LIVE CHAT.alipohojiwa na moja wa Fans wake kuwa alishawahi
kuuza matunda alisema kuwa hajawahi kufanya biashara hiyo kwani muda
mwingi aliutumia kimasomo.
'”Hahaha
si kweli, maisha yangu kabla ya muziki yalikuwa shuleni tu,
kuanzia
1997 mpaka 2010”
kwa
mujibu wa Ben Paul amesema kuwa mbali na muziki kwa sasa anasoma na
kufanya biashara zake za hapa na pale zinazomuwezesha kuendesha
maisha yake na familia yake kiujumla na kumfanya kuendelea kuwa Ben
Paul,
baada
ya kutaka kujua mpango wake katika muziki Ben PAUL alieleza kuwa
anampango wa kuanzisha Band ya kwake mwenyewe ambayo atakuwa
akiitumia kufanya nayo kazi na kufanya Live Shows kwa Band yake
mwenyewe ambayo anatarajia itakuwa teyari mpaka itapofika mwezi
September.
“ndio
nina mpango wa kufanya collabo na wasanii wakubwa kimataifa na
nimeshaanza kuwatumia demos wasanii mbalimbali wa afrika mashariki,
natumai nitajibiwa muda si mrefu, kuhusu bendi yes niko kwenye
maandalizi mpaka kufikia september mwaka huu naamini nitakuwa
nimefanikisha”
0 comments:
Post a Comment