Kipa wa Simba Ivo
Mapunda Ameshangazwa na Kipa Mwenzake wa Yanga Juma K Juma kutokana
na Kipa huyo wa Yanga kutompa mkono wa salamu walipokuwa
Uwanjani
mbele ya Wageni Rasmi.
Kabla ya kuanza kwa mchezo huo
uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, Kaseja
aligoma kumpa mkono Ivo wakati wachezaji wa timu zote mbili
wakisalimiana mbele ya Mgeni Rasmi wa mchezo huo, Waziri wa Sheria na
Katiba, Mathias Chikawe ambaye alikuwa amefuatana na Rais wa
Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamali Malinzi na Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro, George Kavishe.
"Soka ni sehemu nzuri ya
kukutanisha watu, nimekutana na Kaseja uwanjani na nilitegemea
atanipokea vizuri kama Mtanzania na mchezaji mwenzake, lakini
amenishangaza sana kwa kuninyima mkono," alisema Ivo.
"Sijawahi
kutukanana wala kuwa na mgogoro wowote na Kaseja.
Alichokifanya
ni picha mbaya kwa wapenzi wa soka, hasa watoto ambao wanatuangalia
sisi (wachezaji) kama kioo chao,"
0 comments:
Post a Comment