Katika
kile kinachoonekana kupania kupata ushindi dhidi ya Simba Jumamosi,
kikosi cha Mbeya City kinafanya mazoezi mchana wa jua kali Mbeya
kujiandaa
kwa mechi hiyo.Akizungumza kwa simu kocha wa timu hiyo, Juma Mwambusi alisema wako katika maandalizi makali kwa ajili ya mechi zao tisa zilizobaki kukamilisha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
"Tunaendelea na programu za mazoezi na muda huu (saa 6:31 mchana) nazungumza nawe nasimamia programu za mazoezi ya timu. Sisi (Mbeya City) hatufanyi mazoezi kwa ajili ya Simba, bali tunajiandaa kwa mechi zote zilizobaki msimu huu," alisema Mwambusi.
0 comments:
Post a Comment