Wednesday, February 12, 2014

YANGA KUWAFUATA COMORO KESHO BILA KASEJA

Timu ya Young Africans Sports Club wawakilishi wa Tanzania bara kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kesho watakwea pipa saa 6 kamili mchana
kuelekea Visiwa vya Comoro tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Komorozine de Domoni utakaofanyika siku ya jumamosi katika Uwanja wa stade International Said Mohamed Cheik  Mitsamiouli.

Msafara unatarajia kuwa na watu 30 wakiwemo wachezaji 19 Benchi la Ufundi saba (7) pamoja na viongozi wanne (4)
 
Magoli kipa ni: Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez"



Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani na Rajab Zahir



Viungo: Athuman Idd "Chuji", Frank Domayo "Chumvi", Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga na Hamis Thabit



Washambuliaji: Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, Saimon Msuva na Mrisho Ngasa 




0 comments:

Post a Comment